Envaya

Africa Upendo Group imeanzisha program inayojulikana kama SISI KWA SISI.Program hii ni kwa ajili ya wale wote ambao wangependa kujifunza kutumia Computer na kujua kuzungumza kiingereza rika lolote lile.Program hii ni bure haina gharama yoyote ni mtu kuchukua form pale ofisini kwetu na kwa kwa wale wote ambao wanaishi katika Jimbo la Ubungo tumependa kuanzia pale ofisi yetu ilipo kwanza ndipo tutakaposambaa pote Tanzania.Vijana wetu waalimu ni wengi na bado tunahitaji wengi wa kujitolea.Tumesambaza form kwa serikali ya mitaa kadhaa lakini bado tunaweza kupeleka mahali kama watahitaji.Tunamkaribisha mtu yoyote awe ni kijana au mzee waalimu wetu wanauwezo mkubwa wa kufundisha.Wengi ni vijana waliomaliza digree zao wapo katika ajira au bado wanasubiri kupata ajira.Tumeona nchi za jirani watu wakiingia humu kwetu kwa kasi kubwa kwa sababu ya lugha na ufahamu mzuri wa jinsi ya kutumia mitandao na ama computer wakati watu wengi hapa nchini hawajui namna ya kutumia ndio maana tumeliona hili na kuamua kuanzisha program hii.Tuna imani kubwa kuwa watu wenye mapenzi mema watatuunga mkono hata kutusaidia kubeba jukumu hili kubwa.Tunahitaji computer zaidi na waalimu wa kujitolea.Shime tushirikiane kutokomeza ujinga.Pia tunategemea kuungwa mkono zaidi na wadau wetu yaani Dar es Salaam Teknohama Business Incubator(DTBI) pamoja na COSTECH chini ya Eng.George Mulamula.Pia kama wapo wadau wengine tushirikiane tunahitaji pia NGO huko mikoani tushirikiane nao kutekeleza jambo hili.Karibuni

1 Novemba, 2012
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.