Envaya
Maeneo ya ukurasa huu ni kwa Kiingereza. Hariri tafsiri

TAARIFA ZA MRADI WA KUWASAIDIA VIJANA WAUZA CHIPS KUPATA STADI ZA BIASHARA NA KUTENGENEZA MATOROLI YA CHIPS ZINAZOTEMBEA (MOBILE CARTS VENDING CHIPS PROJECT)

Mradi huu ulikuwa unatekelezwa na Shirika la Agape AIDS Control Programme na ulikuwa unafadhiliwa na Shirika la Kazi Duniani (International Labour Organizatio-ILO) Kupitia Foundation For Civil Society (FCS). Lengo kuu la Mradi huu lilikuwa ni kuwawezesha vijana kujipatia kipato kwa njia ya kufanya biashara hususani biashara yenye ubunifu. Bajeti ya Mradi huu ilikuwa Milioni Kumi na Sita (16,000,000 Tshs au 10,000 USD).

Mradi huu umefanikiwa kufanya yafuatayo:

1. Kufundisha vijana wajasiliamali wauza chips juu ya Ujasiliamali na namna ya kuanzisha biashara na kukuza biashara. Mafanikio Vijana 43 wajasiliamali wauza chips kutoka katika Manispaa ya Shinyanga walifundishwa juu ya Ujasiliamli na namna ya kuanzisha biashara Mpya na kukuza biashara walizokuwa nazo.

2. Kufundisha vijana wajasiliamali wa chips namna ya kuunda/kutengeneza matoroli ya chips yanayotembea. Mafanikio Vijana 43 walifundishwa namna ya kutengeneza matoroli hayo na matatu yalitengenezwa ambapo Mkuu wa Wilaya na Kiongozi wa Mbio za Mwenge alipata nafasi ya kukabidhi machine izo kwa vijana hao wajasiliamali

3. Kufundisha vijana wajasiliamali wauza chips juu ya kujenga mahusiano mazuri ya kibiashara na taasisi za kifedha na zile za kiserikali. Mafanikio Vijana 38 walihudhuria mafunzo hayo ya siku 2 katika ukumbi wa katemi hotel na tayari watatu wamepata mkopo kupitia CRDB na wengine 5 wamejiunga kwenye kikundi kupata mkopo kutoka VISION FUND

4. Kusaidia kuunda kikundi cha vijana wajasiliamali wauza chips. Mafanikio Vijana 40 wajasiliamali kutoka katika manispaa ya Shinyanga wameunda kikundi na kupata usajili kutoka manispaa ya Shinyanga ofisi ya Maendeleo ya Jamii

18 Februari, 2015
« Iliyotangulia Ifuatayo »

Maoni (6)

NEW VISION GROUP( muono mpya) (Mwanza, Nyamagana, capr-point.) alisema:
Nimeupenda mradi huo hasa juu ya mobile carts vending chips, hata mwanza kuna haja ya kuanzisha hii ni nzuri sana sana.
22 Februari, 2015
NEW VISION GROUP( muono mpya) (Mwanza, Nyamagana, capr-point.) alisema:
kama mtapata wasaa naomba mtutumie hata picha.
27 Februari, 2015
Salumu salumu (Mtwara) alisema:
Huwa nafurah kuona juhudi za kijana mwenzangu znapofanikiwa
2 Januari, 2016
elizabeth f mungo (Ngokolo shinyanga ) alisema:
That is very nice because it help many youngs in their daily life and i wish to work in that organization so that i may participate in different development activities.
12 Novemba, 2016
seedoplan (karagwe tanzania) alisema:
mmefanja jambo zuli kuwasaidia vijana hasa kwa shughuli inayowezekana na isiyohitaji mtaji mkubwa
18 Januari, 2017
ELISHA MAGAMBO (Kijitonyama, Dar es Salaam) alisema:

Waooh, niwapongeza sana AGAPE na uwongozi mzima kwa kuweza kuthubutu na kufanya kwa ajili ya kusaidia vijana kwa kuwapa ujuzi ambao utawasaidia kuweza kuwapa kitu cha kufanya badala ya kushinda vijiweni na kujiingiza katika makundi maovi safi sana na endeleeni kufanya kazi hii kwa ubora zaidi na Mungu awabariki.

31 Agosti, 2019 (ilihaririwa 31 Agosti, 2019)

Ongeza maoni

Jina lako:
Mahali ulipo:
Email yako:
(sio lazima)
Anwani yako ya email haitachapishwa.