Log in

/parents/post/4: English: WID5BQfPl8nGvYIlzZFM2gjO:content

« Previous   ·   Next »
Base (Swahili) English

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

washiriki wa warsha ya sera ya ardhi ,sheria za ardhi ,ndoa na mirathi-Kata ya katubuka,Kigoma ujiji.

Serikali lawamani kwa kutowajali wajumbe wa mabaraza ya ardhi ya kata,Wajumbe wanasema wapo kisheria na serikali inawatambua kuwa wanahudumia jamii,cha kushangaza Tangu kuudwa kwa mabaraza hadi wajumbe kutekeleza majukumu hakuna mafunzo wala vifaa vya kutendea kazi,kibaya zaidi hata karatasi na faili kwa wajumbe ni ngumu kwao.

Waliyasema hayo katika warsha iliyoendeshwa na KIGOMA SINGLE PARENTS ASSOCIATION(KSPA)wakati wa warsha ya sera ya ardhi na sheria za ardhi katika kata ya Katubuka iliyofadhiliwa na THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY(FCS),Hata hivyo Mwenyekiti wa KSPA aliwaasa na kusema asasi imejipanga kutekeleza majukumu yake na kwa kuanzia ni kata ya katubuka na amewaomba elimu na mafunzo wanayoyapata wasiyaweke kapuni bali yatumike katika kumtendea haki mwananchi na hasa wanawake wajane ambao ni masikini.

Naye mratibu wa Mradi(Afisa miradi wa kujitolea katika asasi Ndugu RAMADHAN JOEL amesema Lengo kuu la mradi ni Kupungua kwa migogoro ya ardhi iliyokithili katika kata na mitaa ya katubuka ambayo inahatarisha amani ipungua na iishe kabisa kwani viongozi,wajane na wajmbe wa mabaraza wana elimu na wanatumia sera na sheria za ardhi katika kutatua migogoro hiyo.

Aidha aliongeza na kusema katika utafiti wa awali ulioendeshwa na KSPA ulibaini kuwa Jamii na wanawake wajane,hata viongozi na wajumbe wa ardhi wa mabaraza hawana uelewa kabisa juu ya sera ya sheria ya ardhi,hivyo mradi huu utatoa uelewa na kukuza uifahamu miongoni mwa jamii juu ya sera na sheria ya ardhi.

Naye mwezeshaji,Bi Lyidia kishimba aliongeza ka kusema:amejitahidi kutoa mafunzo kwa kina na mijadala juu ya elimu ya sera ya ardhi,sheria za ardhi,sheria ya ndoa na mirathi.ni nhimu kila mshiriki kutumia vitini alivyogawiwa iliaelimishe na wengine.

(Not translated)

In order to edit translations, you need to log in. Log in · Register