Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations
shirika lilianza mwaka 2011 mwezi June ,katika kijiji cha KIKUKWE kata ya KANYIGO
Shirika hili limeanza baada ya kuona uhitaji wa vijana katika vijiji vilivyopo katika mkoa wa kagera kwani vijana wengi baada ya kuitimu elimu katika viwango mbalimbali wamekuwa wakiishi maisha ambayo si mujarabu kwa maisha ya binadamu na hii ni kutokana na kukosa elimu ya ujasilia mali.
Shirika hili lilipogundua hali hii likaamua kuwakusanya vijana na kuzungumza nao juu ya kujikwamua katika mambo mbalimbali yakiwemo yale yanayonekana katika ukurasa mkuu wa shirika.
Mwanzilishi wa shirika hili ni ndugu BERNARD KISHAMBA ambaye ni mwalimu kwa taaluma lakini pia amesomea masuala ya maendeleo ya fedha na uwekezaji katika chuo cha maendeleo vijijini DODOMA (IRDP)