Envaya
Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

MCT YAAHIDIWA MSAADA KUHAMIA DODOMA              Na. MED Media Unit

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi amelishauri Baraza la Habari Tanzania (MCT) kuhamia Dodoma na kuahidi kusaidia juhudi za baraza hilo ili lihamishie makao yake Mjini Dodoma.

Dk. Nchimbi alitoa ahadi hiyo wakati wa ufunguzi wa maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyo adhimishwa kitaifa Mkoani Dodoma. Mkuu huyo wa Mkoa wa Dodoma alisema kuwa Dodoma si makao makuu ya Chama na Serikali tu bali pia ni Makao Makuu ya Vyuo Vikuu kutokana na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuwa ni chuo kikubwa kuliko vyote katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa maadhimisho hayo Dk. Nchimbi alisema kuwa redio ni chombo muhimu na chenye ufanisi wa haraka katika kufikisha habari kwa umma. Alisema redio haihitaji msomi, tajiri wala maskini na haina gharama kubwa wala kutumia muda katika kumfikishia habari mwananchi. "Redio ni chombo pekee cha habari kinachowafikia wananchi wengi kwa haraka hata wale wasiojua kusoma wala kuandika" 

Aliongeza kuwa kutokana na umuimu wa redio ni vyema maadili yazingatiwe katika redio ili kuielimisha jamii zaidi badala ya redio kutumika kama sehemu ya burudani na kurushana roho. 

Maadhimisho ya siku ya Redio Duniani yamefanyika kwa mara ya tatu tangu yaanzishwe rasmi na UNESCO mwaka 2012; kauli mbiu ya mwaka huu ni TUSHEREHEKEE USHIRIKI WA WANAWAKE KATIKA REDIO NA WOTE WANAO WAWEZESHA.

 

14 Gashyantare, 2014
« Inyuma

Tanga igitekerezo

Izina ryawe:
Aho uherereye
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.