Fungua
usambara community

usambara community

dar es salaam, Tanzania

Umoja wa Maendeleo Usambara utajengwa katika misingi ya Upendo, uwajibikaji, uwazi, kujitolea na kufanya kazi kwa bidii .

Masuala muhimu katika kuhakikisha lengo linafikiwa ni

(i)      Kuhimiza mshikamano miongoni mwa wenyeji wa Usambara.

(ii)    Kuimarisha ushirikiano miongoni mwa vikundi vya kusaidiana vya watu wa Usambara katika nyanja za kiuchumi, kijamii, kiutamaduni, kisayansi na nyinginezo, na kuunganisha nguvu kwa ajili ya maendeleo ya Usambara.

(iii)   Kufanya jitihada za kutafuta utengamano wa jamii zinazoishi katika Usambara kwa kufanya usuluhishi na kusimamia majadiliano ya pamoja kwa ajili ya kuondoa migogoro.

(iv)  Kuchukua hatua muafaka za kuunga mkono juhudi za jamii, Serikali Mashirika na watu binafsi za kusaidia maendeleo ya Usambara.

(v)    Kuratibu rasilimali zilizopo nje ya wilaya na ndani ya wilaya kwa ajili ya kusaidia kusukuma maendeleo.

(vi)  Kushiriki katika kukuza, kuendeleza na kudumisha utamaduni na historia ya makabila yaliyopo usambara kwa kuandaa matamasha ya utamaduni wa watu wa Usambara ndani na nje ya nchi ya Tanzania.

(vii) Kutafuta vyanzo mbalimbali vya mapato kwa ajili ya kupata rasiliamali za kuchangia maendeleoya usambara.

(viii)                       Kuhamashisha na kusimamia uanzishaji wa vikundi vya kiuchumi mfano SACCOS, VIKOBA [community bank] n.k.

 

Mabadiliko Mapya
usambara community imeumba ukurasa wa Mkuu.
Umoja wa Maendeleo Usambara utajengwa katika misingi ya Upendo, uwajibikaji, uwazi, kujitolea na kufanya kazi kwa bidii .Masuala muhimu katika kuhakikisha lengo linafikiwa ni – (i) Kuhimiza mshikamano miongoni mwa wenyeji wa Usambara. – (ii) Kuimarisha... Soma zaidi
4 Machi, 2013
usambara community imeongeza Habari.
4 Machi, 2013
usambara community imejiunga na Envaya.
4 Machi, 2013
Sekta
Sehemu
dar es salaam, Dar es Salaam, Tanzania
Tazama mashirika ambayo yapo karibu