Envaya

DAKAWA ECONOMIC DEVELOPMENT ORGANIZATION.Inakaribisha wabia wa maendeleo kwa jamii katika kufanya nao kazi ili kufikia lengo la kuanzishwa kwa asasi.Miongoni mwa shughuli ambazo asasi inafanya ni;

UTEKELEZAJI WA MIRADI YA HIFADHI YA MAZINGIRA KATIKA MILIMA YA ULUGURU.

DAKEDEO Kwa ushirikiano na shirika Rafiki la MUUNGANO MAZINGIRA ORGANIZATION.Linachukua fursa ya kuhakikisha kuwa jamii inaishi katika matarajio yasiyo na mashaka,maisha yasiyo na woga wa kushambuliwa na matatizo na majanga yasababishwayo na uharibifu wa mazingira.

Kwa ushirika huo wa mtazamo wa kimaendeleo DAKEDEO Imehakikisha kuwa wataalamu wake wa sekta ya mazingira wanafanya kila jitihada za kuhakikisha kuwa jamii ya watu wanaoishi katika vyanzo vikuu vya maji na uoto asilia ambao haujavamiwa unawekwa katika ulinzina mpango mkakati wa kuuendeleza.

MUUNGANO MAZINGIRA ORGANIZATION Iliendesha mradi wa mafunzo wa "KUWAJENGEA UWEZO WANACHAMA NA JAMII MBINU BORA ZA KILIMO MITI" Katika milima ya Uluguru.Mradi huo umefadhiliwa na KAMPUNI YA SIGARA TANZA

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 MAFUNZO YA AWALI KIDATO CHA KWANZA YASHIKA KASI.

Kituo cha elimu ya kujitegemea na mafunzo ya ujuzi kwa jamii (DAKAWA CENTRE FOR SELF RELIANCE AND SKILL DEVELOPMENT-DCSSD)KINAENDELEA NA MAFUNZO YA AWALI KWA KIDATO CHA KWANZA. ambayo yalianza mwezi november 2013.

Katika kuhakikisha kuwa kituo kinawajenga vema wanafunzi kwa ajili ya kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2014 kituo kimeandaa Safari ya Mafunzo katika Hifadhi za Taifa za UDZUNGWA zilizopo katika wilaya ya Kilombero ziara itakayofanyika katika kipindi cha mwezi wa Disemba.

Ziara hiyo ya mafunzo inakusudia pia kuonesha jinsi asasi ya Uchumi na maendeleo Dakawa.(DAKAWA ECONOMIC DEVELOPMENT ORGANIZATION(DAKEDEO)ambayo ndio inayosimamia kituo cha (DSSDC) katika ushiriki wake wa kukuza utalii wa ndani kwa jamii ambao kwa kiasi kikumbwa haujaeleweka vema kwa jamii.

Asasi inakaribisha wadau ambao ni wakereketwa wa maendeleo ya elimu katika jamii kushiriki katika kufanikisha ziara hiyo ya mafunzo.

 MRADI WA UHIFADHI WA MAZINGIRA.

DAKEDEO itaanzisha  mradi wa hifadhi ya mazingira katika maeneo ya vijiji vilivyopo wilaya ya Mvomero katika kipindi cha mvua za masika 2014.

Mradi huo wenye mfumo shirikishi jamii katika hifadhi za mazingira unahusisha kuanzishwa kwa vitalu maalum vya miche ya miti ambapo aina ya miche kumi na mbili itahusishwa katika uzalishaji wake katika vitalu.

Miche hiyo itazalishwa  na DAKEDEO Ikishirikiana na asasi rafiki (CBO)'

Baada ya kuzalishwa kwa miche hiyo kutakuwepo na utaratibu wa kuipanda katika mashamba yanayomilikiwa na watu binafsi pamoja na asasi za kijamii ambapo wamiliki watahusika na utunzaji wake.

Mradi hhuo utahusisha njia bora za kitaalamu zenye gharama nafuu za kiuendeshaji katika miiradi ya uzalishaji mali lakini yenye tija kubwa katika kipato.

DAKEDEO Itasimamia mpango huo katika shughuli zifuatazo.

(i)Kutoa elimu /kuwajengea uwezo wanajamii mbinu za uhifadhi wa mazingira kwa mfumo wa kilimo miti.

(ii)Kuotesha miche pamoja na kusambaza kwa wadau washiiiriki katika mradi.

(iii)Kutoa huduma za kitaalamu katika kuhudumia mashamba hayo.

(iv)Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya mradi.

(v)Kutafuta wdau na wafadhili wa miradi ya uhifadhi wa mazingira ili washirikiane na wadau wanajamii katika uhifadhi.

DAKEDEO inakaribisha wadau mbali mbalimbali katika kushiriki katika mpango wa uhifadhi wa mazingira.

  

UTEKELZAJI WA MIRADI YA MWAKA 2016/2017.

Maelekezo ya mpango mkakati 2015-2020 wa DAKEDEO. Asasi inakaribisha wadau wa maendeleo kushiriki katika uandaaji na uwezeshaji wa miradi ifuatayo:

I- Utafiti juu ya ufahamu duni wa huduma za afya kwa wazee.

II. Usimamizi na uboreshaji wa miradi ya utunzaji wa mazingira kwa kuimarisha kilimo miti kwa mpango wa jamii kwa jamii na kilimo na rafiki.

III. Mpango maalum wa miradi ya kuondoa umasikini wa kipato kwa katika ngazi ya kaya.

IV. Elimu maalum kwa vijana wanawake na watoto waishio katika mazingira hatarishi.

V. Uhamasishaji jamii juu ushiriki wao katika uimarishaji wa afya ya jamii ikiwemo ushiriki wa mpango wa damu salama.

VI. uendeshaji wa TAMASHA la SANAA NA mAONESHO LA MAKABILA YALIOMO KATIKA WILAYA YA MVOMERO MKOA WA MOROGORO.

VII. Miradi ya elimu ya kujitegemea na ujenzi wa ujuzi kupitia vituo vya DAKAWA CENTRE FOR SELF RELIANCE AND SKILLS DEVELOPMENT katika wilaya za Mvomero, Morogoro mjini, Morogoro vijijini, Kilosa Gairo  na Baadhi ya maeneo ya pembezoni katika mkoa wa Tanga. 

 

 


 MRADI WA ELIMU YA MPIGA KURA.  2020.

DAKEDEO. Kwa ushirikiano na TUME YA UCHAGUZI YA TAIFA ITAENDESHA MRADI WA UTOAJI ELIMU YA MPIGA KURA KWA WAPIGA KURA UCHAUZI WA RAIS, WABUNGE NA MADIWANI 2020.

ELIMU HIYO ITATOLEWA KWA MWONGOZO WA ELIMU YA MPIGA KURA WAKATI WA UCHAGUZI MKUU 2020 KAMA AMBAVYO UMETOLEWA NA TUME YA TAIFA YA  UCHAGUZI.

MRADI HUU UTAANZA DISEMBA 1/2020 HADI TAREHE 27/10/2020.

Kufuatana na mwongozo wa uchaguzi katika kipindi hiki Elimu kwa jamii itajikita katika mabo ya msingi yafutayo:-

1- KAMPENI ZA UCHAGUZI NA MAADILI YA UCHAGUZI.

2- KUPIGA KURA, KUHESABU KURA NA KUTANGAZA MATOKEO.

3. VITI MAALUM VYA WANAWAKE.

4.MAKOSA YA UCHAGUZI.

Katika mada hizo hapo juu mabo mbali mbali yataongelewa, kufundishwa na kujadiliwa. 

Mradi utafikia jamii kupitia mbinu mbali mbali ikiwemo mikutano ya kijamii, mikutano rasmi na wadau mbalimbali wa uchaguzi.

Ama Vyombo vya habari na mitandao ya kijamii itafikiwa katika kufikisha elimu hii kwa jamii. tembelea barua pepe dakawaeconomicdevorganization.facebook / twitter account dakawaeconomic.twitter