Fungua

/chemadev: Kiswahili: WI00026D3A969BB000000984:content

« Iliyotangulia   ·   Ifuatayo »
Asili ((unknown language)) Kiswahili

DIRA/VISION:

Kuwa na jamii iliyoelimika, na yenye Mipango shirikishi na endelevu kielimu, kiuchumi, kiutamaduni kimazingira ili kuondokana na umaskini na kujiletea maendeleo.

 

DHAMIRA/MISSION:

Kujenga mazingira ya kuihamasisha jamii na kuijengea uwezo ili iweze kuinua ubora wa maisha na kuondokana na umaskini.

 

MADHUMUNI

Kuelimisha jamii ili  kupambana na umaskini, utumiaji dawa za kulevya, mila na desturi zinazokiuka haki za binadamu, magonjwa; utetezi wa haki, utunzaji wa mazingira, habari na utamaduni.

 

Kuziunganisha jamii, rika tofauti na jinsia ili kujenga umoja, upendo, uvumilivu na mshikamano miongoni mwao ili waweze kusaidiana kuheshimiana na kuthaminiana.

 

Kusaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hasa yatima na watoto wa mitaani.

 

Kufanya utafiti ili kufahamu mambo mbalimbali yanayoikabili jamii yale yanayoleta madhara katika afya na maendeleo ya jamii

 

Kuhamasisha jamii iweze kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa ili iweze kujiletea maendeleo.

 

SHUGHULI:

 

Shirika litajishughulisha na shughuli za uhamasishaji wa Maendeleo kwa jamii ili iweze kupambana na umaskini na kuleta maendeleo endelevu.

 

Kuandaa na kuendesha mafunzo kwa ajili ya kuijengea uwezo jamii, kwa njia ya Warsha, Semina, Makongamano, Mikutano na Sanaa shirikishi.

 

Kuelimisha jamii kuhusu sera mbalimbali za kitaifa.

 

Kuwaendeleza wanachama kitaaluma kwa kutafuta wataalam wa fani mbalimbali ili waweze kuwafundisha kwa kushirikiana na taasisi zingine.

 

Kuandaa matamasha kwa madhumuni ya kuelimisha na kuburudisha jamii.

 

Kutayarisha Filamu, Michezo ya Kuigiza, vipeperushi na vijarida kwa madhumuni ya kuelimisha na kuburudisha jamii.

 

Kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya

 

Kutoa ushauri nasaha na stadi za maisha.

 

Kusaidia watoto walio katika mazingira magumu, yatima na watoto wa mitaani kwa kuwapatia malazi, chakula, mavazi, elimu.

 

Kusaidia wajane kwa kuwajengea uwezo ili waweze  kutetea haki zao.

 

Kufanya utafiti mbalimbali ili kugundua matatizo na mahitaji yanayoikabili jamii.

(Bila tafsiri)

Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe