Log in

/chavita_dom: English: WI00081588F9689000102257:content

« Previous   ·   Next »
Base (Swahili) English

     MALENGO YA CHAVITA

 

Kama wanajamii, viziwi wanayo haki ya kuchangamana na watu wengine na kushirikishwa  kikamilifu katika shughuli za jamii. Hii ni haki ya msingi ya binadamu. CHAVITA itahakikisha  hili kwa:

 

  • Kuhamasisha matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi popote walipo hapaTanzania, jamii ya watanzania, taasisi na serikali kuhusu haki za Viziwi.
  • Kupigania usawa katika fursa za elimu, huduma za jamii na nyanja zote za maisha ya binadamu.
  • Kupigania kutambulika kisheria kwa Lugha ya Alama yaTanzania.
  • Kujenga mwamko na kukuza matumizi ya Lugha ya Alama kwa matawi ya CHAVITA, jamii ya Viziwi nchini, na kwa jamii ya watanzania kwa ujumla.
  • Kuhakikisha shughuli za maendeleo ya jamii na ki-uchumi kwa matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi nchini zinaboreshwa.
  • Kuhakikisha matawi ya CHAVITA na jamii ya Viziwi nchini wanapata uwakilishi katika ngazi zote za uongozi.
  • Kufanya na kuendeleza utafiti kuhusu masuala yanayowahusu Viziwi
  • Kupambana na Virusi vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI pamoja na majanga mengine yanayowakabili Viziwi.

 

(Not translated)

In order to edit translations, you need to log in. Log in · Register