Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Tanzania Chamber of Commerce Industry and Agriculture (TCCIA) - Tawi la Mkoa wa Mtwara tumeanza utekelezaji wa Mradi wa Kuimarisha Ushiriki wa Jamii katika kufanya Ufuatiliaji wa Matumizi ya Fedha na Raslimali za Umma (PETS) kupitia Mipango ya Kuendeleza Kilimo Wilayani (DADPs) na Mipango Shirikishi Jamii ya Kilimo na Mifugo (PADEP) ambayo ni sehemu ya mipango, mikakati na miradi ya Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (PKSK) au maarufu ASDP.

Mradi huu unatekelezwa katika Halmashauri 6 za Wilaya/Manispaa za Mkoa wa Mtwara za; Tandahimba, Newala, Nanyumbu, Mtwara Vijijini, Mtwara Manispaa na Masasi kwa muda wa miezi kumi na miwili (mwaka mmoja). Mradi huu unafadhiliwa na taasisi ya The Foundation for Civil Society ya Dar Es Salaam kwa gharama ya fedha za shilingi ya Kitanzania zipatazo Milioni Arobaini na Tano (TZS. 45,000,000/=). Mradi umeanza kwa shughuli za; Kuendesha warsha kwa viongozi/watendaji wa Serikali za Mitaa ambao ni, Maafisa Kilimo (W), Maafisa Mipango (W), Wachumi, Maafisa Maendeleo ya Jamii na Wakurugenzi na/au wawakilishi wao ambapo walielezewa malengo ya mradi na kuongezewa uelewa kuhusu dhana na dhima ya PETS. Jumla ya Watendaji/Viongozi 44 tumeweza kuwafikia kati ya 60 waliotarajiwa.

Vilevile tumeeendesha mafunzo kwa wadau tofauti 62 wa maendeleo kutoka katika halmashauri za wilaya/manispaa za Mkoa wa Mtwara ambazo ndizo maeneo ya utekelezaji wa Mradi husika. Mafunzo hayo yaliweza kujenga uwezo kimaarifa, mbinu na stadi kwa wadau hao katika kufanya PETS kwa kuwezeshwa namna ya kukusanya taarifa, kuzichambua, kuandaa ripoti ya mrejesho na jinsi ya kufanya Mkutano wa Mrejesho na mbinu za kufanya ushawishi na utetezi wa matokeo ya zoezi la PETS. Mradi umeanza kutekelezwa katika kipindi cha robo ya kwanza katik ya robo nne zitakazotekelezwa katika mwaka mzima wa utekelezaji mradi husika.

March 4, 2012
Next »

Comments (2)

Envaya ni nyenzo bora na rahisi sana katika kufanya mawasiliano ya kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu tofauti kuhusu masuala ya nyanja mbalimbali miongoni mwa jamii ya AZAKi hapa Tanzania na pengine duniani kote. Tunashukuru kwa ubunifu huu na tunatoa pongezi za dhati tukiamini kwamba mradi huu utakuwa endelevu kwa manufaa ya jamii ya AZAKi na watanzania kiujumla.
March 4, 2012

Tunashauri ubunifu huu wa Envaya ukawafikia na kutumika na AZAKi nyingi kwa kuteuliwa watendaji au waratibu wa Mitandao ya AZAKi ya kila Mkoa ili wajengewe uwezo zaidi kuhusu namna ya kutumia teknolojia hii muhimu sana katika dunia hii. Baada ya kujengewa uwezo zaidi basi wapatiwe assignment ya kuhakikisha kila AZAKi katika Mkoa husika inayoweza kutumia teknolojia hii basi wahakikishe wanazifikia na kuwezesha uwezo wa kutumia Envaya kwa ajili ya kupashana habari na taarifa mbalimbali, ujuzi na uzoefu tofauti. Tunataka kuona miaka 100 ya Uhuru wa Tanzania tunakuwa na AZAKi zilizoimairika na kuboreka mijini na vijijini zikifanya kazi kwa kutumia nyenzo bora na za kisasa kama vile ENVAYA.

March 4, 2012 (edited March 4, 2012)

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.