Injira
kijogoo group for community development

kijogoo group for community development

morogoro, Tanzania

Uru rupapuro ruragaragazwa mu rurimi rw'umwimerere Igiswayire. Edit translations

Habari zenu wadau,

Kijogoo Group for Community Development Imebahatika kuwasilisha maombi ya ruzuku ubalozi wa Ufaranza,hivyo na hamasisha wadau wote tutumie fursa hii kutuma maombi ya Ruzuku ili tuweze kuisaidia Nchi katika kupambana na mabadiliko ya Tabia Nchi na kusaidia Jamii  inayoishi katika mazingira magumu ili sote tusonge mbele na kupiga hatua za kimaendeleo.

Asanteni sana

 

Ramadhan   said

Mkurugenzi

Kijogoo Group for Community Development

1 Kamena, 2016
« Inyuma Ahakurikira »

Ibitekerezo (2)

kijogoo group for community development (Msamvu - Morogoro) bavuzeko
Ofisi ya Kijogoo Group for Community Development ina wakaribisha wadau/mdau anayetaka kujitolea, sisi tuko tayari kumpokea lakini ofisi haina uwezo wa kumpa hata nauli ispokuwa ikitokea fursa yoyote atapewa kipaumbele cha mahitaji muhimu ya kibinadamu.
Asante
Tangazo hili limetolewa na
Mkurugenzi
Bwana Ramadhan Omary
1 Ukuboza, 2016
kijogoo group for community development (Msamvu - Morogoro) bavuzeko
Shirika la Kijogoo Group For Community Development linatafuta wadau wa kusaidiana nao katika harakati za kupinga ukatili wa Kijinsia unaoendelea Wilayani Gairo kwenye Kata za Nongwe,Mandege<Chagongwe na Chanjale dhidi ya ukeketaji wa watoto wadogo wanaosoma darasa la kwanaza na pili hasa katika kipindi hiki cha likizo.
Utafiti uliofanywa na shirika letu kwa kushirikiana na Viongozi na Watendaji wa Serikali ngazi ya Vijiji na Kata wakazi waishio kwenye kata hizo bado wamekuwa wakiendeleza mila zilizopitwa na wakati na tohara hasa kwa wanawake na wamebadili tabia sasa wana wakeketa wakiwa wadogo wanaosoma darasa la kwanza na la pili.
Hali imekuwa ikidhalilisha utu wa mtoto na kumkosea haki zake za msingi hivyo tunawaomba wadau mtakaoguswa na ujumbe huu mtusapoti kifedha ili twende tukaweke kambi ya kutokomeza hali hiyo kwa kuendesha elimu kwa njia ya makongamano na sanaa shirikishi jamii.
Ni mategemeo yetu wadau,mashirika ya ndani na nje,wafadhili wa ndani na nje na serikali pia mtatuunga mkono kwa hili lililopo kwenye jamii ya watu wa Wilaya ya Gairo inayoongozwa na kabila la Wakagulu

Maombi haya yametolewa na
Ramadhan Omary
Mkurugenzi
Kijogoo Group For Community Development
Simu namba 0754 948 767 & 0715 947 897
Email - kijogoogcd@yahoo.com au ramadhankgcd@yahoo.com
1 Ukuboza, 2016

Tanga igitekerezo

Izina ryawe:
Aho uherereye
Your email:
(optional)
Your email address will not be published.