Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

FCS Narrative Report

Introduction

Tanzania Chamber of Commerce Industry and Agriculture - Mtwara Branch
TCCIA Mtwara
Kuimarisha ushiriki wa Jamii Kufuatilia Matumizi ya Fedha na Raslimali za DADPs/PADEP Mkoa wa Mtwara.
FCS/MG/1/11/104
Dates: Januari 01, 2012 hadi Machi 31, 2012Quarter(s): Kwanza
Muhidin Swalehe
S.L.P. 376
Mtwara
Simu: +255 787 193 774
+255 715 193 774
Nukushi: +255 23 2333 807
Barua Pepe:

Project Description

Governance and Accountability
Mradi huu unakidhi eneo la ufadhili la Utawala Bora na Uwajibikaji kwa kuwa umelenga kujenga na kuimarisha ushiriki wa jamii katika kufuatilia matumizi ya fedha na raslimali za umma zinazotengwa na Serikali na Washirika wa Maendeleo kwa ajili ya kuboresha sekta za kilimoa na mifugo. Fedha na raslimali hizo ni zile zinazoletwa kupitia Mipango ya Kuendeleza Kilimo Wilayani (District Agriculture Development Projects - DADPs) na Mipango Shirikishi ya Kilimo na Mifugo (Participatory Agricultural Development Programme - PADEP).

Mradi utawezesha kujenga uwezo kwa wadau tofauti wa maendeleo kuhusu mbinu na stadi za kukusanya taarifa na takwimu; kufanya uchambuzi, uandishi wa taarifa na utoaji wa mrejesho kwa wadau kuhusu mafanikio; mapungufu, changamoto na nini kifanyike ili kuimarisha mafanikio yaliyopatikana, kuboresha mapungufu yaliyojiri na yaliyopo na kutatua changamoto mbalimbali ili kuona kwamba Uwazi, Uwajibikaji na nidhamu ya matumizi ya Fedha na Raslimali za Umma kwa ajili ya wakulima na wafugaji vinakuwepo kupitia DADPs na PADEP. Mradi utatekelezwa katika Halmashauri 6 za Wilaya na Manispaa za Mkoa wa Mtwara ambazo ni; Mtwara Manispaa, Mtwara Vijijini, Tandahimba, Newala, Masasi na Nanyumbu kwa muda wa miezi kumi na miwili (Mwaka mmoja) kuanzia Januari hadi Desemba, 2012.
RegionDistrictWardVillagesTotal Beneficiaries
MtwaraMtwara Manispaa - -10246
MtwaraMtwara Vijijini - -10246
MtwaraTandahimba - -10246
MtwaraNewala - -10247
MtwaraMasasi - -10247
MtwaraNanyumbu - -10247
 Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
Female186318630
Male372637260
Total558955890

Project Outputs and Activities

1.1. Warsha 2 za siku 1 zimefanyika kwa viongozi/watendaji 60 wa Halmashauri za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara na uelewa wao kuhusu mradi wa PETS umeongezeka

2.1 Wawakilishi 60 wamepata uelewa juu ya dhana ya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na rasilimali za Umma (PETS) za sekta za kilimo na mifugo DADPS/ PADEP) katika halmashauri 6 za wilaya za mkoa wa Mtwara

3.1 Kamati 6 za PETS zimeundwa na ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS) za sekta za kilimo na mifugo DADPs / PADEP katika mamlaka za serikali za Mitaa za Mkoa wa Mtwara umefanyika.

4.1. Kufanyika kwa uchambuzi wa taarifa na takwimu zilizokusanywa kutoka Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara na taarifa za mirejesho zimeandikwa na zimekamilika.

5.1. Mikutano 6 ya mirejesho ya taarifa za PETS imefanyika katika Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara kuhusu matumizi ya fedha katika sekta ya kilimo/mifugo kupitia DADPs/PADEP.

6.1. Kuchapishwa na kusambazwa kwa Mabango 1800, Vipeperushi 3000, Fulana 300 vyenye ujumbe wa PETS na kurushwa kwa vipindi 4 vya Radio kuhusu dhana ya PETS na kuongezeka kwa uelewa na ushiriki wa jamii.

7.1. Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara zimefanyiwa ufuatiliaji wa maendeleo ya utekelezaji mradi wa PETS kwa fedha za DADPs/PADEP

8.1. Kufanyika kwa mkutano shirikishi wa tathmini ya mwisho wa utekelezaji wa mradi kwa kushirikisha walengwa/wadau 40 toka halmashauri 6 za wilaya manispaa za Mkoa wa Mtwara

1.1.1. Kufanya warsha ya siku 1 katika awamu 2 kwa viongozi/watendaji 60 wa Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara kuelezea malengo ya mradi wa ufuatiliaji (PETS)

2.1.1. Kufanya mafunzo ya PETS kwa wawakilishi na kubainisha kamati za kufuatilia matumizi ya fedha na rasilimali za umma (PETS ) kwa kila halmashauri 6 za wilaya / manispaa za mkoa wa Mtwara ifikapo Novemba 2011.

3.1.1. Kuchapisha na kusambaza Mbango 1800, Vipeperushi 3000, Fulana 300 vyenye ujumbe wa kuhamasisha jamii kufanya PETS na kurusha vipindi 4 vya Radio juu ya dhana ya PETS ifikapo Juni, 2012.

4.1.1. Kufanya ufuatiliaji na tathmni za maendeleo ya utekelezaji wa mradi na mwelekeo wa ufikiwaji malengo katika Halmashauri 6 za Wilaya/Manispaa 6 za Mkoa wa Mtwara.



1. Kufanyika kwa warsha ya siku 1 katika awamu kwa viongozi /watendaji 60 wa Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara na kuelezewa kwa malengo ya mradi wa ufuatiliaji (PETS)

2. Kuendeshwa kwa mafunzo ya kujengwa uwezo kwa wadau 60 tofauti wa maendeleo juu ya dhana ya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS) na kubainishwa kwa kamati za PETS kwa kila Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara.

3. Kuchapishwa na kusambazwa kwa wadau tofauti wa PETS; Mabango 1800, Vipeperushi 3000, Fulana (T-shirts) 183 katika Halmashauri 5 za Wilaya za Mkoani Mtwara na Manispaa ya Mtwara Mikindani.

4. Kufanyika kwa ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya utekelezaji mradi na mwelekeo wake wa ufikiwaji malengo katika Halmshauri 5 za wilaya na manispaa ya Mtwara Mikindani.

Shughuli ya mafunzo ya kujenga uwezo wa wadau tofauti na kuunda Kamati za PETS kwa kila wilaya ililazimu kufanyika katika vituo vitatu badala ya 2 ili kuongeza ufanisi kufuatia makosa yaliyobainika katika bajeti kwamba hakukuwa na fedha iliyotengwa kwa ajili ya posho ya washiriki wa mafunzo husika. Hali hiyo ilipelekea mafunzo kufanyika, Masasi Mjini, Newala Mjini na Mtwara manispaa badala ya Masasi na Mtwara pekee ili kuongeza ufanisi pasipo kupoteza mantiki ya mradi.
1. Mkutano na watendaji/viongozi kuelezea malengo ya mradi:- (TZS. 2, 866,000/=)

2. Mafunzo kwa wadau tofauti kuhusu PETS:- (TZS. 7,860,000/=)

3. Kuchapisha na kusambaza machapisho tofauti:- (TZS. 5,462,000/=)

4. Ufuatiliaji na tathmini ya mawndeleo ya utekelezaji wa mradi:- (TZS. 746,000/=)

5. Ununuzi wa vifaa na samani mbalimbali ya uendeshaji mradi:- (TZS. 4,534,550/=)

Project Outcomes and Impact

1. Kuimarika na kuboreka kwa upatikanaji na ubora wa huduma za kigani za kilimo na mifugo katika Halmashauri 6 za Wilaya/Manispaa za Mkoa wa Mtwara.

2. Kuongezeka kwa uelewa na ushiriki wa jamii katika kufuatilia matumizi ya fedha na rasilimali za umma (PETS) zinazotengwa na Serikali kuinua sekta ya kilimo kupitia DADPs / PADEP.
1. Kuongezeka kwa uelewa wa viongozi/watendaji 60 wa Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara kuhusu dhana na dhima ya Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha na Raslimali za Umma (PETS) hususan miradi ya DADPs/PADEP.

2. Kuongezeka kwa maarifa, mbinu na stadi kwa wadau 60 tofauti wa maendeleo wa Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara katika kufanya Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha na Raslimali za Umma (PETS) hususan katika sekta ya Kilimo/Mifugo kupitia miradi ya DADPs/PADEP.

3. Kuundwa kwa Kamati 6 za Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha na Raslimali za Umma (PETS) kwenye Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara.

4. Kusambazwa kwa machapisho mbalimbali yenye ujumbe na kuongezeka kwa uelewa wa jamii na mwamko wa kushiriki za Halmashauri 6 za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara katika Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha na Raslimali za Umma (PETS) katika sekta ya Kilimo/Mifugo na nyinginezo.
Mafunzo ya kujenga uwezo kwa Kamati za PETS yamefanyika katika vituo vitatu vitatu vya; Masasi, Newala na Mtwara Manispaa badala ya viwili vya; Masasi na Mtwara Manispaa ili kuleta ufanisi zaidi pasipo kupoteza mantiki na malengo ya mradi.
Kuwezesha kuwafikia walengwa wa mradi katika maeneo yao na kutatua changamoto ya bajeti kukosa fungu la posho ya kujikimu kutokana na makosa ya kiufundi wakati wa kuandaa bajeti ya mradi (posho ya kujikimu kusahaulika)

Lessons Learned

Explanation
Dhana na dhima ya PETS bado haifahamiki kikamilifu miongoni mwa watendaji/viongozi wa serikali pamoja na wananchi kiujumla.
Wananchi wanahitaji kujengewa uwezo zaidi hususan katika ngazi za kata na vijiji ili waweze kufanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na raslimali za umma katika maeneo na ngazi wanamoishi.
Watendaji/viongozi wa serikali za mitaa bado wana mtazamo potofu kwamba kufanya ufuatiliaji wa matumizi na raslimali za umma (PETS) ni sawa na kufanya ukaguzi jambo ambalo sio sahihi.

Challenges

ChallengeHow it was overcome
Bajeti ya mradi kukosa (kusahaulika) kipengele cha posho ya kujikimu kwa washiriki wa mafunzo kwa kamati za PETS.Kuendesha mafunzo katika vituo 3 badala ya 2 vilivyopendekezwa ili kuwasogelea washiriki na hivyo kutolazimu kuwalipa posho ya kujikimu.
Watendaji/viongozi wa serikali za mitaa waliohudhuria warsha ya kuelezea malengo ya mradi kudai kulipwa posho kwa viwango vya serikali.Kuwaelimisha na kuwaelekeza kwamba mfadhili (FCS) hazingatii viwango vya posho za serikali na kwamba wana mwongozo wa uombaji na utoaji ruzuku kwa wadau (AZAKi) na unapaswa kuzingatiwa.
Washiriki wa mafunzo ya kujenga uwezo katika kufanya ufuatiliaji (PETS) kudai kiwango cha posho hakitoshelezi kukidhi haja na mahitaji ya hali ya maisha ya sasa.Walielekezwa kwamba viwango vya malipo yote vilivyopo ni kwa mujibu wa bajeti na makubaliano ya Mkataba kati ya FCS na TCCIA Mtwara wa kutekeleza mradi husika.

Linkages

StakeholderHow you worked with them
Maafisa Kilimo, Mifugo, Mipango na Wachumi wa Halmashauri za wilaya/manispaa 6 za Mkoa wa Mtwara.Kuhudhuria warsha ya kujenga uelewa na kuelezea malengo ya kufanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha na raslimali za umma (PETS) katika sekta ya Kilimo/Mifugo.
Waandishi wa HabariKuhudhuria mafunzo ya kujenga uwezo kwa kamati za PETS na kutangaza/kuhabarisha wananchi kuhusu taarifa mbalimbali za mradi.
Wawakilishi wa Asasi za Kiraia (AZAKi)Kuhudhuria mafunzo ya kujenga uwezo kwa kamati za PETS na kuwa sehemu ya wajumbe wa kamati hizo
Waheshimiwa MadiwaniKuhudhuria mafunzo ya kujenga uwezo kwa kamati za PETS na kuwa sehemu ya wajumbe wa kamati hizo
Wakulima na wafugajiKuhudhuria mafunzo ya kujenga uwezo kwa kamati za PETS na kuwa sehemu ya wajumbe wa kamati hizo

Future Plans

Activities Planned1st Month2nd Month3rd Month
Kufanya zoezi la kufuatilia matumizi ya fedha na rasilimali za umma PETS katika sekta za kilimo mifugo kupitia miradi ya DADPs / PADEP kwa kila halmashauri 6 za wilaya / manispaa za mkoa wa Mtwara.xxxxxxx
Kufanya uchambuzi wa taarifa na takwimu zilizokusanywa katika zoezi la PETS na kuandaa taarifa za marejesho kwa kila wilaya / manispaa za mkoa wa Mtwara ifikapo Desemba 2011xxxxxxx
Kufanya ufuatiliaji na tathmini za maendeleo ya utekelezaji wa mradi na mwelekeo wa ufikiwaji malengo katika Halmashauri 6 za Wilaya/Manispaa 6 za Mkoa wa Mtwara. xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Beneficiaries Reached

    Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
WidowsFemale75750
Male2252250
Total3003000
People living with HIV/AIDSFemale34340
Male24240
Total58580
ElderlyFemale51510
Male1531530
Total2042040
OrphansFemale--
Male--
Total--
ChildrenFemale--
Male--
Total--
DisabledFemale17170
Male51510
Total68680
YouthFemale30300
Male90900
Total1201200
OtherFemale149314930
Male298529850
Total447844780
Wakulima, wafugaji na wafanyabiashara.

Events Attended

Type of EventWhenLessonsActions Taken
Mkutano wa upasahanaji wa Habari za Ruzuku toka FCS 2008Namna ya kuomba ruzuku kutoka FCS kwa kuzingatia mwongozoKuomba ufadhili toka FCS kwa kuzingatia mwongozo na hatimaye kufanikiwa kufadhiliwa.
Mafunzo ya Kusimamia Ruzuku ya Mradi (MYG)Juni/Julai, 2011Namna ya kusimamia fedha za ruzuku toka FCS na kutekeleza shughuli za mradi kiufanisi.Kusimamia fedha za ruzuku kwa mujibu wa taratibu na kutekeleza mradi kiufanisi sawa na mkataba uliosainiwa kati ya FCS na TCCIA Mtwara.

Attachments

« Previous

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.