TAARIFA YA KIKAO NA MAAZIMIO YALIYOFIKIWA KATI YA POVERTY FIGHTING TANZANIA NA TEYODEN
TAREHE: 02/10/2012.
LENGO LA KIKAO:KUJADILI NAMNA YA KUSHIRIKIANA KATIKA KUPUNGUZA UMASIKINI WA KIPATO KWA VIJANA KUPITIA MPANGO WA VICOBA KATIKA MANISPAA YA TEMEKE.
MAHALI KIKAO KILIPOFANYIKA:OFISI ZA PFT-TANDIKA MTAA WA KITUNDA PLOT NO:38,TEMEKE.
WALIOHUDHURIO:
- Issa Mohamed Tunduguru -PFT
- Hassan Mohamed Pwemu –TEYODEN
- Abela Kamulali -TEYODEN
- Yusuph Kutegwa -TETODEN
- Kasali Mgawe -TEYODEN
- Emmanuel Kwilasa - PFT
- Robert Duma - PFT
AGENDA ZILIZOJADILIWA/MADA ZILIZOJADILIWA
- KUANZISHA USHIRIKIANO KATI YA PFT NA TEYODEN KATIKA KUPUNGUZA UMASIKINI WA KIPATO KWA VIJANA
- TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA
- USHIRIKI WA VIJANA KATIKA VIKUNDI VYA UZALISHAJI MALI/VIKUNDI VYA KUWEKA NA KUKOPA/VIKUNDI VYA SHUGHULI ZA KIUCHUMI.
- MENGINEYO
Kikao kilifunguliwa na Mkurugenzi mtendaji wa shirika la POVERTY FIGHTING TANZANIA kwa kuwakaribisha wageni na kisha kutoa nafasi ya kujitambulisha kwa kila mjumbe aliehudhuria kikao.
Wajumbe wote walipata nafasi ya kujitambulisha na baada ya hilo,Mkurugenzi wa PFT alitoa nafasi ya kuendelea na agenda zilizokuwa mezani.
- KUANZAISHA USHIRIKIANO KATI YA PFT NA TEYODEN KATIKA KUPUNGUZA UMASIKINI WA KIPATO KWA VIJANA.
Agenda ya kwanza ilianza kwa Mkurugenzi kutoa maelezo kwa ufupi juu ya wito uliotolewa kwa TEYODEN kufika ofisi za PFT ili kujadili juu ya mambo muhimu kwa mstakabali wa vijana wa Tanzania hususan ni Manispaa ya Temeke.
Mkurugenzi alieleza namna PFT inavyoendesha programu ya VICOBA kama njia ya kukabiliana na umasikini wa kipato miongoni mwa jamii.Alieleza jinsi ambavyo programu hii imekuwa chombo cha kuwaunganisha wanajamii kupitia vikundi vyao vya vicoba ambapo hukutana kila wiki kwa ajili ya kununua hisa pamoja na mambo mengine kujadili masuala mtambuka kama vvu/ukimwi.
Lakini pia jinsi ambavyo familia zenye kipato cha chini kinavyoweza kumudu kujikimu katika maisha ya kila siku.Ilielezwa kuwa mfumo huu wa vicoba unawanufaisha wanakikundi pia katika kujifunza mambo yanayo husu maana ya vicoba na umuhimu wake kwa watu wenye kipato cha chini na hasa kwa wale wasio weza kumudu kupata mikopo kutoka katika taasisi za kifedha ambazo mara nyingi huhitaji kuwa na dhamana pamoja na mashariti mengine ambayo humfanya mtu wa kipato cha chini kushindwa kupata mikopo,ilielezwa namna mwana kikundi jinsi anavyonufaika na elimu ya utawala bora katika vikundi vyao vya uzalishaji mali,mambo ya kibenki na kujengewa uwezo katika mambo mbali mbali ikiwemo elimu ya ujasiriamali na namna ya kuendesha biashara ndogo ndogo na za kati.
Hata hivyo kabla ya kumaliza kutoa maelezo kwa kifupi juu ya programu zinazoendeshwa na PFT,mshauri mwelekezi wa PFT alipewa fursa ya kusoma takwimmu zinazoonyesha asilimia ya vijana waliojiunga katika mpango huu wa VICOBA unaoratibiwa na PFT.
Mshauri mwelekezi alitoa takwimu zikionyesha kwamba kati ya vikundi 115 vya VICOBA ambavyo tayari vimeshaanzishwa ni asilimia 32% ya wanachama vijana wenye umri wa kuanzia miaka 18-35 walio katika programu ya vicoba.Aidha ni asilimia 17 tu ya wanachama wa vicoba ambao ni wanaume.
Nafasi iliyotolewa kwa wajumbe kutoka TEYODEN ili waeleze shughuli za mtandao wa vijana.Katibu wa TEYODEN alieleza shughuli zinazofanywa ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya stadi za maisha kwa vijana,programu ya VVU na ukimwi,afya ya uzazi(Reproductive health),ujasiriamali kwa wasichana waliopata mimba za utotoni(Young mothers in financial involvement),kuwawezesha vijana kukabiliana na mazingira hatarishi na sanaa kwa maendeleo(SMK).Katibu wa mtandao aliendelea kueleza kuwa TEYODEN ina vituo vya vijana katika kila kata nk.
Hata hivyo TEYODEN walieleza jinsi ambavyo wamefanikia kuanzisha SACCOS ya vijana ambayo tayari imeanza kazi.
Mwenyekiti wa TEYODEN aliushukuru uongozi wa PFT kuwakaribisha na kupongeza kwa kufikiria na kuona inafaa kufanya kazi kwa pamoja na hasa kwa kuliangalia tatizo la vijana na umasikini.Alisema hili ni wazo zuri ambalo kwayo likitiliwa mkazo litakuwa ni moja ya njia ya kuwasaidia vijana wanaoelemewa na lindi la umasikini na ukosefu wa ajira.
Baada ya maelezo hayo kwa ufupi kuhusu kazi zinazofanywa na PFT na TEYODEN,wajumbe walikaribishwa kuendelea na mjadala ili kuona ni namna gani tunaweza kushirikiana kwa pamoja ili kuweza kuwashirikisha vijana kwa wingi katika kuunda vikundi vya kiuchumi na kuweza kuzitumia fursa zilizopo kupitia mbinu binafsi(Self initiatives).
Baadhi ya changamoto zilizotolewa na mjumbe kutoka TEYODEN alisema,Kuna haja ya kuangalia namna ya kubadilisha mtizamo wa vijana (Mind-set) ili ushiriki wa vijana katika mambo ya maendeleo uwe na tija,mfano alisema leo hii vijana wakiitwa kwenye semina ya kuwanufaisha wao bado kwa sehemu kubwa watataka walipwe,pasipo malipo huenda wasihudhurie kabisa au wasiendelee na semina,nyingine ni kwamba vijana wana fani zao lakini hawazifanyii kazi.
Mjumbe mwingine kutoka mtandao wa vijana alisema vijana hawana mitaji,vijana wanahitaji mafanikio ya haraka haraka,lakini pia kufuatia takwimu zilizopatikana kutoka PFT wakati wa zoezi la kutambua uwiano wa wanachama wa VICOBA kwa umri wao na jinsia zao (Sex and Age distribution),ilifahamika kuwa ni asilimia ndogo sana ya vijana walioko katika vikundi vya vicoba,je wengine wako wapi?je ni kwanini vijana wengi hawajiungi na makundi ya kichumi/uzalishaji mali?
Baada ya majadiliano marefu pande mbili kati ya PFT na TEYODEN wajumbe walikubaliana kuwa kuna haja ya kuanzisha ushirikiano wa pamoja kuitumia programu ya vicoba kama chombo cha kuwakwamua vijana kutoka katika lindi la umasikini wa kipato.
- TATIZO LA AJIRA KWA VIJANA
Kufuatia wimbi la vijana wengi wanaoingia katika soko la ajira kuwa kubwa (angalia jedwali)
Residence |
Age Group |
||||
15-24 |
25-34 |
35-64 |
65+years |
Total |
|
Urban areas (Including Dar es salaam) |
9.3 |
3.0 |
1.0 |
1.1 |
3.7 |
Rural |
1.2 |
0.9 |
0.3 |
0.3 |
0.7 |
Total |
3.1 |
1.5 |
0.5 |
0.4 |
1.5 |
Source:Intergrated Labour Force Survey(ILFS) 2006 (NBS,2007 b)
Agenda hii ilizungumzwa kwa upana wake na wajumbe huku wakiangalia uwiano wa ajira katika sekta iliyo rasmi na sekta isiyo rasmi.Takwimu zinaonyesha sekta isiyo rasmi ndio inayotoa ajira kwa vijana wengi na kwa ujumla wake takwimu zinataja kuwa sekta isiyo rasmi inaajiri 63% zaidi ya ajira zilizo katika sekta rasmi,hivyo wajumbe walijadili namna gani vijana wanaweza kujiajiri au kuajiriwa katika sekta isiyo rasmi.
Changamoto zilizobainishwa na wajumbe ni pamoja na ukosefu wa mitaji,ukosefu wa elimu ya ujasiliamali,kutokuwa na sehemu rasmi za kufanyia shughuli zao,ushiriki mdogo wa kuunda vikundi vya kiuchumi/uzalishaji mali,Je ni kwa kiwango gani vijana wanashiriki katika kuandaa sera mbalimbali zinazohusu maisha yao kwa ujumla?na je ,ushiriki wa vijana wa kawaida katika masuala ya sera una umuhimu gani?vijana kuwa na mawazo ya kuajiriwa nk.
Wajumbe walijadili kwa kuzingatia uhalisia wa vijana ambao wengi wapo kwenye mtandao wa vijana kutokuwa na fursa za kushiriki katika shughuli za uchumi.
Maazimio
1) PFT na TEYODEN washirikiane katika kukuza ajira kwa vijana kupitia sekta isiyo rasmi,kwa kuunda vikundi vya kiuchumi/uzalishaji mali ili vijana wengi zaidi waweze kujiajiri,vikundi hivi vitajengewa uwezo kiuchumi kwa kuwashirikisha vijana katika vikundi vyao vya kiuchumi ili waweze kupata mitaji kupitia mikopo itakayotolewa kwenye vikundi vya vicoba.
2) PFT na TEYODEN iiombe idara ya vijana manispaa Temeke na ngazi ya wizara kushirikiana na wizara ya viwanda na biashara kuhamasisha vijana kuijua na kuitumia,sera ya maendeleo ya vijana na sera ya wajasiliamali wadogo na wa kati ili vijana iwawezeshe kuwapatia mwongozo na dira katika kutekeleza shughuli zao kwa ufasaha na pia kuifanya itumike ipasavyo.
3) Kuiomba wizara ya kazi na ajira iandae sera ya ajira na sheria za kazi kwa sekta isiyo rasmi ambapo vijana wengi wanaajiriwa huko.
4) Kuhamasisha matumizi ya mfuko wa vijana unaotolewa na serikali ili utumike kama chachu na nyongeza ya mitaji kwenye vikundi vya vicoba vya vijana vitakavyoratibiwa kwa ushitika kati ya PFT na TEYODEN.
5) Kuhamasisha urasimishaji wa shughuli/biashara za vijana/wanyonge ili ziweze kutumika kama dhamana ya mikopo kutoka vyanzo vingine vya mapato (Mkazo utawekwa kwenye kuhamasisha MKURABITA.
6) Kuimarisha mfumo wa mafunzo ya kuwajengea uwezo vijana katika stadi mbali mbali ikiwemo stadi za ujasiriamali,usimamizi wa fedha na biashara nk
7)
- Ushiriki wa vijana katika vikundi vya kiuchumi/uzalishaji mali
Kufuatia ushiriki mdogo wa vijana katika vikundi vya kukopa na kuweka,vikundi vya VICOBA wajumbe walijadili kwa kina ni kwa nini vijana wengi hawashiriki katika vikundi vya vicoba,vikundi vya kuweka na kukopa.
Baadhi ya sababu zilizobainika kutokana na majadilianao ya wajumbe ni kwamba vijana wengi wana haraka ya maendeleo ya ghafla,na hivyo kushindwa kwenda sambamba na mifumo mbali mbali ya kuweka na kukopa ikiwemo vicoba ambapo utaratibu huchukua muda kidogo hadi kufikia kuanza kukopeshana,hii hupelekea vijana kutokuwa na shauku ya kujiunga,kutokuwa na uvumilivu wa kuanza shughuli za uzalishaji mali/biashara kwa kianzio/mtaji mdogo,kukosa elimu ya ujasiriamali nk
Pia vijana wengi imebainika kutokuwa na habari hata juu ya mfuko rasmi wa vijana ambao ungeweza kusaidia kuwa chanzo cha fedha kutunisha mitaji yao ama kukopeshana kupitia vikundi vyao.
Kutokuwa na elimu ya kuunda vikundi na kuvisimamia,kujiendesha,kujua utawala na namna ya uchaguzi wa shughuli za kufanya za uzalishaji mali.
Maazimio
1) Kupanga mkakati madhubuti wa kuwahamasisha vijana washiriki katika vikundi vya kiuchumi
2) Kuandaa mpango maalumu wa mafunzo wa kuwajengea uwezo vijana ili wapende na waweze kushiriki katika vikundi vya uzalishaji mali.
3) Kuwaelimisha vijana juu ya kupanga mipango yao ya maendeleo kwa kuweka mipango ya muda mfupi,mipango ya muda wa kati na mipango ya muda mrefu.
4) Kuwafuata vijana huko waliko kwenye mitaa yao ili kuwapelekea mpango huu wa VICOBA itakayokuwa ni chombo cha kuwafanya wakutane kila wiki na kubadilishana uzoefu na mbinu na kuwa chachu ya wengine kuunda vikundi.
4.Mengineyo.
Agenda hii iliweka muafaka wa kukutana tena katika siku itakayo pangwa ili kuona hatua itakayofuata katika kupanga namna ya kuanza kutekeleza programu hii itakayo kuwa imejielekeza kwa vijana.
Ilikubalika kwamba kabla ya kuanza kazi italazimika kuandaa mkataba wa makubaliano(Memorandum of agreement) utakao eleza makubaliano hayo kati ya PFT na TEYODEN,Nini cha kufanya,mgawanyo wa majukumu na mambo mengine muhimu yatakayo saidia kutekeleza programu hii kwa ufanisi.
Mwenyeketi wa TEYODEN alifunga kikao kwa kuwashukuru wote waliohudhuria,namna michango ya mwazo na mijadala ilivyokuwa na tija na pia alishukuru PFT kwa kuleta wazo hili na hasa kuwashikisha TEYODEN.
Kikao kiliahirishwa mnamo saa 7:38 mchana mpaka hapo kitakapo itishwa tena.