Fungua
Temeke Youth Development Network

Temeke Youth Development Network

Temeke/Chang'ombe, Tanzania

Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

VIJANA TANZANIA TUNAELEKEA WAPI?

Temeke Youth Development Network (Dar-es-salaam)
10 Aprili, 2013 16:31 EAT

Habari ndugu zangu?natumaini mu wazima wa afya tele.Kwanza nianze kwa kuwapongeza sana vijana wote Tanzania ambao kwa namna moja ama nyingine,wanapolala na kumka wanajiuliza maswali ya msingi kama ifuatavyo"mimi ni nani?, kwa sasa nipo wapi?naelekea wapi?nitafikaje ninakotaka kwenda? najua yapo maswali mengi na ya msingi kama haya ambayo kwa kweli kama vijana tunapaswa kujiuliza.

Kwa kweli mi niseme tu nimechoka na masuala ya kulalamika,kwa kuwa ni muda mrefu tumelalamika lakini ni mangapi umefanikiwa wewe mwenyewe kuyokana na kulalamika.Haiwezekani wote tuwe wanasiasa lakini pia kila mtu ana uwezo na ujuzi wake kwa namna moja ama nyingine.Mara ngapi tumejihadi kuhakikisha kuwa angalau kila siku tunaongeza jambo katika yale tunayoyaweza? Sasa tuseme baasi nimechoka na sasa nataka nijiendeleze mwenyewe kwa kaadili ninavyoweza ili niweze angalau kuchangia jambo katika familia,jamii na nchi yangu.

Sasa kuna tatizo kubwa la ajira,lakini pia taarifa kutoka ILO zimebainisha kuwa kutakuwa na tatizo kubwa la ajira katika miaka michache ijayo mara mbili ya kadilio la sasa.Na hii inatokana na kuwa vijana wengi sasa wanamaliza elimu ya sekondari na vyuo.Suala la ajira sasa si tu linahitaji elimu ya juu lakini pia ubunifu na uzoefu zaidi katika eneo ambalo unalifanyia kazi.Hakuna muda ambao masuala ya ubunifu yanahitajika kama sasa.

Vijana tumejiandaaje na tunaelekea wapi?au ndo kutwa kuchambua masuala ya mwenendo wa nchi na masuala ya uchumi hata kama si wanachumi.Uchambuzi wa masuala ya siasa hata kama sisi zio wanasiasa, kuchambua masuala ya sheria hata kama sisi sio wanasheria.

Tunaelekea wapi?Wote tunaweza kuwa wabunge?Wote tunaweza kuwa Mawaziri jamani?

tunaelekea wapi? dira yetu n nini? tunataka tuweje please tell me.


Ongeza Ujumbe Mpya

Karibisha watu kushiriki