Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations
- MED itaendesha vipindi vya Radio kuanzia Machi 2011 kupitia Radio Kifimbo FM.
- Midahalo ya wazi kujadili masuala ya Maendeleo.
- Mikutano ya Club za Marafiki itafanyika katika viyuo vya Mazengo, Kikuyu, Hazina na Image kwa mwezi Machi, 2011
- Mafunzo ya Uandishi wa Habari za jamii kwa Marafiki wa Elimu yatafanyika Kikuyu Sekondari, tarehe 10 Septemba, 2011
HERI YA MWAKA MPYA 2012
Pamoja na salam za mwaka mpya; Asasi ya Marafiki wa Elimu Dodoma inawatakia kila la kheri katika kushiriki kikamilifu katika masuala mbalimbali ya maendeleo ya nchi yetu.
Mwaka 2012 MED inatarajia kujikita zaidi katika masuala yafuatayo:-
- Kuongeza kasi ya uhamasishaji wa jamii, wanafunzi na wazazi katika kuboresha miundombinu ya Elimu ili kuyafanya mazingira ya kujisomea na kujifunzia katika shule zetu kuwa rafiki kwa walimu na wanafunzi.
- Kuwezesha ufanyikaji wa Mijadala ya wazi, Midahalo, Mikutano ya wanafunzi na jamii katika masuala ya Maendeleo.
- Kuimarisha KLABU za Marafiki katika shule mbalimbali za Msingi na Sekondari na kuanzisha KLABU mpya ndani ya shule na nje ya shule.
- Kuendeleza juhudi za wanaharakati wa Elimu na maendeleo katika kuibua mijadala mbalimbali na kuzifanyia kazi changamoto zilizopo.
- Kuimarisha mijadala kuhusu haki za wanafunzi na kutambua wajibu wao kwa walimu na jamii.
- Kuendesha vipindi mbalimbali vya Radio kwa ajili ya kuhamasisha, kuelimisha na kujadili masuala muhimu ya jamii hususan Elimu, Afya na Maendeleo.
- Kuboresha data base ya Marafiki wa Elimu Dodoma kwa kuhuisha kumbukumbu za wanaharakati na kuongeza wanaharakati wapya.
- MED kwa kushirikiana na wadau wake kutafuta namna ya kukabiliana na changamoto ya umaskini inayozidi kuwaandama wananchi wa Tanzania hususan Dodoma ili kuongeza kipato chao.
- Kuimarisha kitengo cha Upashanaji habari kwa kuweka audio na video katika mtandao ili wale wasioweza kusoma wasikilize na kuona baadhi ya taarifa za matukio mbalimbali ya wanaharakati.