Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

TEYODEN NA TRA MAKAO MAKUU WAFANYA MAFUNZO KWA VIJANA 100, KUHAM ASISHA URASIMISHAJI WA BIASHARA NA ULIPAJI WA KODI.

Tunasema kuwa hakuna wakati ambao vijana wanahitaji kuongeza juhudi za kujiajiri wenyewe kuliko kipindi hiki.Vijana wengi sasa wameanzisha biashara ili waweze kukidhi mahitaji ya kila siku ya maisha.

Upo umuhimu mkubwa wa vijana kupata elimu mbalimbali ili waweze kundesha biashara zao vizuri ikiwemo elimu ya ujasiriamali,stadi za masha,umuhimu wa usajili wa biashara na ulipaji wa kodi.Mafunzo haya huwafanya waweze kufanya biashara kwa utaratibu na kufuata sheria na kupunguza hatari za kuchukuliwa kama wanavunja sheria na kuhadhibiwa.

Mtandao wa vijana Manispaa ya Temeke(TEYODEN) na Tanzania Revenue Athority(TRA) tumeshirikiana kuwezesha mafunzo ya siku 1 kwa vijana 100 wafanyabiashara kutoka kata 30 za Manispaa ya Temeke.Mafunzo haya yamefanyika katika ukumbi wa Chuo cha utalii,kilichopo Tandika,Temeke Dar-es-salaam.Pamoja na mambo mengine vijana walijifunza umuhimu wa kusajili biashara,umuhimu wa kulipa kodi na elimu ya ujasiriamali.

TRA na TEYODEN tutaendelea kuelimisha wafanyabiashara vijana ndani na nje ya Temeke ili kuwawezesha kufanya biashara kwa uhakika na kuleta tija kwao na kwa vijana wengine.

April 11, 2013
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.