Envaya

Baadhi ya wanamichezo vijana kutoka chuo cha Victory kilichopo chini ya taasisi ya VIYOSO wakiamasisha michezo kwa jamii

SHIRIKA LA VIYOSO LATOA SEMINA KWA VIJANA MKOANI MOROGORO


Shirika la VIYOSO kwa kushirikiana na shirika la YES IDO yameendesha semina ya ujasiliamali kwa vijana zaidi ya 63 kutoka kata 29 za manispaa ya Morogoro.

Semina hiyo ilikuwa na lengo la kuwajengea uwezo vijana juu ya kujitambua na jinsi ya kuwa mjasiliamali hili kuinua kipata na kuchangia maendeleo ya Taifa.

 

 

Mkurugenzi wa Asasi ya vijana VIYOSO mkoani Morogoro Bw. Freddy Ng'atigwa akifungua semina ya ujasiliamali kwa vijana wa manispaa ya morogoro semina iliyoandaliwa kwa ushirikiana wa asasi ya viyoso pamoja na YES IDO kutoka marekani.

mwezeshaji Bi Ashura kutoka ofisa za Manispaa Morogoro Kitengo cha Biashara akitoa mada juu ya fulsa za wajasiliamali vijana kupata leseni katika kuanzisha shughuli zao

Mwezeshaji wa semina kutoka ofisi za TRA  kitengo cha mlipa kodi Bw. Ibrahim wa kwanza kushoto waliosimama akitoa mada juu ya umuhimu wa wajasiliamali kulipa kodi bila kushulutishwa hili kuchangia pato la Taifa.

Mtoa Mada juu ya Kijana kujitambua Dr. Bagati Richson akiwasilisha mada juu ya kijana kujitambua

vijana wa manispaa wakiwa katika kikundi kazi wakijadili mambo mbalimbali juu ya ujasiliamali

Baadhi ya vijana wakiwa katika kikundi kazi wakijadili mambo mbalimbali kuhusu mafunzo ya ujasiliamali yaliyotolewa na asasi ya viyoso

Kijana Frola John akiwasilisha maoni ya kikundi kazi kuhusu fulsa za kijana katika ujasiliamali

Kijana Irene Cyprian kutoka manispaa ya morogoro akiwasilicha mchango wa maoni kutoka kwa Vijana kuhusu changamoto za ujasiliamali baada ya kazi za vikundi