Ni jambo linaleta faraja kubwa kwa kiongozi kwenye busara kuwa karibu na wananchi wake kujua changamoto zinazowakabiri,kuzungumza kulingana na mazingira wanayoishi,kwani zipo semi mbalimbali zinenazwo"kama hatutaweza kukaa karibu nao tukazungumza nayo,na wao kuwa karibuni nasi na kuzungumza nasi,hata nasi kamwe tuwezi tukazungumza tukaelewana.
Kiongozi wa kweli kuonyesha mfano,kwa kuzungumza na watu wake bila ya kujali dini,rangi au utaifa wake,hiyo ndio chimbuko la maendeleo ya kweli kwa kuifanya dunia kuwa mahali pa amani,pasipo na mfarakano na masengenyo.
Viongozi wa serikali wanajukumu kubwa la kuwahamasisha wananchi kuchangia maendeleo yao,Miongoni mwa viongozi hao ni Mhe.Mbunge wa Bagamoyo Dk Shukuru Kawambwa ambaye ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi stadi amekuwa mstari wa mbele katika kukakikisha maendeleo yanapatikana katika jamii.
Mkurugenzi Mtendaji wa CHACODE,Thadei Hafigwa,Akimkabidhi Mjane wa Jamii ya Kimasai msaada wa fedha kwa ajili ya ada ya mtoto wake,aliyesimama katika ni Mtendaji wa Kijiji cha Kihangaiko Idd Simba
Maisha ya Kijiji,wakati mwingine kutokana na ukosefu wa vifaa mbalimbali vya kurahisisha shughuli zako za kila siku za kujiongezea kipato kama vile trekta,plau dhana inayotumika katika kilimo au jembe la kukotwa kwa Ng'ombe au wanyama pia hata hukosa mwevuli wa kujikinga na mvua pindi mvua inyeshapo,hutumia jani la Mgomba kujikinga na mvua,hapa Mkurugenzi Mtendaji wa CHACODE,Thadei Hafigwa ili kuendana na mazingira ya Kijiji amelazimika kutumia Jani la Mgombea kujikinga na mvua.
Kiwango cha maisha ya watanzania walio wengi ambao huishi vijijini wanajenga nyumba zao kwa kutumia dhana za asili,nyasi zinatumika kujenga na kuezeka.Tanzania ina safari ndefu ya kuhakikisha ya kuwa kila mtazania anaishi katika nyumba bora na ya kisasa,mlo wake si wa kubahatisha,watoto wanakwenda shule,wanafunzi wanafundishwa vema na walimu wao walioandaliwa mazingira mazuri ya kufundisha.
baadhi ya maeneo vijijini wanajikuta bado wanatumia kinu na mche kutwanga nafaka ili waweze kupata unga utakaotumika kuandaa chakula chao,hii inatokana kukosekana na kwa wawekezaji wa kupeleka mashine za kusaka nafaka.
Hii ni hatua mbalimbali katika kufanya tafiti mbalimbali ikiwemo hali ya mazingira na uharibifu wa uoto wa asili.
Juhudi mbalimbali zinafanywa na serikali lakini kutokana na kuwepo kwa changamoto mbalimbali za maendeleo taarifa nyingi jamii hasa wa vijijini wanakosa kuzipata.Asasi ya CHACODE imedhamiria kuwa kiungo
madhubuti katika kuongea na wananchi kujua kero na changamoto zao ili kujenga utetezi kwa mamlaka husika.
ASASI ya CHACODE iliweza kufanya utafiti katika masuala ya kuhifadhi mazingira na mambo ya kale.Jambo hili limetokana na tabia ya mapokeo waliokuwa wakiitumia wazee katika kuridhishana na kupeana taarifa na kumbukumbu mbalimbali za matukio ya kihistoria,mila na desturi utaratibu ambao kwa sasa umeanza kufutika kutokana na kukua kwa teknolojia ya mawasiliano na kumbukumbu.
Asasi imechukua jukumu la kufanya utafiti mdogo juu ya wazee wa kale walivyoweza kuwa na uwezo wa kufanya matukio ya kihistoria ambayo kwa uwezo wa kawaida ni vigumu kutafanya.Kwa mfano kutumia kisigino cha mguu kuweka mchoro kwenye mwamba wa jiwe na kuweka alama ambazo haziwezi kufutika.
Jambo hilo limetokea katika mkoa wa Morogoro Wilaya ya Morogoro vijijini katika eneo la makutano ya mto Mngazi na Mtombozi.Mkurugenzi Mtendaji wa CHACODE Thadei Hafigwa aliweza kufika katika eneo hilo na kufanikiwa kushuhudia michoro hiyo inayosadikiwa kuchorwa na wazee wa Kabila la Waluguru Mkoani Morogoro Miongo kadhaa iliyopita
Viongozi wa serikali ni wadau wakubwa wa maendeleo na asasi zisizo za kiserikali kwa kuwa lengo ni moja kuhakikisha ya kuwa wananchi wanapata maendeleo katika maeneo yao na kuzikabili changamoto mbalimbali wanazokutana nazo wakati wa kutekeleza majukumu yao
Mkurugenzi Mtendaji wa CHACODE Thadei Hafigwa akiwa studio ya RFA akielezea jambo kuhusiana na utendaji wa asasi yake