Injira
Nuru Halisi

Nuru Halisi

Wilaya ya Ilala Ukonga Mazizini, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

large.jpg

Wanachama wa Nuru Halisi wakiwa katika vikao vyake vya kila wiki. Wanachama hawa hufanya zoezi la usafi wa mazingira kabla ya kuanza kikao.

large.jpg

Hii ni moja kati seminar zinazotolewa na Nuru Halisi zikiwashirikisha wadau wa mazingira.

Viongozi na wanachama wa Nuru halisi leo tumefanya usafi katika mifereji ya kandokando mwa barabara ya Mombasa-moshi bar,mitaro hii imekuwa michafu kwa muda mrefu na tumeona ni vyema kuisafisha na ndio tuanze kuzungumza na wafanyabiashara wa kandokando mwa barabara hii pamoja na wamiliki wa machinjio ya Ukonga-mazizini na kujadili namna ambavyo kila mmoja atawajibika kwa sehemu yake

Hizi ni baadhi ya changamoto tunazokumbana nazo. Ni watu wakubwa na wenye uwezo ndio wanaochafua mazingira kwa kutoa taka ndani ya mageti na kuziweka nje.  Wanaoathirika ni watoto wa maskini wanaocheza kwenye malundo ya taka hizo na wakazi wa kipato cha chini wanaotumia maji ya visima ambavyo havijachimbwa kitaalamu na taka hizi huingia kwenye visima nyakati za mvua. Tunaomba msaada tuwafikie na kuwaeleza namna ambavyo wanaweza kutoa ushirikiano na kuondoa dhana hiyo.

MIRADI YA MAENDELEO

Nuru Halisi Development Group sasa wameanza kupewa mafunza ya kutengeneza Uyoga na tayari wameanza kwa vitendo kwa kushiriki wenyewe kuandaa vitendea kazi. Wanachama watakuwa wakifanya kazi kwa pamoja ili wapate elimu hii ili iweze kuwasaidia mmoja mmoja kujibunia miradi yake nje ya kikundi. Malengo ya kikundi hiki ni kuwawezesha wanachama kuwa na uwezo wa kujitegemea kwa kutumia rasilimali walizonazo bila kutegemea kusaidiwa. Wanachama wamejiwekea akiba wenyewe na sasa wameweza kuanzisha mradi huu. Hii ni sehemu tu ya mikakati ya NURU HALISI

WANACHAMA NA VIONGOZI WA NURU HALISI MKOA WA DAR ES SALAAM TAR 28 JULY 2010

NURU HALISI yapata tuzo ya kwanza ya mazingira Mkoa wa Dar es salaam. Hapa ni wanachama na viongozi wa Nuru Halisi pamoja wa wageni waalikwa wakifurahia tuzo hiyo

Wakati NURU HALISI inaendelea na mikakati ya kutoa elimu juu ya Utunzaji wa mazingira, Uongozi na wanachama wa shirika wamesema hawata kaa ofisini na badala yake watakua wakitoka wakati wote na kuifuata jamii ilipo. Hayo yamesemwa na afisa uhusiano wa shirika hilo Philipo Mtoro wakati walipokua wakitoa maelezo ya kazi zao kwa vitendo mbele ya mgeni rasmi wakati wa kupokea tuzo. Vile vile aliwaomba wadau wengine wa mazingira kujitokeza ili kusaidiana na CBO's pindi zinapokua tayari kujitolea kwa jamii.

Shirika la NURU HALISI jana tarehe 28 July ilikabidhiwa rasmi tuzo ya mazingira iliyotolewa tarehe 5 May 2010 na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam. Tuzo hiyo ilikabidhiwa na mkuu wa kitengo cha Mazingira kwa niaba ya Mkurugenzi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala. Hafla ya kupokea tuzo hiyo ilifanyika katika Ukumbi wa Arawa Mazizini Ukonga.