Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

Kikundi cha Mwanambogo United Youth Development kimeanzishwa kwa ajili ya kukamilisha mtazamo wa muda mrefu wa kuikomboa jamii na kuiunganisha pamoja lengo kuu likiwa ni kujikwamua kimaisha. Ikiwa ni pamoja na kuwa na mfumo / utaratibu wa kusaidiana kwa namna mbali mbali kupitia katika kikundi hiki.

 Kikundi hiki kimeanzishwa na vijana wenye kutaka kuipa jamii maisha bora kwa kila mwanajamii. Kikundi hiki kimeanzishwa katika maeneo ya kijiji cha Chogo,Wilaya ya  Handeni ,Mkoa wa Tanga, kikiwa na wanakikundi waanzilishi kumi (10)idadi inatarajiwa kuongezeka.

 Ukijaribu kufanya utafiti wa kina utafahamu kuwa hakuna maendeleo ya kuletwa bila kujiletea wenyewe / mwenyewe. Na ila uwe na maendeleo lazima uwe mstari wa mbele katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayokukabili na kudumisha maendeleo ya jamii. Ndio maana kikundi hiki kimejikita zaidi katika kuikwamua jamii kimaisha mazuri na yenye maendeleo kwa kugusa mazingira yanayowazunguka elimu pamoja na uchumi na hasa kuelimisha jamii juu ya adui wa maendeleo kama vile magonjwa n.k.

 Wengi wetu tukiwa hatuna elimu ya kutosha, tukiwa ni miongini mwa jamii, Kuna kila sababu ya kila jamii kupenda kusoma kujua haki zao kwa njia mbali mbali kulingana na mazingira na uchumi. Harakati hizi za kumhamasisha na kumkomboa mwanajamii kujitegemea ni hatua madhubuti katika kuikomboa jamii kuondokana na hali ya kujidharau, kukosa matumaini na kujikwamua kutoka katika lindi la kina kirefu cha umaskini, maradhi na ujinga.

Kikundi kitatumia vipaji vya mwanakikundi katika kuendeleza jamii kwa kuelimisha kwa njia mbalimbali ili jamii iweze kujishughulisha, kumiliki mali na kujiajiri wenyewe kulingana na wakati (mabadiliko ya kila siku).

 Jitihada zetu ni kuikomboa jamii na kuendeleza utamaduni wetu, na hii ni kauli mbiu yetu Mwanambogo United Youth Development – TUAMKE LEO ILI TUISHI KESHO ili kutimiza malengo ya jamii kwa ufanisi zaidi.