Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

Kituo hiki kilianzishwa tarehe 16/3/2010 na kupata usaji wake tarehe 13/1/2012(CAP.318 R.E.2002) Lengo ni kuwaunganisha Waislam wote kuwa kitu kimoja kwa kila jambo linalogusa Waislamu na Uislamu na kuweza kushiriki katika maendeleo ya kukuza Elimu ya Akhera,Elimu ya Duniani na kukuza uchumi katika kuinua kipato na kushiriki katika shughuli za kijamii  kwa kushirikiana  waslamu wote bila ubaguzi.                                                      Kituo hiki kilianzishwa na Vijana na baadhi ya Wazee wa Kislamu wanaoishi Jijini Dar es salaam kutokana na Wingi wa Waslamu wa Vuga waishio Dar es salaam                                      Kituo kilianza na wanachama 30 wanaume 18 na wanawake 12 na mpaka sasa kituo kinawanachama 301. Makao Makuu ya Kituo yapo Kijiji cha Bazo Kata ya Vuga Tarafa ya Soni Halmashauli ya Bumbuli Wilaya ya Lushoto Mkoa wa Tanga