Mafunzo ya project management Naivasha Kenya yatakuwa chachu ya mabadiliko ya vijana kuelekea ujasiriamali na utengenezaji ajira binafsi kwa vijana.
Siku 8 za mafunzo ya uendeshaji wa miradi yaliyoandaliwa kwa ushirikiano na ILO y2y fund pamoja na UNHABITAT youth fund zimebadilisha mtazamo wa mameneja 10 kutoka Tanzania.Mameneja hao kwa sasa, wanafikiria kuboresha miradi 10 ambayo ILO wameichagua kati ya miradi 103 iliyoombwa katika mfuko huo wa vijana kwa mwaka 2012.miradi ya mwaka huu imegusia maeneo ya taka ni pato,ulimaji wa mboga mboga kwa njia za kiasili,uongezaji wa thamani katika mazao ya chikichi,uvunaji wa asali,uboreshaji wa sabuni za maji na utengezaji wa batiki,uboreshaji wa bidhaa za ngozi,new chips vending,uboreshaji wa mazao ya muhogo kutengeneza biskuti.
Mameneja watakuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa miradi inakwenda vizuri na kutoa ajira kwa vijana nchini Tanzania.
Mafunzo yalikusanya mameneja wa miradi kutoka nchi za Togo.benin,zambia,kenya uganda,malawi.kongo,Tanzania,mauritius,misri na nyingine nyingi.
Hata hivyo mifuko hiyo itaendeleo kuwezesha vijana barani afrika na kwingineko kuwawezesha vijana kuongeza ajira binafsi kwa kuwa tatizo la ajira rasmi na zenye tija limekuwa ni kubwa sana.
Maoni (3)