Envaya
Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri
TEYODEN: WAAHIRISHA MDAHALO WA VIJANA LEO

Kutokana na kuwepo kwa mkutano wa vijana unaohusu changamoto zinazowakabili vijna katika shughuli za ujasiriamali ulioandaliwa na One Stop Youth Centre ( OSYC) cha Dar Es Salaam,leo TEYODEN haitakuwa na mdahalo wa vijana hadi wiki ijayo na mada itakuwa ni ileilie ilyokuwa ikiendelea wiki mbili zilizopita.Hivyo vijana wote na wadau mbalmbali mliokuwa mmealikwa kwa ajili ya kutoa ufafanuzi kuhusiana na mapambano dhidi ya ukimwi na changamoto zake mnaombwa radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

Vijana zaidi ya 40 wa TEYODEN leo wataungana na vijana wenzao kutoka katika wilaya za Kinondoni na Ilala pale katika ukumbi wa Karimjee katika kuzijadili changamoto zinazowakabili katika suala zima la ujasiriamali ili kujikomboa kiuchumi.
5 Juni, 2010
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.