Log in
Foundation for Civil Society

Foundation for Civil Society

Dar es Salaam, Tanzania

Respondent: SHANGWE COUNSELING CENTRE
Time Submitted: September 7, 2011 at 9:02 PM EAT

Introduction

SHANGWE COUNSELING CENTRE
SHAC
Kuimarisha utawala bora kwa wanawake vijijini
FCS/MG/2/10/099
Dates: Tarehe; June 1,2011-31 Aug,2011 kipindi cha robo mwaka 2Quarter(s): Robo mwaka 2
Samuel Philimon Ngwipa (Meneja Mradi)
P.O.BOX 3101
Mbeya
Samuel Philimon Ngwipa
P.O.BOX 3101
Mbeya
Tel:0764047358Project Description

Governance and Accountability
Mradi huu unakidhi malengo muhimu ya eneo tulilochagua kwa sababu inalenga utoaji elimu juu ya haki za kiraia hasa wanawake ambao ndio walengwa hasa wa mradi,uwajibikaji wa viongozi wa vjiji ,kata na wilaya ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wanawake katika mipango mbalimbali ya maendeleo
RegionDistrictWardVillagesTotal Beneficiaries
MbeyaRungweKisondela,Mpuguso,Kyimo,Lufingo na BujelaSimike,Kalalo,Kagwina,Itete,Lugombo,Ipongola,Igalabwe,Bulyaga juu,Igamba,Bulyaga kati,Mtindo,Bugoba,Lutete,Kisuba,Ndubi,Kibatata,Nampuga,Ilenge,Isyukula,Kibisi,Kyimo,Katabe,Mibula,Ipummbuli,Isaji,Bujela,Isongola,Ipombo,Kyamandege,Segela60
 Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
Female1631
Male449
Total6040

Project Outputs and Activities

Mkutano juu ya utetezi wa haki za wanawake kwa viongozi 60 wa kata na vijiji umefanyika.

Kuendesha mkutano wa utetezi juu ya haki za wanawake kwa viongozi wa serikali za vijiji na kata.

Kuendesha mkutano juu ya utetezi wa haki za wanawake kwa viongozi wa vijiji na kata

Kufanya zoezi la ufuatiliaji

Mafanikio tuliyoyapata katika kipindi hiki ni wanawake kupewa nafasi ya kusikilizwa mawazo na matatizo yao, na hivyo masuala ya wanawake kuendeshwa kiufanisi hadi kufikia suluhisho lenye kujenga.
Hakuna tofauti
Kuendesha mkutano na viongozi wa kata na vijiji- 1,251,000/=

Ufuatiliaji - 3,132,000/=

Project Outcomes and Impact

Wanawake wameweza kupata uwakilishi katika ngazi mbalimbali ya vyama vya maendeleo na uzalishaji kwenye vijiji mfano mwanamke mmoja ameweza kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa wakulima wa chai katika kata ya Lufingo ambapo kwa miaka mingi walikuwa ni wanaume tu. Vilevile kuna wajumbe 3 wanawake kwenye chama hicho chenye wanachama 20.
Viongozi wa vijiji/kata wamekuwa mstari wa mbele katika kushughulikia masuala ya wanawake hasa baada ya kufanya mkutano na kutambua kwa dhati haki za wanawake kuliko hapo mwanzo ambapo nao walishiriki katika kumkandamiza mwanamke kwa kutosikiliza malalamiko yao na hivyo kuwafanya wanwake kukata tamaa na kubaki na shida zao huku wakiteseka.
Badiliko jingine kubwa ni wanawake kuwa na umoja katika kudai haki zao na kutokuwa na woga kwani vikundi mbalimbali vya kiuchumi vimeanzishwa kwa lengo la kumkwamua mwanamke kiuchumi na kusaidiana hasa pale ambapo kuna aina yoyote ya ukandamizaji juu ya wanawake katika maeneo yao.
Hakuna.

Lessons Learned

Explanation
Mambo muhimu tuliyojifunza ni kwamba viongozi wa vijiji hawana miongozo iliyowazi katika kuongoza makundi yao na inaonyesha madaraka waliyopewa ni nusunusu kwani wengi wao wamekiri kwamba wanashindwa hata kutatua migogoro mbalimbali ya vijiji ikiwemo matatizo ya wanawake na hivyo kutumia miongozo ya kimila na desturi ambazo zina mapungufu katika kutatua matatizo na hivyo kuendelea kumkandamiza mwanamke.
Jambo la pili tulilojifunza ni matarajio ya unafuu kwa mwanamke katika Wilaya ya Rungwe, Viongozi wa vijiji na kata ndio wenye dhamana kubwa katika kutatua migogoro ya wanawake, lakini dhamana hiyo haikutumika vema hapo awali, baada ya viongozi hawa kupata mafunzo wamekiri kwamba kutokana na uelewa mdogo katika kutatua shida za wanawake na kutokujua sheria, hali ya wanawake ilikuwa mbaya sana kwani mashtaka yote yaliyopelekwa kwao yaliishia kuendelea kumkandamiza mwanamke.
Wazo jingine tulilolipata ni juu ya kuendelea kuwapatia mafunzo ya utawala bora viongozi wa vijiji na kata kwani wengi wao wamekiri kubeba majukumu wasiyoyajua mfano kiongozi mmoja wa kijiji cha itete alikiri kwamba hajawahi hata kuona katiba ya nchi na wala hajui kama kunakitu kinaitwa utawala bora, kwake ni mara ya kwanza kusikia kwenye mafunzo haya. Viongozi hawa wa vijiji ni wengi na ndio waliokaribu zaidi na wananchi, hivyo wanatakiwa kujengewa uwezo zaidi juu ya masuala ya uongozi , utawala na utawala bora.

Challenges

ChallengeHow it was overcome
Changamoto ambayo bado tunapambana nayo ni kuhusu mifumo ya kiutawala vijijini, bado hawaamini kama mwanamke anaweza kuwaongoza mfano kwenye mkutano uliofanyika idadi ya wanaume viongozi waliohudhulia walikuwa wengi kuliko viongozi wanawake.Hii inaonyesha kuwa viongozi wanawake bado hawajapewa nafasi zaidi za kuongoza.Tulichokifanya katika mkutano huo ni kuendelea kufanya utetezi juu ya umuhimu wa mwanamke katika maendeleo, na wao walikiri kwamba wamewanyima wanawake nafasi nyingi za kiutawala kwenye maeneo yao na hivyo kuuhakikishia mkutano kubadili mifumo inayomkandamiza mwanamke
Changamoto nyingine ni kuhusu posho, kwakweli ukiwaita viongozi wa serikali katika mkutano au semina wanataka kupewa kiwango cha serikali ambayo ni 65,000/= kwa siku kwa kweli jambo hili lilileta hadithi nyingi.Tuliendelea kuwaelimisha tofauti zetu na serikali kwa nia njema na kuwaomba waangalie zaidi umuhimu wa mkutano kwa faida ya maendeleo ya vijiji/kata zao
Kuongezeka kwa wanawake wanaohitaji msaada wa kisheria Tumejaribu kufanya rufaa mbalimbali mfano kwenye ofisi za ustawi, mahakama ya mwanzo na wote waliozingatia na kufatilia rufaa hizo wamepata msaada.

Linkages

StakeholderHow you worked with them
Ofisi ya mkuu wa Wilaya ya RungweKufungua mafunzo na kutoa kibali kwa watendaji wa kata kuhudhulia mkutano tuliokuwa tumeuandaa na kuendesha.
Asasi zisizo za kiserikali mfano AFNET TanzaniaWameweza kutusaidia kuwaelimisha zaidi viongozi wa kata na vijiji juu ya elimu ya kiraia kwani AFNET wanauzoefu mkubwa juu ya utoaji wa elimu ya kiraia kwa ufadhili toka UNDP.

Future Plans

Activities Planned1st Month2nd Month3rd Month
Mpango uliopo ni kufanya mkutano wa pamoja wa tathmini ambao utajumuisha wadau mbalimbali katika wilaya ya Rungwe ili kutahmini mafanikio na mapungufu yaliyojitokeza katika mradi na kwamba tufanyeje.XXX
Kutoa ripoti ya utekelezaji kwa wadau mbalimbali wa shangwex

Beneficiaries Reached

    Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
WidowsFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
People living with HIV/AIDSFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
ElderlyFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
OrphansFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
ChildrenFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
DisabledFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
YouthFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
OtherFemale(No Response)(No Response)
Male(No Response)(No Response)
Total(No Response)(No Response)
Moja kwa moja ke 16, me 44, Wasio wa moja kwa moja ke 51, me 9

Events Attended

Type of EventWhenLessonsActions Taken
----
----
----

Attachments

« Previous responseNext response »

« Back to report