Envaya
  • UTUME WA CHAVITA-MISSION

  

CHAVITA itahakikisha kuwa jamii ya viziwi ina maisha bora, inayojijengea uwezo wa kujiamini, kujithamini, kujiendeleza, kukuza lugha ya alama ya Tanzania na kushiriki kikamilifu katika shughuli zote za kimaendeleo, kiuchumi na kijamii kwa kushirikiana na serikali na taasisi nyingine.”

                                                      

  • DIRA YA CHAVITA-VISION

  

CHAVITA itahakikisha kuwa jamii ya watanzania inawatambua, inawakubali, inawathamini, inawashirikisha viziwi na kuhakikisha hawasumbuliwi na umasikini, unyanyasaji, ubaguzi na ukandamizaji wa aina yoyote”

 

  1. MALENGO YA CHAVITA

 

Kama wanajamii, viziwi wanayo haki ya kuchangamana na watu wengine na kushirikishwa kikamilifu katika shughuli za jamii. Hii ni haki ya msingi ya binadamu. CHAVITA itahakikisha hili kwa:

 

  • Kuhamasisha matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi popote walipo hapa Tanzania, jamii ya watanzania, taasisi na serikali kuhusu haki za Viziwi.
  • Kupigania usawa katika fursa za elimu, huduma za jamii na nyanja zote za maisha ya binadamu.
  • Kupigania kutambulika kisheria kwa Lugha ya Alama ya Tanzania.
  • Kujenga mwamko na kukuza matumizi ya Lugha ya Alama kwa matawi ya CHAVITA, jamii ya Viziwi nchini, na kwa jamii ya watanzania kwa ujumla.
  • Kuhakikisha shughuli za maendeleo ya jamii na ki-uchumi kwa matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi nchini zinaboreshwa.
  • Kuhakikisha matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi nchini wanapata uwakilishi katika ngazi zote za uongozi.
  • Kufanya na kuendeleza utafiti kuhusu masuala yanayowahusu Viziwi
  • Kupambana na Virusi vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI pamoja na majanga mengine yanayowakabili Viziwi.
Mabadiliko Mapya
CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA (CHAVITA) WILAYA YA KONDOA imehariri ukurasa wa Historia.
Ilianzishwa kama klabu ya viziwi ambayo watu walikuwa wanaidharau na kusema ni machizi (vichaa) – Baadae ikaanzishwa kikundi cha viziwi likijulikana kama kikundi cha viziwi kondoa (kiviko). – Baadae CHAVITA) mkoa Dodoma walitoa mafunzo ya lugha ya Alama (L.A.T)katika tawi la wilaya ya kondoa ndipo likaanzishwa CHAMA CHA... Soma zaidi
10 Desemba, 2012
CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA (CHAVITA) WILAYA YA KONDOA imeongeza Habari.
Chavita imetoa mafunzo ya Lugha ya Alama kwa Taasisi za serikali na Wazazi wanaoishi na Watoto Viziwi katika kata 5,ambazo ni Bereko,Kondoa mjini,Pahi,Kilimani na Chemchem katika Wilaya ya Kondoa. Mafunzo ya lugha ya alama kwa Taasisi za... Soma zaidi
10 Desemba, 2012
CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA (CHAVITA) WILAYA YA KONDOA imeumba ukurasa wa Mkuu.
UTUME WA CHAVITA-MISSION CHAVITA itahakikisha kuwa jamii ya viziwi ina maisha bora, inayojijengea uwezo wa kujiamini, kujithamini, kujiendeleza, kukuza lugha ya alama ya Tanzania na kushiriki kikamilifu katika... Soma zaidi
10 Desemba, 2012
CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA (CHAVITA) WILAYA YA KONDOA imeongeza Habari.
Jamii yetu ifahamu matumizi ya lugha ya Alama kuwe na uwiano wa mawasiliano kati yetu (viziwi na jamii nyingine). – Kutetea haki ya viziwi kwa vyombo ya usalama,mahakama na polisi ili kuwatambua jamii ya viziwi. – Kujenga ushirikiano na taasisi (asasi) mbalimbali ili kuwawezesha kulitambua kundi hili. ... Soma zaidi
27 Aprili, 2012
CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA (CHAVITA) WILAYA YA KONDOA imeongeza chama cha viziwi tanzania kwenye orodha yake ya Mashirika ya Ubia.
22 Desemba, 2011
CHAMA CHA VIZIWI TANZANIA (CHAVITA) WILAYA YA KONDOA imeongeza Habari.
Kuna changamoto kubwa katika kundi letu la Viziwi kutokutambulika hata Vijijini kutokujua hasa umuhimu wa watoto Viziwi kwenda kupata elimu ya awali,msingi na sekondari na hata Ufundi.Na changamoto zingine Viziwi wanatakiwa kuwezeshwa ili wafikie malengo yao ya milenia mpyaViziwi wengi tuko nyuma kimaendeleo lisha ya kuwa... Soma zaidi
22 Desemba, 2011
Sekta
Sehemu
Kondoa , Dodoma, Tanzania
Tazama mashirika ambayo yapo karibu