Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Chama cha michezo cha viziwi -Tanga kilianzishwa mwaka 2009 kwa juhudi za viziwi wenyewe baada ya kututoshirikishwa kikamilifu na kutokuwa na chombo cha kuwatetea na kudai haki zao katika sekta ya michezo mbalimbali mkoani Tanga.kwa muda mrefu mkoa wa Tanga umekuwa na wanamichezo viziwi ambao walikuwa katika vilabu mbalimbali lakini uwepo wao na ushiriki wao katika vilabu hivyo ulikuwa haupewi kipaumbele kutokana na wahusika katika vilabu hivyo kutowapa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao hivo viziwi wanakuwa hawafanikiwi wala kufika mbali katika tasnia ya michezo.CHAMIVITA kilianzishwa na msukumo wa viziwi kwa ushrikiano mkubwa na afisa utamaduni wa halmashuri ya jiji la Tanga ambaye amekuwa bega kwa bega na viongozi wa CHAMIVITA na kuhakikisha kuwa viziwi wanakuwa na chombo cha kuwaunganisha katika michezo.

MAFANIKIO KWA MWAKA 2012

Kwa mwaka huu 2012 CHAMIVITA Kimefanikiwa kufanya mikutano na wanachama wa wilaya 4 za mkoa wa Tanga ambazo ni Tanga,Muheza,Korogwe,na Handeni. Na katika mikutano hii CHAMIVITA inatoa mafunzo juu ya SERA YA TAIFA YA MICHEZO kwa ufadhili wa shirika la FOUNDATION FOR CIVILI SOCIETY (FCS) lengo la mafunzo hayo ni kuwajemgea uelewa viziwi juu ya utekelezaji wa sera ya Taifa ya michezo najinsi ya kuwafanya wawe na ufahamu wa kufutilia sera hizo ikiwemo utekelezaji wake. pia CHAMIVITA kimemfanikiwa kujenga mahusiano na vyama vingine vya michezo mkoani TANGA