Log in

/zayadehe/history: English: WIMWFYgi8gIFGvmOBMcqQP8t:content

« Previous   ·   Next »
Base (English) English

ZANZIBAR YOUTH ASSOCIATION WHICH DEAL WITH EDUCATION AND HEALTH

         sisi ni wanachama wa jumuiya ya zanzibar youth association which deal with education and health(zayadehe)Tuulika kikao cha pamoja chini ya usimamizi wa mwenyekiti wa muazilishi bibi RAYA M.HAJI na kushirikiana na katibu muazilishi BW:HASSAN M.MAKUBULI tarehe 19/02/2008 saa tisa alasiri nyumbani kwa BW:FAUZI A.KHATIBU.kujadili na hatimae kufikia mamuzi ya kuazishwa jumuiya kwa jumuiya ya vijana itakayo jihusisha na utoaji wa elimu mbali mbali pamoja na afya kiiujumla.

ZANZIBAR YOUTH ASSOCIATION WHICH DEAL WITH EDUCATION & HEALTH(ZAYADEHE)

        Na kwa kua maambukizo ya virusi vya ukimwi pamoja na waathirika wa majanga mengine mbali mbali yakiwemo madawa ya kulevya,mimba za utotoni,uchafuzi wa mazingira nk. yamekuwa yakiengezeka licha ya kuwa taasisi kadha zinazopambana na majanga haya visiwani hapa kufanya kazi hizi kwa juhudi kubwa na moyo wa kujitolea,hivyo jumuiya hii ina lengo la kuunga mkono juhudi hizi za mapambano dhidi ya majanga tofauti yaliyomo ndani ya visiwa vyetu ili kupunguza idadi ya maambukizi na waathirika pia kutoa elimu ya mapambano,kujikinga,na kuondokana na unyanyapaa kwa waathirika.

ZANZIBAR YOUTH ASSOCIATION WHICH DEAL WITH EDUCATION & HEALTH(ZAYADEHE)

        Kwa kua jambo hili ni jema na la kikatiba,huku likiwa ni muitikio wa wito wa serikali yenye kuwataka wananchi kujikusanya na kuazisha taasisi zao wenyewe zitakazo unga mkono juhudi za kiserikali za kupiga vita na kupambana na ujinga,maradhi pamoja na umasikini.

ZANZIBAR YOUTH ASSOCIATION WHICH DEAL WITH EDUCATION AND HEALTH(ZAYADEHE)

         Siku ya jumapili ya tarehe 11/05/2008 saa kumi na nusu jioni tulikutana tena eneo hilo hilo na hatimae kulipitisha wazo hili na kutafuta njia za kuweza kufanikiwa katika kuinzisha asasi hii na jinsi gani tutaweza kuipata katiba na kuisajili ili kuwa muongozo wa utendaji wa kazi zetu zote za jumuiya,hata hivyo hakukutokea pingamizi yoyote kwa mwanachama badala ya zile zile zilizotolewa marekebisho hapo hapo.

        hivyo wanachama wote walikubaliana na mwwazo hili na kuanzisha jumuiya hii kwa lengo la kutoa elimu mjumuisho katika jamii.

 

 

(Not translated)

In order to edit translations, you need to log in. Log in · Register