Envaya
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

CHUO CHA VICTORY CHATOA VYETI KWA WAHITIMU WA MAFUNZO YA ICT

Victory & Faith Training Centre kimewakabidhi vyeti zaidi ya vijana 16 waliohitimu mafunzo ya compyuta ICT ngazi ya cheti.

Mkurugenzi wa Victory ambaye pia ni Mkurugenzi wa shirika la vijana morogoro-VIYOS0 aliwaasa vijana kutumia ujuzi walioupata wa ujasiliamali na compyuta kujiajili na kutosubili kuajiliwa.

Vijana nao walikishukulu chuo cha VICTORY kwa malezi bora kwa vijana na ufundishaji wenye tija unaokwenda na technologia ya kisasa na kuwataka vijana ndani na nje ya Morogoro kujiunga na Kituo kihi cha vijana hili kujiendeleza kitaaluma.

Mkurugenzi wa Shirika la Vijana - VIYOSO Bw. Freddy Ng'atigwa akiwa na baadhi ya wanachuo wa VICTORY waliohitimu mafunzo ya ICT mara baada ya kupewa vyeti vyao Mai 3,2014

VICTORY YASHIRIKI MEI MOSI

Chuo Cha Victory & Faith Training  Centre kimeshiriki katika maazimisho ya siku ya wafanyakazi duniani Mei mosi katika viwanja vya Jamuhuli Mkoani Morogoro.

Mkurugenzi wa chuo cha Victory akiwa na  baadhi ya wanachuo wakifuatilia kwa makini maazimisho ya siku ya Mei mosi katika uwanja wa Jamuhuri Mkoani Morogoro

Baadhi ya wanachuo wakifuatilia maonyesho yaliyofanyika katika  siku ya wafanyakazi Mei mosi ndani ya uwanja wa Jamuhuli morogoro

CHUO CHA VICTORY & fAITH TRAINING CENTRE CHAAMASICHA UTALII WA NDANI KWA VIJANA

Chou cha Victory Kilichopo Mkoani Morogoro ambacho kipo chini ya shirika la VIYOSO kimeamasisha utalii wa ndani kwa vijana kwa kutembelea maeneo mbalimbali ya utalii yaliyopo ndani ya mji wa morogoro.

Akizungumza na wanachuo Mkurugenzi Bw. Freddy Ng'atigwa Alisema wakati umefika sasa kwa vijana kuwa na utamaduni wa kufanya utalii wa ndani ilikujua historia ya nchi yao hasa katika siku za mapumziko ya masomo yao.

Baadhi ya wanachuo cha VICTORY wakiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wao na mkurugenzi wa chuo hiko Bw. Freddy Ng'atigwa

Katika kufanikisha ziara yao ya utalii wa ndani wanachuo cha Victory hawakusita kuoga maji ya mto Morogoro

Wanachuo wakifurahia jambo kwa pamoja walipotembelea chanzo cha mto Morogoro

Wanachuo wa victory wakiwa na mkurugenzi wao Bw. Freddy Ng'atigwa walipofanya utalii katika milima Uluguru.

CHUO CHA VICTORY TRAINING CENTRE CHAFANYA MAONYESHO WIKI YA ELIMU

Victory & Faith Training Centre ni chuo kinachotoa mafunzo ya Vocation  na Ujasiliamali kwa jamii ya vijana mkoani Morogoro yakiwemo masomo ya Secretarial, Ushonaji, Hotel Managment, Computer na Lugha.

Victory ni cvhuo kilichopo chini ya shirika la vijana la VIYOSO na kinatoa mafuzo hayo ya Vocation kwa jamii ya vijana wanaotoka katika familia duni Mkoani morogoro.

Hivi karibuni Chuo kilishiriki wiki ya elimu iliyoanzimishwa chuoni hapo ambapo pia ndio makao ya shirika la VIYOSO

Volontia kutoka chuo kikuu huria Bw.Hamisi akiongea na wanachuo wa Victory wakati wa ufunguzi wa wiki ya elimu

Vijana Wanachuo cha Victory wakiwa kwenye sherehe za ufunguzi wa wiki ya elimu zilizo fanyika makao makuu ya shirika la VIYOSO-MOROGORO

Wanachuo wa victory wakigonga grasi zao kuashiria ufunguzi wa wiki ya elimu