Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

Mradi wa Uoteshaji na Upandaji miti

 Uharibifu wa mazingira ni uzoreteshaji wa mazingira kwa njia ya kupungua kwa rasilimali kama vile hewa, maji na udongo; uharibifu wa ikolojia na kupotea kwa wanyamapori. Kama inavyoonyeshwa na formula hii I=PAT , athari za mazingira (environmental impact, I) au uharibifu unasababishwa na muunganiko wa kuongezeka kwa idadi ya watu (increasing human population, P), kuongezeka kwa shughuli za kiuchumi (per capita affluence, A), na matumizi ya technolojia ya viwanda (polluting technology, T). Kwa ufupi Uharibifu wa mazingira ni kupungua kwa uwezo wa mazingira kuhudumia mahitaji ya kijamii na ikolojia.

Uharibifu wa mazingira ni moja ya vitisho kumi yalioonywa na Umoja wa Mataifa. Uharibifu wa mazingira ni wa aina nyingi. Wakati makazi asili yanaharibiwa au maliasili kutumiwa vibaya, tunasema kuwa mazingira yanaharibiwa.

Uharibifu wa mazingira kutokana na shughuli za kiuchumi
Mabadiliko ya mazingira na afya ya binadamu:- Sehemu maalum katika Raslimali za Dunia 1998-99, inaeleza jinsi magonjwa yenye uwezo wa kuzuiwa na vifo vya mapema bado huzidi kuongezeka kwa idadi kubwa. Ikiwa kuna marekebisho makubwa katika mabadiliko ya mazingira, afya za binadamu zinaboreka pia, mamilioni ya watu wangeishi kwa muda mrefu,na maisha yenye afya nzuri kuliko awali.


Katika maeneo masikini katika dunia inakadiriwa kuwa mmoja katika watoto watano hawataweza kuona siku yao ya kuzaliwa ya tano, hasa kwa sababu ya magonjwa yanayohusiana na mazingira. Watoto Milioni kumi na moja duniani kote hufa kila mwaka hasa kutokana na malaria, shida ya kupumua au kuhara - magonjwa ambayo yanaweza kukingwa.
Njia nzuri na nyepesi ya kuhakikisha mazingira yetu yanaboreka ni kupanda miti.

WAENDELEE inaendelea kupanda miti ili shughuli zingine za kiuchumi ziweze kufanyika kwa ufanisi zaidi na shughuli inayounganishwa moja kwa moja na ustawi wa misitu ni Ufugaji nyuki.

Upandaji miti (Afforestation) ni upandaji wa mbegu au miti ili kutengeneza misitu katika eneo ambalo halijawahi kuwa na msitu hivi karibuni, au ambalo halijawahi kuwa na msitu kamwe.  Upandaji miti au mbegu unafanywa ili kuirejesha misitu baada ya kuondolewa katika eneo, kwa mfano wakati miti imekatwa kwa sababu za utengenezaji wa mbao.


Serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali kama WAENDELEE hujihusisha moja kwa moja katika mipango ya upandaji miti ili kurejesha misitu na kusaidia kuhifadhi viumbe tofauti ambavyo viko hai.

Ufugaji wa nyuki (NYUKI NI KILIMO):-Zaidi ya asilimia 80 ya Watanzania hujikimu kupitia kilimo. Ni asilimia 17 pekee ya ardhi nchini Tanzania inayofaa kwa kilimo. Kutokana na ukosefu wa nafasi na kuwepo kwa watu wengi uharibifu wa mazingira ni jambo ambalo haliwezi epukika. Hii ndio sababu katika sehemu hii ya ufugaji wa nyuki, tunaangalia njia za kutunza na kuhifadhi udongo na maji ili kuimarisha uzalishaji na kulinda mazingira.


Ufugaji wa nyuki ni shughuli muhimu inayosaidia jamii kujipatia mapato ya ziada ili kuboresha maisha yao. Nchini Tanzania, takriban asilimia 90 ya ardhi inafaa katika ufugaji wa nyuki.
Ufugaji wa nyuki ni mfumo wa kilimo unaohimili na wenye manufaa kwa mazingira. Ufugaji wa nyuki huwapatia watu walio ndani ya umaskini mapato ya ziada ya mara kwa mara, husaidia mazingira na huwa na manufaa mengine mengi.


(ii)  Madhumuni
Kupunguza umaskini wa kipato na uboreshaji wa mazingira kupitia ufugaji wa nyuki na upandaji miti Wilaya ya Singida Vijijini.


(iii)  Matarajio yanayotegemewa

  • Kushiriki kikamilifu kwa wananchi kwenye upandaji na ufugaji nyuki
  • Kurudisha uoto wa asili tuliokuwa tunauona siku na miaka ya nyuma na upatikaji wa uhakika wa  maji.
  •  Kuongeza kipato kwa wanajamii wa Singida Vijijini kupitia ufugaji wa nyuki lakini pia shughuli za kilimo na ufugaji zitaboreka zaidi.
  • Kuweka mfumo endelevu wa wanajamii wote wa kutunza mazingira kupitia vikundi mbalimbali kama shule, SACCOS, vijana, akina mama n.k.
  • Kuimarika kwa afya na kuondoa maradhi ambayo yanaweza kuzuilika kwa kuimarika kwa mazingira.


(iv) Viashiria vya mafanikio

  • Kufanyika kwa ufanisi upandaji miti, mradi ulioko mbele yetu
  • Kuenea kwa elimu na uelewa wa utunzaji miti na mazingira kwa ujumla kwa jamii na maeneo yanayopandwa miti.
  • Kuongezeka kwa uoto wa asili utakaombatana na upatikanaji endelevu wa maji.
  • Hamasa ya kufuga nyuki miongoni mwa jamii yetu
  • Ukuaji wa bidhaa za nyuki kutoka Singida.



(v) Shughuli Kuu

  1. Kufanya semina mbali mbali kwa wanajamii kuwaongezea na kuboresha uwezo wao katika uzalishaji mali.
  2. Kutambua, Kuhimiza na kutumia na  ubadilishaji wa uzoefu wa utaalamu mbalimbali wa wanachama wote walioko kwenye jumuiya na jamii iliyoko Singida kwa maendeleo ya maeneo yetu na Taifa kwa ujumla.  
  3. Kuhimiza uhusiano wa wataalamu wetu na shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazofanyika Singida Vijijini ili kuongeza ushiriki wa utaalamu wao kwenye fani mbalimbali kufanikisha malengo ya maendeleo.
  4. Kutoa msaada wa kitaalamu kwenye shughuli mbalimbali kwa maendeleo ya Wilaya yetu.
  5. Kutambua maeneo yenye mapungufu makubwa ya kimaendeleo na kushiriki kwenye utatuzi wake kwa kushirikiana na mamlaka zinazohusika.


(vi) Wanaonufaika na mradi
Mahitaji ya kuendeleleza mazingira ya Wilaya yetu ni muhimu kwa wananchi wote wa Wilaya, kwa hiyo wananchi wote ni wadau wakuu kwenye mradi huu na unawanufaisha kwa kuwezesha shughuli za kiuchumi kufanyika kwa ufanisi mkubwa.