Asili (Kiingereza) | English | |
---|---|---|
Utangulizi. Asasi yetu inaitwa Mwanza Education And Talent Integration Initiatives (METI). Ni asasi isiyo ya kiserikali (AZAKI), makao yake makuu yakiwa jijini Mwanza katika jengo la CCM kata ya Buhongwa wilaya ya Nyamagana. Asasi hii ilianzishwa mwaka na wanachama kumi 2008 na kupata usajili rasmi wa kitaifa mwezi Juni 2009 kwa namba 00NGO/0003213. Kwa sasa inafanya kazi katika wilaya za Nyamagana na Ilemela zinazounda halmashauri ya jiji la Mwanza. Lengo la asasi ni kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi ili kuwajengea uwezo wa kudumu na kuendeleza maisha yao badala ya kuendelea kuwa mzigo na kero kwa jamii. Walengwa wakuu wa asasi hii ni watoto wanaoishi mitaani na watoto wanaoishi katika familia maskini sana wakiwemo yatima waliofiwa na mzazi mmoja au wote ambao walikuwa tegemeo la maisha yao. Madhumuni ya METI:
Malengo ya Muda Mrefu ya Asasi:
Ufafanuzi wa nembo ya asasi
Nembo ya asasi ina vitu vifuatavyo:
WANACHAMA WA METI Uanachama katika asasi ya METI ni wa hiari na unategemea mtu kukubaliana na katiba ambayo inaongoza asasi. Kila anayejiunga na asasi hutoa kiingilio kilichokubaliwa pamoja na ada ya kila mwezi. Kwa sasa asasi ina wanachama 15 wote wakiwa ni waajiriwa katika serikali kuu, serikali za mitaa pamoja na mashirika ya umma. Wachache ni wajasiria mali wenye kujiajiri. Kiingilio na ada za wanachama ndiyo chanzo kikuu cha asasi kwa ajili ya matumizi muhimu ya asasi kama vile kulipia pango, samani za ofisi pamoja na vifaa vya ofisi. Bado asasi haijapata ruzuku toka kwa wafadhili na juhudi zinaendelea kuwatafuta wahisani watakaosaidia kufikia malengo yetu. Kwa sasa Foundation for Civil Society Tanzania wameahidi kutoa ruzuku kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya ujengaji uwezo wa asasi. Hii itakuwa ni ruzuku ya kwanza kwa asasi na tunaamini itasaidia kufungua milango ya kupata ruzuku kutoka wahisani mbalimbali. SHUGHULI ZA METI Hivi sasa asasi imekwishafanya utafiti katika kata saba za jiji la Mwanza (wilaya za Nyamagana na Ilemele) kwa ajili ya kuwabaini watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi. Lengo ni kubaini sababu za mazingira magumu wanamoishi na madhila ya maisha yanayowakabili pamoja na kujua mahitaji yao makuu ya msingi. Utafiti huu umefanyika kupitia shule za msingi na mitaa teule katika kata hizo. Tunaendelea na uchambuzi yakinifu ili baadaye tuone raslimali gani zitahitajika katika kuwahudumia watoto hao. Aidha, asasi imeshaandaa dodoso kwa ajili ya kuwabaini watoto wanaoishi katika mitaa jijini Mwanza ili kupata taarifa za msingi katika juhudi za kutaka kufanya kazi na serikali za mitaa kuwahudumia watoto hawa kwa mujibu wa malengo yetu. Aidha, asasi imeshapata eneo ambalo litatumika kujenga kituo cha kutoa huduma tarajiwa kwa watoto waishio katika mazingira magumu. Eneo hili lina eka takriban kumi katika eneo la Kishili katika kata ya Igoma. Pindi tupatapo fedha shughuli za asasi zitahamishiwa katika eneo hili. VIKAO: METI inafanya vikao vyake kila mwezi mara moja ambapo wanachama wote huhudhuria ili kujadili masuala ya msingi ya asasi yetu. Tumepanga ratiba ya vikao na kila mwanachama hupaswa kuhudhuria isipokuwa pale anapokuwa na udhuru
Baadhi ya wanachama baada ya kikao cho cha kawaida Mawasiliano na asasi yapitie kwa Katibu Mtendaji wa METI – kwa sasa ni Mr. Mafuru Maregesi Yango (contact person) kwa njia zifuatazo: Email: metimwanza10@gmail.com au myango55@gmail.com SLP 10288, Mwanza – Tanzania Simu ya mkononi: (+255) 754 845 084 / 713 340 200 / 732 375 144
KARIBU JIJI LA MWANZA (The ROCK city)
|
(Bila tafsiri) |
Ili kuhariri tafsiri, lazima ufungue. Fungua · Jiandikishe