Envaya
Maeneo ya ukurasa huu yametafsiriwa toka (unknown language) kwa Kiswahili. Ona asili · Hariri tafsiri

KIKUYU YAUNDA KAMATI YA KURATIBU SHUGHULI ZA CLUB ZA MARAFIKI

Marafiki wa Elimu katika shule ya Sekondatri Kikuyu wameamua kuunda kamati ya shule kwa ajili ya kuratibu shughuli za Marafiki ili kuongeza ufanisi na uendelevu wa harakati za Marafiki katika shule hiyo.

Uamuzi wa wanaharakati hao kuwa na Kamati hii ni kuhakikisha kuwa Marafiki wa shule hiyo wanafanya kazi yao kwa umakini zaidi na kuongeza tija katika mijadala na uhuru wa kutoa maoni na kuchangia mada mbalimbali za Club za Marafiki katika shule hiyo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Shule ya Kikuyu ina jumla ya Club 9 za Marafiki ambazo zinahusisha mikondo 9 ya kidato cha kwanza hadi cha tatu. “Kuundwa kwa Kamati hii kutasaidia kuimarisha uhuru wa mijadala na kuzifanya Club zidumu kwani zitasimamiwa na wanafunzi wenyewe”. Club za Marafiki wa Elimu Kikuyu zinajiendeshwa kwa kusimamiwa na Kamati ya Marafiki wa Elimu Dodoma kwa kushirikiana na Mwalimu Mlezi wa Club hizo.

Timu ya Marafiki wa Elimu katika shule ya Sekondari Kikuyu Mkoani Dodoma imeonesha mabadiliko makubwa katika kutetea walimu kwa kutoa wito kwa wadau mbalimbali kuwatetea walimu ili kupata stahiki zao na kuboresha ari ya walimu kufanya kazi zao pasipo kinyongo.

Wanaharakati hao wameeleza kuwa kuendelea kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika shule za sekondari hasa za kata ni matokeo ya kupuuzwa kwa ushauri wa walimu au walimu kusahaulika. Vijana hao wamewataka wadau hasa taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali kusaidia kupaza sauti juu ya kilio cha walimu ili kuwaongezea ari katika kutekeleza majukumu yao.

 

 

 

15 Agosti, 2011
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.