Log in
RUKWA LEGAL AID ORGANIZATION
Parts of this page are in Swahili. Edit translations

NI ZAMU YA RUKWA SASA

NI MSIMU WA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KWA MKOA WA RUKWA

SHERIA YETU

Misingi Mikuu ya Sheria za Ardhi

Sheria ya Ardhi na Sheria ya Ardhi Vijijini zimeorodhesha misingi mikuu ya ardhi kama ilivyobainishwa chini ya Sera ya Ardhi ya Taifa 1995. Baadhi ya misingi hiyo ni:-

  • Ardhi ni mali ya umma na imekabidhiwa kwa Rais kama mdhamini kwa niaba ya raia wote.
  • Raia wote wanawake na wanaume wana haki sawa ya kupata, kumiliki na kutumia ardhi.
  • Miliki za ardhi zilizopo ikiwa ni pamoja na za kimila zinatambuliwa na kulindwa kisheria.
  • Kuhakikisha kwamba ardhi inatumika kwa manufaa yanayozingatia maendeleo endelevu.
  • Kuhakikisha kwamba fidia kamili na ya haki inalipwa kwa mmilikaji bila kuchelewa pale ardhi yake inapochukuliwa na serikali chini ya sheria mpya za ardhi, au chini ya sheria ya uchukuaji ardhi, kwa manufaa ya umma.
  • Kuweka mfumo bora wa utawala wa ardhi ambao unawawezesha wananchi wote kushiriki katika kufanya maamuzi yanayohusiana na masuala ya ardhi wanayokalia au kutumia.