Log in
Nuru Halisi

Nuru Halisi

Wilaya ya Ilala Ukonga Mazizini, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations

Hizi ni baadhi ya changamoto tunazokumbana nazo. Ni watu wakubwa na wenye uwezo ndio wanaochafua mazingira kwa kutoa taka ndani ya mageti na kuziweka nje.  Wanaoathirika ni watoto wa maskini wanaocheza kwenye malundo ya taka hizo na wakazi wa kipato cha chini wanaotumia maji ya visima ambavyo havijachimbwa kitaalamu na taka hizi huingia kwenye visima nyakati za mvua. Tunaomba msaada tuwafikie na kuwaeleza namna ambavyo wanaweza kutoa ushirikiano na kuondoa dhana hiyo.

MIRADI YA MAENDELEO

Nuru Halisi Development Group sasa wameanza kupewa mafunza ya kutengeneza Uyoga na tayari wameanza kwa vitendo kwa kushiriki wenyewe kuandaa vitendea kazi. Wanachama watakuwa wakifanya kazi kwa pamoja ili wapate elimu hii ili iweze kuwasaidia mmoja mmoja kujibunia miradi yake nje ya kikundi. Malengo ya kikundi hiki ni kuwawezesha wanachama kuwa na uwezo wa kujitegemea kwa kutumia rasilimali walizonazo bila kutegemea kusaidiwa. Wanachama wamejiwekea akiba wenyewe na sasa wameweza kuanzisha mradi huu. Hii ni sehemu tu ya mikakati ya NURU HALISI

 

August 6, 2010
« Previous Next »

Add a comment

Your name:
Your location:
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.