Log in

/envaya/post/115497: English: CMzA1lFDMWm9aDyGshXDuZgA:content

« Previous   ·   Next »
Base (English) English
Tumeona tuchambue wazo lenu na kulimega mafungu matano:
Kujenga Uwezo wa wanachama wenu na viongozi wa Kikundi/Shirika/ Chama au
Asasi yenu kwa pamoja au kwa nyakati tofauti kwa:
a) Kubainisha mahitaji ya msingi (vipaumbele)
b) Kuangalia udhaifu wa asasi na Uwezo wa Asasi na kujibobeza katika
jambo moja au kadhaa
c) Kuingia kwa undani katika dira ya Asasi (mtazamo, imani, madhumini
na shughuli)
d) Kuongeza kipato (fund raising) na mbinu zake
e) Kujenga uhusiano, kutandaa, kushirikiana na asasi nyingine za
kitaifa, kikanda na kimataifa
Haya yanachambuliwa kitaalam kwa kuyaainisha katika mikakati, mipango na
sera kwa kuzingatia muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu. Kimsingi haya
yote hujengwa kwa kuzingatia falsafa inayoongoza asasi kutoka ndani na nje
ya asasi. Ili kupata dhana nzima ya falsafa ya asasi pia utafiti kubainisha
mapungufu ya jamii inayowazunguka hufanyika. Kwa mfano unataka kuandika
mradi wa kutokomeza umaskini katika Kijiji J. Lazima kuangalia katika dira
(vision), mtazamo (mission), madhumuni (objectives) ya asasi yenu
kuna kipengere cha kutokomeza umaskini? Ukitaka kupanga mikakati ya asasi
utafanya hivyohivyo. Utajiuliza maswali mfano hali ikoje kwa dunia, ukanda
wa Afrika na Afrika Mashariki, Tanzania, mkoa wako, wilaya hadi kijiji
hicho. Utafiti utakuwezesha kupta data/hadari na takwimu sahihi za kusaidia
kujenga hoja kuhusu mradi wa kutokomeza umaskini katika Kijiji J.
Kuna mengi ya kuangali tukichambua moja baada ya jingine na mabingwa
wamefanya tafiti nyingi na kuandika vitabu na machapisho mengi. Haitoshi
kuzungumzia suala hili kwa uchache wa maelezo haya. Tunalo darasa la
kuandika miradi, kuwezesha vikundi vya vijana na wanawake, tumeunda pia
vikundi vyetu, tunatoa mafunzo ya ujasiriamali, uongozi wa vikundi na asasi
za aina zote, Tutafute tunapatikana katika website yetu:
www.envaya.org/rural-media4-change au piga simu 0755893303 au baruapepe:
benno.apondo@gmail.com
(Not translated)

In order to edit translations, you need to log in. Log in · Register