Log in
voice of wise women

voice of wise women

Mtwara, Tanzania

FURAHA IKO WAPI?

voice of wise women
September 27, 2012 at 11:39 PM EAT

FURAHA IKO WAPI?

Najua wengu wenu mtachukulia hii kama hadithi yakutunga ila napenda kuwaambia kua haya nimambo nilio weza kupitia kwa kipindi kifupi cha Mwaka 2011-2012 na mpaka leo tar 21/9/2012 bado yanaendelea kunitokea mengine ambayo nitawashirikisha pia…

Sinto sahau siku ile nilipo sikia baba yangu niliekua naishi nae alipo niita mwana haramu iliniuma na nikakosa lakufanya zaidi ya kulia na kujiuliza kwanini aliniita vile nilizidi kumwombea kwa mungu kwani yeye ndie mzazi wangu nilie nae.

Tarehe 9/9/2011 usiku kuamkia tarehe 10/9/2011, nakumbuka tulikua tukisafiri pamoja na ndugu zangu sita akiwemo mchumba wangu tukielekea Unguja na meli ya Mv. Spice islander kumpeleka bibi arusi tayari kwa arusi iliokua ikitarajiwa kufungwa uko unguja, ila tulipofika Nungwi, meli yetu ilikumbwa na dhoruba kubwa nakushindwa kuendelea na safari na ndipo meli ya MV Spice Islander I ilianza kupata msukosuko katika mkondo wa Nungwi kwenye majira baina ya saa 6.30 hadi 7.00 za usiku kwa kuingiza maji kwa wingi kupitia kwenye matundu yaliyopo nyuma ya meli. Mabaharia wa meli hiyo walijitahidi kuyatoa kwa kutumia pampu na zilipoharibika walitumia ndoo lakini yaliwashinda, hali iliyopelekea meli kupoteza wizani na kulala upande wa kulia. Nahodha alitoa tangazo la kuwataka abiria kuhama kutoka upande wa kulia kwenda kushoto. Hata hivyo muda huo huo jenereta na injini ya meli zikazimika na meli ikatitia kwa nyuma na kuinuka mbele na kuanza kuzama .Hali ilikuwa ni ya taharuki baada ya meli kuanza kuzama, baadhi ya abiria waliweza kupata makoti ya uokozi (life jackets) na kujitosa baharini na wengine walijitosa ama kutupwa na meli baharini bila ya kuwa na makoti hayo. Ndani ya maji kila mtu alijaribu kujiokoa Kwa kutumia vitu mbali mbali, kwa mfano magodoro, madumu ya mafuta ya kupikia na mapolo ya viatu. Abiria wengine waliingia katika maboya ya kuokolea maisha (life rafts) yaliyokuwemo Melini, nami nikafanikiwa kujishikilia kwenye mzigo wa viatu ila nguvu ziliniishia na kuamua kujiachia nizame na kwa baati nzuri kabla sijaanza kuzama aliniwai mvulana mmoja ambae alinishika mkono na kuniweka juu ya boya lililo nistiri mpaka kulipokucha tulipokuja kuokolewa ila ndugu zangu wote walifariki akiwemo na yule mchumba wangu, tokea pale furaha yangu ilitoeka nikaamua kurudi pemba kwa wazazi ambapo lile jina la mwanahara lilizidi adi kwakina shangazi na maneno mengine yalikuwa akitamkiwa baba “unaangaika nini kumsomesha mtoto asiye wa kwako?”

 

na apo mawazo ndio yalinizidi na kuamua kumuuliza mama ukweli ya yale niliokua nikiyasikia, mama alinificha kwakua nilikua bado nasoma.

Nilishukuru mungu pale alipo kuja baba yangu mdogo iliekua anaishi mtwara na kutaka aondoke na mimi nami nilikubali tokaenda nae mtwara ambapo maisha yangu mapya yalianza, ndani ya mwaka huo baba mdogo aliamua kunibadilisha jina na kunipa lake na la mzazi pia nikawa natumia lake na kuniambia kuanzia sikuile mimi nitakua ni mwanae, akaniandikisha chuo kimoja apo mtwara ambapo nilichukulia certificate ya secretarial na mwaka 2012 nilimaziza na kuamua kurudi pemba kuwasalimia wazazi. Nashukuru mungu niliwakuta wazima na ndugu zangu watatu pia walikua wazima yaani kaka zangu walio nitangulia wawili na dada mmoja.

 

Chuo kilipo karibia kufunguliwa baba mdogo alinitaarifu kua natakiwa kurudi ili niendelee na diploma ila mimi niliona ule ndio ulikua muda muafaka wa mimi kufahamu ukweli kuusu baba yangu na ndipo nilipo kata shauri la kumuuliza tena mama, kwa uchungu mama aliniambia amfahamu baba yangu kwani alivamiwa njiani na vijana asio wafahamu siku aliyokua anatoka unguja kununua vitenge na kumbaka kiasi cha kupoteza fahamu na pindi alipo amka alijikuta yupo hosipitalini na siku zilivyozidi kwenda aligundua ni mjamzito hivyo akuweza kujua ni wa nani pia akuweza kumsingizia mumewe kwani alikua safarini Dubai takribani kwa miezi sita, sikuile aliporudi na kumkuta mama na hali ile alikasirika kiasi chakutaka kumuua mama ila wazee walioshuhudia yaliotokea walimsii na kumwambia hayo yote yamefanyika kwa kupangwa na mdogo wake kwani anajua alikua ataki baba amwoe mama. Basi kuanzia pale mama alichukua jukumu la kunilea paka pale nilipo maliza form four na baba mdogo alipo amua kunichukua nikasome certificate bado mama aliendelea kunisomesha.

Sikukata tamaa ya kutaka kumjua baba yangu kwani ule ulikua ni ufunguo wa ufahamu juu ya baba yangu na niliendelea kumsumbua mama yangu na ndipo alipo niambia kijana mmoja alifahamika kua alitokea arusha na wengine walikua ni wa palepale pemba ila walipotea baada ya kutenda yale ila mama aliniadi kuendelea kufanya uchunguzi mpaka ampate baba yangu nami nilimshukuru na kumkumbatia mama uku nikilia. Wiki iliyofuata niliamua kufunga safari ya kutoka Unguja kurudi Mtwara ambapo mama alinisindikiza mpaka Dar-es-salaam na kunipatia fedha kwaajili yakulipia chuo diploma kwa muula wa kwanza na kuniadi ya muula unao fuata atanitumia, kesho yake tarehe 18/07/2012, alinipakiza ndani ya basi la Maning Nice lililokua likielekea Mtwara na kuanza safari yakwenda mtwara nae kwenda kupanda meli kurudi Unguja siku ile ambayo mimi nilikua naenda mtwara. Sintosahau pale ilipofika saa nane mchana nilipigiwa simu nikiwa njiani kua “meli aliokua amepanda mama yako kurudi pemba iliokua ikifahamika kam. Mv.Skagit Imezama eneo la bahari ya chumbe na atujui kama atakua hai” nilijikuta tu nikiteremsha machozi na safari kuiona chungu ila nilivumilia mpaka nilipofika Mtwara nikangojea mpaka kesho yake ambapo nilipokea tena simu iliokua ikinitaarifu kua mama yangu ajaonekana, na siku ya tatu walisema amepatikana ila akiwa amesha fariki, nililia sana kwani matumaini yangu yote ya kumpata baba yangu yalipotea nay ale yakua na mtu anae nipenda pia yalipotea nilijiona ni kama kifaranga kilicho totolewa na kupokwonyo kutoka kwa mama yake na kuwekwa kwenye mvua kubwa kinyeshewe na kupigwa na baridi badala ya kuwekwa kwenye joto la makwapa au kifua cha mama yake, nilikosa lakufanya zaidi yakumshukuru mungu kwa kile kilichotokea. Tulisafiri na baba mdogo adi pemba ambapo tulienda kumpumzisha mama kwenye nyumba yake ya milele na kurejea mtwara, ila sikuweza tena kuanza chuo kwani sikufahamu endapo nitalipia muula ule wa kwanza nani atanilipia iyo miula mingine na ndipo apo nilipo amua kuanza kufanya vibarua vidogovidogo na mpaka kufikia mwezi wa tisa niliweza kuwa na kiasi cha shilingi laki nne nilizokusanya ila kwa baati mbaya chuo nilikua nimechelewa kuanza hivyo niliamua kughairisha mpaka mwaka uliofuata mwezi wa kwanza pale watu watakavyo anza kujiandikisha tena kwa muula wa kwanza.

 

uwezi amini mpenzi msomaji wangu mwezi ule aukuisha likajitokeza tatizo jingine. Sikumoja ilikua juma tatu nilirudi mapema nyumbani kutoka kwa rafiki yangu, kwakua nilikua nimechoka niliamua kuingia chumbani kwangu na kujipumzisha na ndipo nilipomsikia baba mdogo akiongea sebuleni na mke wake kua anasikitika na ajui atanielezaje kua amepewa uamisho wa kwenda singida kikazi na anatakiwa aende na familia yote ndani ya siku 14 awe amesha fika Singida, kiukweli niliumia na kusubiria niitwe, aiukupia dakika nyingi aliniita na kuniambia kua ameamishiwa singida ila mimi ataniacha mtwara kwa rafiki yake, nilijaribu kuuliza sababu za kuniacha mimi kwa rafiki yake akunijibu zaidi aliniambia nitakufanyia mpango utapata kazi apa mtwara we baki tu kwa rafiki yangu alafu tutakua tunawasiliana, nilishindwa kujizuia kulia niliondoaka na kuingia chumbani nakuzidi kulia. Ndugu msomaji nilisikitika sana kwa yale yaliokua yakinitokea nikijiangalia bado mdogo wa 1991 kama wazazi wangu wangekuwepo aya yote yasingetokea, ata baba basi angetokea saivi mimi niko radhi kumsamee nakurudi kwake, mama nae amenikimbia wakati bado namwitaji, kwanini mimi yote aya.

Sikuzote ukweli utabaki kujitenga na uongo nashukuru japokua iliniumiza zaidi pale nilipo pata ukweli wa kile kilichokua kinaendelea, kua ule ulikua ni mpango wa kunitelekeza mimi Mtwara kwani aliwai kumsikia Baba mdogo akiongea na simu kwa kufokeana ambapo yule aliekua akiongea kwenye simu alikua ni baba yule wa pemba ambae alikua akimgombeza mdogo wake kua achane na mimi kwani sio damu yao na ata akinisaidia nikafanikiwa sintokuja kuwasaidia hivyo anifukuze nipotee kwenye ukoo wao, bamdogo kumjibu kua mwezi wa tisa atapata uamisha ambapo ataniacha mimi mtwara na kukatisha mawasiliano na mimi na huo ndio utakua mwisho wa mimi kuishi nae, na kweli ule wakati ulifika, ukweli nilizidi kuumia na kuamua kumfuata baba mdogo na kumlilia na kumweleza kua yeye ndie tumaini langu alie baki asiniache gizani kwani maisha yangu ndio yatakua yameisha kabisa nibora nimfuate mama yangu kule aliko kuliko kunifanyia hivi ukizingatia mimi bado mdogo kuweza kujitegemea.

Siku zote mungu ammtupi mja wake japo majaribu kwangu ni mengi, wakati nasubiria kuondoka kwa wazazi wangu walezi kuelekea alipo amishiwa kikazi niliendelea kumuomba mungu anipe moyo wa ushujaa mpaka ilipo fika jumamosi Tar 22/9/2012 nilipoamka asubui sana nakuanza kufanya usafi kwa mara ya mwiso kwenye nyumba niliokua nikiependa sana nikiwa na majonzi nahuku nikifahamu kua ile ndio ilikua siku yangu ya kwenda kule ambapo nilitakiwa kuamishiwa, sikuamini pale mama aliponifuata nakuniambia “nenda ukanywe chai ila uchukue chakula kilichopo kwenye Hotport dogo na Lile kubwa ni langu, mwanangu na mume wangu”, niliumia nakujiuliza maswali mengu kichwani mwangu “mbona chai asubui sana?, au kwakua naondoka?, na mbona leo nimetengewa chombo?, au ndio nimeanza kubaguliwa?”, kiukweli nilikosa majibu nikaamua kupigia simu rafiki yangu mda hulehule kumwomba ushauri, nashukuru mungu alipatikana kwenye simu na nitamshukuru sana kwa ushauri wake “Hallow…., ndio nimekusikia……, sasa chakufanya kwakua unaondoka leo basi we endelea nakazi zako usiende kunywa chai ngojea mpaka baadae, ukiona njaa inazidi nenda ata mtaani ukanywe chai ya kununua ila leo usinywe wala kula apo nyumbani….”. Niliamua kuufanyia kazi ushauri wake aikupita lisaa nilimsikia mama ndani akigombana na kaka “kwanini umekula icho chakuala, akikua chako aya fanya araka nenda kwenye friji uchukue maziwa…. Fanya araka mwanangu utakufa” kuanzia pale niliweza kufahamu nini kilikua kikiendelea nilimpigia tena simu Yule rafiki yangu nakumshukuru kwa ushauri wangu na nilimwona kwangu nikama mkombozi wa maisha yangu kama Yule alie niokoa kuzama kwenye ile ajali ya Mv spice Islander iliotokea kule Nungwi.

Ndugu zangu mnao soma ujumbe huu, naomba mniombee naamini kila jaribu linamlango wake wakutokea na kila chenye mwanzo kinamwisho na mungu anawaaibisha adui zangu mbele za macho yangu. Mungu awabariki kwakutumia muda wenu kusoma ujumbe huu ila mpaka sasa sijajua “je furaha iko wapi?” and if you love some one, do your best to make HER or HIM  happy today while SHE or HE is exist, because you never knows if you are going to see them tomorrow, I LOVE YOU MAMA AND I MISS YOU. Kama baba yangu utasikia ujumbe huu au yeyote anae mfahamu kwa mujibu wa habari hii kama naomba tuwasiliane kwakupitia njia hii ya facebook natamani sana japo niwe ata na mzazi mmoja ambae ni baba mzazi kwa yote aliyo yafanya kwa mama mimi nilisha samehe.

 

 

Pole dada,Mungu si Athumani zidi kumuomba atakufungulia milango zaidi. lakini jipe moyo kwani hakuna anayezaliwa kwa bahati mbaya, Mungu ana mpango maalumu na wewe. Kuwa mwaminifu na ishi kwa kumtegemea hatimaye utafahamu nini makususdi yake kwa maisha hayo unayoyapitia. (MBEYA)
April 16, 2014 at 2:12 PM EAT

@voice of wise women: 

denis (arusha)
April 25, 2014 at 11:12 PM EAT

@voice of wise women: 

denis (arusha)
April 25, 2014 at 11:16 PM EAT
hakuna lenye mwanzo lisilokua na mwisho ipo cku tu Mungu atakupa pa kutokea

Add New Message

Invite people to participate