Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri
TEYODEN YASHIRIKIANA NA WILAC KUJENGA UWEZO WA VIJANA KUKABILIANA NA UKATILI DHIDI YA WANAWAKE.
Katibu waTEYODEN mwenyekiti na Mkurugenzi wa WILAC wamefanya kikao cha makubaliano ya ushirikiano ili kuwezesha vijana kuchukua majukumu katika kuhakikisha kuwa matatizo ya ukatili dhidi ya wanawake katika Halamashauri ya Manispaa ya Temeke unapungua.
Mwenyekiti wa TEYODEN alimwambia Mkurugenzi wa WILAC kuwa mradi huu unahitajika sana kwetu Temeke kwa kuwa asilimia zaidi ya 60 wanawake wanaofanyiwa ukatili huu ni vijana kati ya miaka 15-35 ambao ni umri ambao TEYODEN unaufanyia kazi.WILAC na TEYODEN tutashikiana kwa muda wa miezi 6.
Pichani ni vijana wa Kata ya Tandika mara baada ya kutoka kwenye mafunzo:-
24 Januari, 2017
Maoni (2)
Kazi nzuri kwenu TAYODEN, Pongezi kwenu kwa kuwa wadau wakubwa katika harakati za kutokomeza ukatili wa kijinsia nchini.
Harakati za pamoja zinahitajika zaidi katika kuhakikisha Usawa katika nyanja zote muhimu unazingatiwa.