Log in
Foundation for Civil Society

Foundation for Civil Society

Dar es Salaam, Tanzania

Respondent: Lindi Non Governmental Organization Network
Time Submitted: December 5, 2011 at 3:08 PM EAT

Introduction

Lindi Non Governmental Organization Network
LINGONET
Kujenga Uwezo na Stadi za AZAKi za Ushawishi na Utetezi na Kuimarisha Ushiriki katika Sera na Maendeleo.
FCS/MG/3/08/95
Dates: 01 Septemba, 2011Quarter(s): 30 Novemba, 2011
Bw. Sharifu Maloya
S.L.P. 92
LINDI
Simu Mezani: +255 23 220 2630
Nukushi: +255 23 220 2630
Simu Kiganjani: +255 787 187 008
+255 712 316 141
+255 762 565 383
Barua Pepe: smaloya22@yahoo.com
smaloya@hotmail.co.uk

Project Description

Policy Engagement
Civil Society Capacity Strengthening
Mradi huu una malengo ya kujenga na kuongeza uwezo wa Asasi za Kiraia (AZAKi) za wilaya 5 za Mkoa wa Lindi za; Liwale, Ruangwa, Nachingwea, Kilwa na Lindi. Mradi unawezesha kujenga uwezo wa viongozi wa AZAKi katika uendeshaji na uendelezaji wa asasi zao kiufanisi kwa kufanya mafunzo kwa viongozi wa AZAKi kimuundo, kiutendaji na kiuendeshaji (Organizational Development). Mradi unawezesha viongozi kutambua dhana na dhima ya AZAKi kwa ajili ya ustawi na maendeleo ya watu tangu wakati kabla ya ukoloni, wakati wa ukoloni, baada ya uhuru na hatimaye ndani ya mfumo wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa. Pia kuangalia Dira, Dhima, Malengo, Maadili na mambo mengine muhimu kwa ajili ya kuwezesha AZAKi kuendeshwa na kuendelezwa kwa ufanisi.

Vile vile mradi unalenga kuinua na kuboresha uelewa wa AZAKi na jamii kuhusu michakato mbalimbali ya kisera na maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Michakato hiyo ni pamoja na uandaaji wa mipango na bajeti za maendeleo, utungaji wa sheria ndogondogo na utoaji wa maamuzi mbalimbali. Imedhamiriwa na kukusudiwa kwamba kwa kufanya hivyo itawezesha kuongeza na kuboreka kwa uelewa na ushiriki wa AZAKi na jamii kiujumla katika michakato husika ya kisera, kisheria na maendeleo kiujumla. Pia kuimarisha na kuboresha ushirikiano na mahusiano baina ya AZAKi kwa upande mmoja na Serikali kwa upande mwingine ili kuhakikisha kwamba wananchi wakiwa walengwa wakuu wa michakato yote wanawezeshwa kupunguza umaskini uliokithiri na kujiletea maendeleo endelevu.

RegionDistrictWardVillagesTotal Beneficiaries
LindiLiwale - - 480
LindiLindi - - 480
LindiNachingwea - - 480
LindiKilwa - - 480
LindiRuangwa - - 480
 Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
Female62141
Male78199
Total140340

Project Outputs and Activities

1. Wawakilishi 30 wa AZAKi toka wilaya ya Lindi wamejengewa uwezo na uelewa wa maarifa, mbinu na stadi za kufanya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamii (SAM) katika miradi na shughuli za maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ifikapo Desemba, 2011.

2. Viongozi/watendaji 20 wa Halmashauri za Wilaya/Manispaa Lindi na wawakilishi 20 wa AZAKi wamejadiliana, kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu kuhusu uandaaji, utekelezaji, usimamizi na tathmini za miradi na shughuli za maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ifikapo Desemba, 2011.

3. Ushirikiano na mahusiano baina ya viongozi/watendaji wa Halmashauri 2 za wilaya/manispaa Lindi na wawakilishi wa AZAKi vimeimarika na kuboreka ifikapo Desemba, 2011.

4. Ushiriki wa walengwa/wadau katika ufuatiliaji wa maendeleo ya utekelezaji mradi umeongezeka na kuboreka katika Halmashauri za wilaya/manispaa Lindii ifikapo Desemba, 2011.
1. Kuendesha mafunzo kwa wawakilishi wa AZAKi 30 juu ya dhana ya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamii (SAM) kwa siku 2 katika kila wilaya 5 za Mkoa wa Lindi ifikapo Desemba 2011.

2. Kufanya vikao vya siku 1 vya wadau 20 wa maendeleo kati ya viongozi/watendaji wa Halmashauri za Wilaya/Manispaa za Mkoa wa Lindi na wawakilishi wa AZAKi vya kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu kuhusu uandaaji mipango na bajeti za maendeleo, utekelezaji, usimamizi na tathmini za utekelezaji ifikapo Desemba, 2011.

3. Kufanya ufuatiliaji na tathmini shirikishi walengwa/wadau za maendeleo ya utekelezaji mradi katika Halmashauri za Wilaya/Manispaa 5 za Mkoa wa Lindi ifikapo Desemba, 2011.

1. Viongozi 30 wa AZAKi toka Halmashauri za wilaya/manispaa Lindi wamejengewa uwezo na kuongezewa maarifa, mbinu na stadi za kufanya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamii (SAM) katika miradi na shughuli za maendeleo vinavyotekelezwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa yaliyofanyika Oktoba, 2011.

2. Kufanyika kwa kikao cha pamoja cha wadau 20 kati ya viongozi/ watendaji wa Halmashauri ya Wilaya Lindi na wawakilishi wa AZAKi kujadiliana na kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu tofauti kuhusu uandaaji, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya mipango na bajeti za maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichofanyika Oktoba, 2011.

4.Kufanyika kwa kikao cha pamoja cha wadau 20 kati ya viongozi/watendaji wa Halmashauri ya Manispaa Lindi ili kujadiliana na kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu tofauti kuhusu uandaaji, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini za mipango na bajeti za maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichofanyika Oktoba, 2011.

5. Kufanyika kwa ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi kwa kushirikisha walengwa/wadau 40 kwa idadi ya 20 toka kila halmashauri za wilaya na manispaa Lindi uliofanyika mnamo Novemba, 2011.
1. Ndiyo, tofauti iliyopo ni kubadilishwa kwa shughuli ya mradi kutoka ya Kuendesha mafunzo kwa wawakilishi wa AZAKi wa wilaya 5 za Mkoa wa Lindi juu ya Programu ya Maboresho ya Serikali za Mitaa (LGRP) na badala yake kuwa Mafunzo kwa wawakilishi wa AZAKi juu ya dhana ya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamii (SAM). Hata hivyo kabla ya kufanyika kwa mabadiliko haya Mratibu wa Mradi aliwasiliana na Afisa Programu anayesimamia mradi huu katika FCS, Bi. Rose Kihulya na kutoa idhini ya kutekelezwa kwa shughuli hiyo pasipo kupoteza walengwa na mantiki ya mradi.
1. Mafunzo juu ya dhana ya SAM kwa AZAKi za wilaya ya Liwale na Ruangwa (TZS. 1,851,000/=)

2. Vikao vya wadau kati ya viongozi/watendaji wa Halmashauri na AZAKi katika wilaya za Liwale na Ruangwa (TZS. 3,080,000/=).

3. Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ua utekelezaji mradi katika wilaya za Liwale na Ruangwa (TZS. 1,470,000/=)

4. Gharama za Utawala na Uendeshaji wa Mradi (TZS. 2,065,000/=).

Project Outcomes and Impact

1. Kuongezeka kwa Uwezo na uelewa wa kimaarifa, mbinu na stadi kwa AZAKi za kufanya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamiii (SAM).

2. Kuimarika na kuboreka kwa Ushiriki wa AZAKi na jamii katika kufuatilia Uwajibikaji Kijamii (SAM) katika miradi na shughuli za maendeleo katika Halmashauri za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi.

3. Kuboreka kwa Uwajibikaji wa viongozi katika utekelezaji na usimamizi wa miradi na shughuli za maendeleo katika Halmashauri za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi.

4. Kuongezeka na kuboreka kwa Uwazi wa viongozi na watendaji wa Halmashauri katika utekelezaji wa miradi na shughuli za maendeleo katika Halmashauri za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi.

5. Kuimarika na kuboreka kwa Ushirikiano na mahusiano baina ya viongozi/watendaji wa Halmshauri za Wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi na AZAKi.

6 Kuongezeka, kuimarika na kuboreka kwa Upashanaji na upatikanaji wa habari na taarifa za utekelezaji, usimamizi na ufanisi wa mipango na bajeti za maendeleo.
1. Kuongezeka kwa uwezo na uelewa wa AZAKi juu ya dhana ya SAM.

2. Kuongezeka na kuboreka kwa Ushiriki wa AZAKi na wananchi katika michakato ya Sera na maendeleo.

3. Kuimarika na kuboreka kwa Uwezo wa wananchi kufuatilia uwajibikaji wa kijamii kwa viongozi na watendaji wa Halmshauri za wilaya/manispaa husika.

4. Kuboreka kwa Ushirikiano na mahusiano baina na miongoni mwa wawakilishi wa AZAKi

5. Kuimarika na kuboreka kwa Mahusiano na ushirikiano baina ya viongozi/watendaji wa Halmashauri za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi na Wawakilishi wa AZAKi katika michakato ya maendeleo.

1. Viongozi/watendaji wa Halmashauri za wilaya/manispaa wametambua kuwa maendeleo ya kweli hayawezi kupatikana pasipo kushirikishwa walengwa na wadau wa maendeleo husika.

2. AZAKi na wawanchi wamefahamu kwamba pasipo ushiriki wao kamilifu katika michakato ya mipango na bajeti za maendeleo itakuwa ni vigumu kufikiwa kwa maendeleo ya kweli na yaliyo endelevu.
Hakuna sababu zozote za tofauti katika mabadiliko yaliyotokana/kuletwa na mradi.

Lessons Learned

Explanation
Kuwepo kwa mahusiano na ushirikiano usioridhisha/ sio mzuri kati ya viongozi/watendaji wa Halmashauri za wilaya/manispaa na wawakilishi wa AZAKi na wananchi kiujumla kuhusu michakato ya sera na maendeleo.

Wananchi hawashirkishwi kikamilifu na ipasavyo katika michakato ya uandaaji wa mipango na bajeti za maendeleo katika ngazi ya vijiji.mitaa, vitongoji, kata na wilaya.
Mipango na miradi ya maendeleo katika Halmashauri za wilaya/Manispaa haitekelezwi kama ipasavyo na sawa na ilivyokusudiwa.
Kukosekana kwa uwazi wa kutosha na uwajibikaji duni kwa viongozi na watendaji wa Halmashauri za wilaya/manispaa za Mkoa wa Lindi.
Wananchi kukosa uelewa juu ya haki na wajibu wao katika michakato ya sera na maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na hivyo kupelekea kuwepo kwa ushiriki duni.
AZAKi nyingi hazina uwezo, maarifa wala mbinu za kufanya ushiwishi na uchechemuzi kuhusu haki na wajibu wa wananchi kushiriki/kushirikishwa katika hatua tofauti za michakato ya kisera na maendeleo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Challenges

ChallengeHow it was overcome
Viongozi na watendaji wa Halmashauri za wilaya/manispaa kuwa na fikra mgando kwamba wao ndio wanaojua kila kitu na kwamba ndio serikali yenyewe.Kuelimishana na kupeana habari na taarifa kuhusu wajibu na majukumu ya viongozi na watendaji wa Halmshauri katika kuandaa, kutekeleza na kusimamia mipango na bajeti za maendeleo.
AZAKi kutotekeleza wajibu wao wa kuhamasisha na kuelimisha jamii ipasavyo kutambua nafasi, wajibu na haki zao katika michakato ya sera na maendeleo.Kuhamasisha AZAKi kutimiza wajibu wao wa kuelimisha na kuhamasisha jamii katika masuala tofauti ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.
AZAKi kukosa/kuwa na maarifa, mbinu na stadi visivyokidhi haja na mahitaji ya kufanya ushawishi na uchechemuzi kuhusu haki na wajibu wa wananchi kushiriki katika michakato ya sera na maendeleo.Kuelimisha na kuhamasisha AZAKi kujengeana uwezo na stadi za kufanya ushawishi na uchechemuzi wa kudai haki na wajibu wao na jamii katika michakato ya sera na maendeleo.
Kupanda kwa gharama za baadhi ya mahitaji na vifaa muhimu katika utekelezaji wa shughuli za mradi kiufanisi; mf. Vyakula, nauli kwa washiriki n.k.Kununua/kulipia vifaa na/au mahitaji ya utekelezaji wa mradi yanayoendana na bajeti iliyopo kwa kuzingatia ubora na hali halisi iliyopo.
Baadhi ya watendaji/viongozi wa AZAKi kutofahamu vyema malengo ya mradi na matokeo/mabadiliko yaliyokusudiwa na kutarajiwa.Kuelimishana na kuelekezana malengo ya mradi, matokeo/mabadiliko yaliyokusudiwa na kutarajiwa.

Linkages

StakeholderHow you worked with them
Halmashauri za Wilaya na Manispaa LindiKukubali kushiriki katika vikao vya majadiliano na kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu tofauti kuhusu michakato ya sera na maendeleo katika Hlamshauri ya wilaya husika.
Mkurugenzi Manispaa Lindi na Mkurugenzi Mtendaji - Halmashauri ya Wilaya LindiKufanya ufunguzi rasmi na kutoa nasaha katika vikao vya majadiliano na kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu tofauti kuhusu uandaaji, utekelezaji, usimamizi na tathmini ya utekelezaji mipango na bajeti za maendeleo za Halmshauri za Wilaya.
Idara za Mipango Halmashauri za Wilaya na Manispaa LindiKuandaa na kuwasilisha mada kuhusu wajibu wa Idata ya Mipango katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo katika wilaya kwa faida na manufaa ya wananchi.
Idara za Maendeleo ya Jamii - Halmashauri za Wilaya na Manispaa LindiKuandaa na kuwasilisha mada kuhusu wajibu wa Idara ya maendeleo ya jamii katika kusukuma mbele gurudumu la maendeleo katika wilaya kwa faida na manufaa ya wananchi.
Waandishi wa Habari na Wawakilishi wa asasi za KiraiaKushiriki mafunzo ya SAM na vikao vya majadiliano na kubadilishana habari na taarifa, ujuzi na uzoefu tofauti kuhusu michakato ya sera na maendeleo katika Halmashauri za wilaya na manispaa husika.

Future Plans

Activities Planned1st Month2nd Month3rd Month
Kuendesha mafunzo ya siku 2 kwa wawakilishi 30 wa AZAKi wa wilaya ya Kilwa juu ya dhana ya Ufuatiliaji Uwajibikaji Kijamii (SAM) ifikapo Desemba, 2011. XX XX
Kufanya ufuatiliaji na tathmini shirikishi ya maendeleo ya utekelezaji mradi katika wilaya ya Kilwa ifikapo Desemba, 2011. XX XX XX

Beneficiaries Reached

    Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
WidowsFemale1330
Male1538
Total2868
People living with HIV/AIDSFemale918
Male1229
Total2147
ElderlyFemale1433
Male1847
Total3280
OrphansFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
ChildrenFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
DisabledFemale1021
Male1229
Total2250
YouthFemale1639
Male2156
Total3795
OtherFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total140340
(No Response)

Events Attended

Type of EventWhenLessonsActions Taken
Mafunzo ya Usimamizi wa Ruzuku (MYG) 2009Maarifa, mbinu na stadi za kusimamia utekelezaji wa mradi na matumizi ya fedha za ruzuku kwa ufanisi.Kutumia maarifa, mbinu na stadi zilizotolewa kusimamia utekelezaji wa mradi na matumizi ya fedha za ruzuku kiufanisi.
Mikutano ya Upashanaji Habari za Ruzuku toka FCS2005 na 2008Jinsi ya kuandaa na kuwasilisha maandiko miradi yenye sifa, vigezo na ubora unaohitajika na kukubalika na FCS na wadau wengine Kuendeleza jitihada za FCS kujenga uwezo wa AZAKi changa juu ya uandishi wa miradi yenye ubora na vigezo stahili.
Matamasha ya AZAKi 2009 na 2010Umuhimu wa kufanya kazi kwa umahiri na ubunifu mkubwa ili kupata ufanisi na kuleta mabadiliko chanya katika jamii.Kuhamasisha AZAKi kuwa wabunifu na kuchapa kazi kwa umahiri na ustadi mkubwa ili kupata mafanikio makubwa.
Maonesho ya AZAKi Bungeni2006,2007,2008,2009Umuhimu wa kufanya kazi karibu na wabunge ili kuwashawishi mabadiliko katika sera na sheria mbalimbaliKuwashawishi baadhi ya wabunge kuwa karibu na AZAKi ili wasaidiwe katika kutambua na kukabiliana na changamoto za maendeleo katika majimbo yao.
Mafunzo ya kubadilishana uzoefu wa kusimamia miradi ya ruzuku ya kati (MG)2011Kubadilishana maarifa na stadi, ujuzi na uzoefu tofauti katika kusimamia Fedha za Ruzuku ya Kati (MG), Mafanikio, Changamoto na mbinu za utatuzi zilizotumika.Kuwezesha asasi nyingine kupata maarifa na stadi, ujuzi na uzoefu katika kusimamia Fedha za Ruzuku ya Kati (MG)

Attachments

« Previous responseNext response »

« Back to report