Log in

/envaya/post/115497: English: CMybvhg6Ueihon5xG5cUglBW:content

« Previous   ·   Next »
Base (English) English
Kama ada, OLAI inaendelea kufanya shughuli zake kuielimisha jamii kwa kuipatia elimu ya sheria ya ardhi Na. 5 ya vijiji ya mwaka 1999. Wito wangu kwa wadau hususan kwa NGOs popote, tufanye kazi zetu kwa uadilifu wa hali ya juu kwa lengo lilelile la kuiona jamii inakuwa na mabadiliko na hatimae kujiletea maendeleo yatakayoboresha maisha yao. Ingawa mashirika mengi yasiyo ya kiserikali hufanya shughuli zake pasipo faida, juhudi za kiutendaji zifanywe kwa uadilifu ili kuijengea imani kubwa jamii, kwa kile kinachoitwa "umaana wa uwapo wa mashirika haya" hapa nchini kwetu Tanzania. OLAI inatoa wito kwa wadau wa sekta ya Ardhi na wale malengo kama hayo, wakiwemo mashirika yenye kuiunga mkono kwa hali na mali ili ifanye kazi kwa ufanisi ambacho ni dhima ya OLAI. Karibuni OLAI, tujumuike pamoja.NGOs juu sana.
(Not translated)

In order to edit translations, you need to log in. Log in · Register