Injira
MTANDAO WA HABARI ZA KIJAMII TANZANIA(MHAKITA)

MTANDAO WA HABARI ZA KIJAMII TANZANIA(MHAKITA)

Morogoro Manispaa, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

 

 

Madhumuni ya MHAKITA

 

  1. Mhakita unaanzishwa kwa malengo ya: 

(a)   Kuandika habari za jamii hususani jamii ya watu waishio vijijini

(b)  Kuelimisha jamii juu ya masuala mbalimbali kupitia taaluma ya habari kwa mfano,Utunzaji wa mazingira katika dhana endelevu

 

(c)   Kuelimisha jamii juu ya kilimo cha kisasa kwa kupitia vyombo vya habari

 

(d)  Kuelimisha wakulima na wafugaji dhidi ya kanuni bora za kuendesha shughuli za kilimo na ufugaji ili kuweza kupunguza umasikini

 

(e)   Kuwahamasisha wananchi juu ya afya ili kukabiliana na magonjwa mbalimbali

 

(f)     Kujenga misingi imara na kuboresha maisha ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi.

 

(g)   Kuelimisha wazee wasiojiweza, wajane kwa kutoa elimu ya ujasiliamali ili waweze kukabiliana na makali ya maisha katika maeneo ya vijijini

 

(h)  Kujengea uwezo na Kuelimisha vyombo mbalimbali vya maamuzi katika sekta ya elimu, afya, maliasili na mazingira, kilimo, maendeleo ya jamii,jinsia na watoto, katiba na sheria juu ya masuala mbalimbali ili kuleta ustawi mzuri kwa mtanzania.

 

(i)     Kushirikiana na vikundi, mashirika, Asasi na kampuni mbalimbali za kitaifa na kimataifa katika kutimiza malengo ya Mtandao

 

(j)     Kufanya tafiti mbalimbali juu ya masuala yahusuyo jamii

 

(k)  Kubuni na kuendesha miradi mbalimbali katika kutimiza malengo ya jamii

 

(l)     Kutangaza na kuchapisha majarida, vipeperushi, vitabu na makala mbalimbali kuhusu haki za binadamu, utunzaji wa mazingira, habari za kilimo, ardhi,wafungwa, maliasili,uongozi na utawala bora, elimu ya uraia, jinsia na makundi maalum

 

(m)                        Kutafuta vyanzo vya fedha ikiwemo kufanya harambee kwa ajili ya kutimiza malengo ya Mtandao

 

(n)  Kutoa misaada ya hali na mali kwa yatima, wajane, walemavu wa aina zote, wazee na watu walio katika mazingira magumu

 

(o)   Kutoa huduma ya ushauri wa kitaalam katika masuala yahusuyo tasnia ya habari

 

(p)  Kufanya mambo mengine ambayo yataendeleza malengo ya Mtandao

Amakuru agezweho
MTANDAO WA HABARI ZA KIJAMII TANZANIA(MHAKITA) yasanze Envaya.
14 Werurwe, 2012
Ibyiciro
Aho uherereye
Morogoro Manispaa, Morogoro, Tanzaniya
Reba ibigo mwegeranye