Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

TEYODEN YAFANYA MAFUNZO REJEA KWA MENTORS MRADI WA KUJENGA UWEZO WA KINAMAMA WADOGO WALIOSAHAULIKA.

TEYODEN imefanya mafunzo rejea ya siku 3 kwa mentors(walimu wa wasichana) 16 kutoka kata za Azimio,Kibada,Vijibweni na Mtoni.Mentors hawa hapo awali walipatiwa mafunzo ya satdi za maisha,elimu ya ujasiriamali na mafunzo ya uwezeshaji ili waweze kuwa walimu,waangalizi lakini kama walezi kwa wasichana 80 katika kata 4 za mradi kama zilizokwisha taja hapo juu.

katika tathimini ya TAMASHA iliyofanywa na mwakilishi wa TAMASHA katika Mradi huu bi Aziza ulikuta mapungufu kidogo kwa walimu hawa ikiwemo uwezo usiridhisha katika utoaji wa masomo kwa wasichana ngazi ya kata za mradi.Hivyo ufumbuzi wa haraka ulionekana ni kuwarusha katika mafunzo ya hatua ya pili ili kukazia hasa katika eneo la mbinu za uwezeshaji.

Mwisho wa mafunzo haya ya siku 3  wawezeshaji rika(mentors) walijiwekea mipango kazi yao ili kuwezesha kufanya kazi kwa urahisi na kwa mwelekeo wa pamoja.

Mategemeo ya TEYODEN ni kwamba wasichana wataboresha shughuli zao ili tuwawezeshe kupata mitaji ya kuanzisha na kuboresha shughuli zao za  kiuchumi.

TEYODEN inategemea kuwapa kiasi cha sh 8,000,000/= sawa na sh 1,000,000 kwa kila kikundi.Kila kata inavikundi 2 vya wasichana 10 kila kimoja.

March 31, 2012
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.