Asili (Kiswahili) | English |
---|---|
Katika tamaduni nyingi za makabila ya Kitanzania, kukaziana macho wakati wa mazungumzo ni jambo geni. Mara nyingi watoto hawaruhusiwi kuwatazama watu wazima usoni wakati wa mazungumzo. Kufanya hivyo ni ukosefu wa adabu. Hali kadhalika katika makabila mengi wanawake pia hawakupaswa kuwaangalia wanaume usoni wakati wa mazungumzo. Kufanya hivyo ilikuwa dalili ya uchakaramu. Nakumbuka nilipofika hapa Marekani kuanza masomo swala hili lilinipa shida sana kwani nilikuwa siwezi kuongea na maprofesa, wanafunzi wenzangu na watu wengine huku nikiwa nimewakazia macho usoni. Nilizidi kuchanganyikiwa zaidi pale wasichana wa Kimarekani walipokuwa wakiongea nami huku wamenikazia macho usoni. "Wasichana gani hawa wasio na aibu?" Nilikuwa nikijiuliza mara kwa mara.
Sikujua kuwa hili lilikuwa ni tatizo mpaka siku moja mshauri wangu aliponiita ofisini kwake na kuniambia kwamba watu walikuwa wakilalamika kwamba nilikuwa siwaangalii machoni wakati wa mazungumzo. Aliniambia kwamba kwa Wamarekani kuongea na mtu bila kumwangalia usoni ni jambo baya sana. Linaonyesha kwamba pengine unachokisema si cha kweli na kwamba wewe siyo mtu wa kuaminika. Japo nilijibidisha sana kufanya mabadiliko na kuanza kuwakazia watu macho usoni wakati wa mazungumzo, ni lazima nikiri hapa kwamba hili halikuwa jambo rahisi. Na kusema kweli mpaka leo sijalizoea jambo hili na daima huwa sijisikii huru kufanya hivyo. Ndiyo maana hii katuni kidogo imenishangaza. Pengine ni matokeo ya utandawazi na minyororo yake ya kitamaduni. Ni tangu lini mke na mume wa Kiswahili wakakaziana macho wakati wa mazungumzo? Pengine wanandoa wasomi wa mijini lakini siyo kule vijijini. Na simlaumu huyo baba kwenye katuni kwa kushindwa kwake kuhakikisha kwamba kunakuwa na "eye contact" kati yake na mkewe. Huu si utamaduni wetu na kwa sisi wazee hili ni jambo ambalo inabidi tujifunze kama kuna ulazima wa kufanya hivyo. Kwa tofauti na mifano mbalimbali ya migongano ya kitamaduni kati ya Waafrika na Wazungu (hasa Wamarekani) jaribu sana kusoma kitabu mashuhuri cha Profesa Mbele kiitwacho Africans and Americans: Embracing Cultural Differences. |
In many tribal cultures of Tanzania, kukaziana eyes when the conversation is not new. Often children are not allowed to look at adults face during the conversation. Doing so is a lack of discipline. Likewise, women in many tribes they also should look at men face conversation. Doing so was a sign of uchakaramu. I remember when I got here in the U.S. to begin studies this issue lilinipa very difficult because I was not able to talk with professors, classmates and other people while I am ahead gaze. Exceeded more confused when American girls as they were speaking to me with eyes nikazia face. "What these girls have no shame?" I was wondering from time to time. I never knew that this was a problem until one day my mentor was poniita his office and told me that people were complaining that I was not looking eyes during conversation. He told me that for Americans to talk to someone without looking to the future is something very wrong. Shows that probably is not true to say that you are not a reliable person. Although I was very hard to make changes and start kuwakazia people face when the eyes of the negotiations, we must admit here that this was not easy. In fact, until today I have this and she that was arrayed always do not feel free to do so. That is why this little cartoons imenishangaza. Perhaps it is the result of globalization and its cultural bonds. Since when is a wife and husband of Kiswahili and kaziana eyes during conversation? Maybe a couple of urban elites, but not in rural areas. And I blame the father on the cartoons for his failure to ensure that there are "eye contact" between him and his wife. This is not our culture and for us older people this is something we have to learn if there is a necessity to do so. In contrast to various models of cultural conflict between Africans and Europeans (especially Americans) tried to read the famous book of Professor front called Africans and Americans: Embracing Cultural Differences . |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe
Historia ya tafsiri
|