Fungua
DAKAWA ECONOMIC DEVELOPMENT ORGANIZATION

DAKAWA ECONOMIC DEVELOPMENT ORGANIZATION

WAMI DAKAWA, Tanzania

DAKEDEO NA USHIRIKIANO NA ASASI ZA KIRAIA .

DAKEDEO  Imeendesha mafunzo ya kuwajengea uwezo wanachama wa asasi za kiraia zilizopo Wilaya ya Mvomero kwa lengo la kuziongezea ufahamu juu ya Mbinu mbalimbali za Kiungozi katika kuleta Mafanikio katika kukuwa kwa asasi hizo.

Asasi zilizonufaika na mafunzo hayo ni pamoja na asasi ya  WECA (WOMEN ENVIRONMENT CONCERVATION ASSOCIATION) asasi yenye makao yake makuu Wikaya ya Mvomero Mtibwa,

Asasi nyingine iliyonufaika na mafunzo hayo ni pamoja na USHIRIKIANO GROUP Iliopo katika Wilaya ya Mvomero Kata ya Kidudwe.

katika makubalianoya baadae DAKEDEO inatarajia kutekeleza miradi yaubia na asasi za kijamii za wilaya ya Mvomero (CBO).

Zaidi ya hapo DAKEDEO ina mpango pia wa kutoa mafunzo ya matumizi ya Kompyuta kwa Wanachama wa asasi mbalimbali katuka wilwya ya Mvomero ,mafunzo yanayotarajiwa kufanyika katika mwezi wa Julai mwaka 2013.

5 Mei, 2013
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Maoni (1)

amir zumbe (Mvomero) alisema:
hongereni kwa kuona umuhimu wa asasi ndogo ambazo zina ongoza katika mustakabali wa uchumi wa nchi
21 Juni, 2014

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.