TANZANIA_DAIMA.pdf TEYODEN YAZINDUA MAJUKWAA 12 YA VIJANA KATIKA KATA ZA SANDALI,TANDIKA,YOMBO VITUKA,AZIMIO,MAKANGARAWE,MJIMWEMA,KIBADA
CHARAMBE,KIMBIJI,SOMANGILANA CHANG'OMBE ZOTE ZA MANISPAA YA TEMEKE.
TEYODEN imezindua majukwaa ya vijana katika kata 12 zilizotajwa hapo juu kama hatua ya kwanza ya robo ya pili ya mradi wa kuongeza ari ya uwajibikaji,ushiriki na ushirikishwaji wa vijana katika shughuli za kijamii na maendeleo Manispaa ya Temeke.katika midahalo hii wastani wa vijana 123 walifikiwa katika kata zote 12 za mradi.Lengo hasa la uzinduzi wa majukwaa haya ya vijana ni kuwezesha vijana katika kata za mradi ni kuwa na maeneo na nafasi huru za kujadili masuala mbalimbali ikiwemo uwajibikaji,ushiriki na ushirikishwaji wao katika masuala muhimu.Lakini pia kupata nafasi ya kujadili changamoto za maisha na jinsi ya kukabilina na changamoto hizo.
Mafanikio yaliyopatikana katika shughuli hii ni pamoja na kupokelewa vizuri na watendaji wa kata hizi lakini vijana waliyapokea majukwaa haya kwa moyo mmoja kama vile walikuwa wanayasubili kwa kipindi kirefu.Vijana katika siku moja ya uzinduzi huu walipata nafasi ya kujadili dhana nzima ya uwajibikaji,ushiriki na ushirikishwaji.
Vijana katika baada ya uzinduzi walikubaliana kufanya vikao vya majukwaa haya mara 4 kwa mwezi huku wengi wakipendekeza siku za mwisho wa wiki kuwa ni nzuri zaidi kwa vikao
Watendaji wa kata katika kata 12 za mradi walikubali kutoa kumbi za ofisi za kata ili zitumike kwa shughuli hizo za vikao vya jukwaa na kuwataka vijana wengi kushiriki.
Maoni (1)