Log in
Women Against Poverty and HIV/AIDS

Women Against Poverty and HIV/AIDS

Mbezi Mshikamano, Tanzania

Parts of this page are in Swahili. Edit translations
wapa kesho tutakua kwenye mkutano unaohusu wanawake wajane wanoishi na VVU kujadili changamoto zinazowakabili kama wajane wenye VVU
wapa tunaungana na mitandao yoteya watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI pamoja na baraza la watu wanaoishi na virusi vya ukimwi Tanzania kwa kuadhimisha siku ya kuwasha mishumaa kuwakumbuka wanaharakati walioishi na virusi vya ukimwi na kufariki kwa ukimwi, tarehe 30/05/2010 katika uwanja wa mashujaa mnazi mmoja dar es salaam. wao walijitoa muhanga katika kuielimisha jamii ya watanzania ili kupunguza kasi ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kazi walioiacha nasi tunaiendeleza Mungu aziweke roho za marehmahala pema peponi.
Tathimini ya utawala bora imefanyika jana katika ofisi zetu za wapa hapa mbezi walioshiriki ni pamoja na afisa maendeleo ya jamii kata ya mbezi mjumbe kutoka serikali za mitaa mtaa wa mshikamano pamoja na wajumbe wa wapa.
Wapa baada ya kufanya mafunzo ya utawala bora kwa viongozi wa kata ya mbezi na wananchi wa kata hii ya mbezi , keshotarehe 25/05/2010, tutafanya tathimin ya mafunzo ya utawala bora katika ofisi za wapa zilizoko kata ya mbezi wanaohusika na tathimin hii wameshapewa taarifa, karibuni sana..
habari wana envaya ,wapa imeona kwamba katika mapambano dhidi ya ukimwi ,elimu imetolewa ila bado kuna idadi ndogo ya wanaume wanaojitokeza kupata huduma hiii,na hata wale wachache wanaojitokeza na kuonekana wana vvu,imekuwa vigumu kufuata matibabu kikamilifu ikiwemo matumizi sahihi ya arvs,hivyo wapa imeona kuna haja ya kufanya uhamasishaji kwa wanaume kujitokeza kupima vvu kwa hiari na kutoa mafunzo ya matumizi sahihi ya dawa za arvs, pia kuwahamasisha wale ambao wameshapima na kukutwa wana vvu ,na watumie vituo ambavyo viko karibu na maeneo wayoishi,hii itasaidia kupunguza unyanyapaa katika jamii inayotuzunguka,kwa kuliona tatizo hili wapa tunaomba ufadhili ili tuweze kufanya uhamasishaji kwa jamii.
Leo wapa tupo katika ofisi zetu na tunajiandaa kwa ajiri ya maonyesho ya sabasaba , bidhaa zetu ni mlonge na batiki tutawapa taarifa tutakua banda gani karibuni sana
wapa tunatarajia kufungua tawi mkoa wa pwani wilaya ya mkuranga mwezi juni 2010
wapa inatoa wazo wana envaya wa Tanzania tufahamiane kupitia mtandao huu
wapa tunapokea vijana wengi wanaohitaji huduma ya upimaji wa vvu kwa hiari lakini tunashindwa kutoa huduma hii kwani kituo chetu hakina wataalam waliosomea upimaji tunaomba tusaidiwe ili huduma hii ipatikane,na katika mtaa huu wa mshikamano hakuna kituo kinachotoa huduma hii ya upimaji, maoni waliotoa vijana waliofika katika ofisi za wapa,walisema wanahitaji wapate huduma hii kwa karibu zaidi