Log in
Foundation for Civil Society

Foundation for Civil Society

Dar es Salaam, Tanzania

Respondent: Union of Liwale District Non Governmental Organizations
Time Submitted: April 2, 2012 at 5:58 AM EAT

Introduction

Union of Liwale District Non Governmental Organizations
ULIDINGO
Ushiriki wa AZAKi katika michakato ya Undaaji wa Mipango na Bajeti ya Miradi ya Maendeleo
FCS/MG/3/11/110
Dates: 01 Januari, 2012 hadi 31 Machi, 2012Quarter(s): Kwanza
Ally Ligai
S.L.P. 141
LIWALE, LINDI.
Simu: +255 715 066 152
+255 782 066 152
Nukushi: +255 732 933 338
Barua Pepe: allyligai@hotmail.com

Project Description

Civil Society Capacity Strengthening
Governance and Accountability
Mradi unakidhi maeneo ya ufadhili yaliyotajwa hapo juu kutokana na ukweli kwamba; umelenga na kukusudia kujenga uwezo wa Asasi za Kiraia katika kuelewa mchakato wa uandaaji mipango na bajeti ya maendeleo katika ngazi tofauti za Mamlaka za Serikali za Mitaa hususan katika; Vitongoji, Mitaa, Vijiji, Kata na Halmashauri ya Wilaya. Pia kuhimiza ushiriki wao katika michakato hiyo sambamba na kuelimisha na kuhamasisha wananchi kushiriki, kufuatilia na kutathmini ufanisi wa utekelezaji mipango na bajeti husika. Vilevile mradi utawezesha kujenga uwezo na uelewa wa Viongozi (Madiwani) na Watendaji wa ngazi za msingi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa (Watendaji wa Vijiji na Kata) kuhusu mchakato wa uandaaji wa mipango na bajeti za maendeleo na kuzingatia umuhimu wa ushiriki na kushirikishwa AZAKi na wananchi katika michakato hiyo ili kutekeleza dhana na dhima ya utawala bora katika ngazi za jamii.
RegionDistrictWardVillagesTotal Beneficiaries
LindiLiwaleKata 20 za Wilaya ya LiwaleVijiji 76 vya Wilaya ya Liwale4430
 Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
Female1481480
Male2952950
Total4434430

Project Outputs and Activities

• Viongozi wa AZAKI watakuwa wamepata mafunzo juu ya uandaaji wa mipango na bajeti ya miradi ya maendeleo ifikapo Disemba 2012.

• Madiwa 27 toka kata 20 Wilayani Liwale watapata mafunzo juu ya wajibu wao na mfumo wa uandaaji wa mipango na bajeti ifikapo Disemba 2012.

• Kuongezeka na kuimarika kwa amasa ya ushiriki kwa jamii katika kupanga, kutekeleza, kufuatila na kutathimini miradi ya maendeleo
• Kuendesha mafunzo ya siku 3 kwa viongozi wa AZAKI 70 kwa wamu 2 juu ya mchakato wa Uandaaji wa mipango na Bajeti ya Miradi ya Maendeleo.

• Kuendesha mafunzo siku 2 kwa madiwani 27 juu ya mfumo wa Uandaaji wa mipango na bajeti za miradi ya maendeleo.

• Kufanya ufuatiliaji na tathimini shirikishi ya mradi


Wawakilishi wa AZAKi 70 wa Wilaya ya Liwale wamejengewa uwezo kuhusu mchakato wa uandaaji mipango na bajeti ya maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kufikia 29 Februari, 2012.

Madiwani 26 wa kata 20 za Wilaya ya Liwale wamejengewa uwezo kuhusu mchakato wa uandaaji mipango na bajeti za maendeleo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na umuhimu wa ushiriki wa wananchi kufikia, 29 Februari, 2012.

Wadau 40 wa maendeleo wa kata 20 za wilaya ya Liwale wameshiriki katika zoezi la ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi kufikia 31 Machi, 2012.
Katika shughuli ya mafunzo kwa Madiwani idadi yao imepungua kutoka 27 hadi 26 kufuatia mmoja wao kufariki dunia kabla ya utekelezaji wa mradi kuanza.
Mafunzo kwa Asasi za Kiraia kuhusu mchakato wa uandaaji mipango na bajeti za maendeleo katika Serikali za Mitaa (TZS. 9,262,500/=)

Mafunzo kwa Madiwani kuhusu mchakato wa uandaaji mipango na bajeti za maendeleo katika Serikali za Mitaa (TZS. 4,238,000/=)

Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya maendeleo ya utekelezaji wa mradi (TZS 1,009,950/=).

Project Outcomes and Impact

• Viongozi wa AZAKI 70 watakuwa wamepata mafunzo juu ya uandaaji wa mipango na bajeti ya miradi ya maendeleo ifikapo Disemba 2012.

• Madiwa 27 toka kata 20 Wilayani Liwale watapata mafunzo juu ya wajibu wao na mfumo wa uandaaji wa mipango na bajeti ifikapo Disemba 2012.

• Kuongezeka na kuimarika kwa amasa ya ushiriki kwa jamii katika kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathimini miradi ya maendeleo
Wawakilishi 70 wa AZAKI wameongezewa ufahamu juu ya umuhimu na ushiriki wao katika mchakato ya uandaaji wa mipango na Bajeti za maendeleo tofauti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Madiwani 26 wamepatiwa mafunzo na kuongezewa uelewa juu ya haki na wajibu wao wa kusimamia uibuaji, upangaji, utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini shiriki wananchi katika michakato ya mipango na bajeti za maendeleo za Serikali za Mitaa

Kuongezeka kwa ari ya uwajibikaji kwa AZAKi katika kuhamasisha jamii kushiriki kikamilifu katika michakato ya uandaaji, utekelezaji, ufufuatiliaji na kutathmini ya ubora na kiwango cha utekelezaji wa miradi husika katika maeneo yao.

Kuboreka kwa mahusiano na ushirikiano wa kimaendeleo baina ya AZAKI na Viongozi na Watendaji wa Halmashauri ngazi ya; Mitaa, Vitongoji, Vijiji na Kata katika kubaini mafanikio yaliyopatikana na kuyadumisha, changamoto zilizopo na kushauriana namna ya kukabiliana nazo kabla hazijaleta athari na/au kupunguza taathira zake.

Kuibuliwa kwa Mipango Kazi ya AZAKi na Madiwani ambayo inabainisha mambo yatakayofanyika kwa kila kundi baada ya kumalizika kwa mafunzo. (Angalia viambatanisho vya taarifa hii). Shughuli walizobainisha ni pamoja na:-

Kutoa mrejesho wa mafunzo kwa viongozi na wajumbe wa Asasi.

Kuksanya taarifa mbalimbali juu ya utawala bora katika mamlaka za
serikali za mitaa.

Kuchambua taarifa za utawala bora zilizokusanywa katika mamlaka za serikali za mitaa.
kuhudhuria katika mikutano na vikao mbalimbali yaserikali za mitaa ngazi ya mtaa, vitongoji, vijiji, kamati ya maendeleo ya kata(WDCS), Baraza la madiwani na kamati ya ushauri yaa Wilaya (DCCS).

Kushiriki katika uandaaji wa mipango na bajeti ya miradi ya maendeleo katika serikali za mitaa.

Kuandaa na kutuma maandiko miradi juu ya utawala bora na uwajibvikaji katika ngazi za jamii kwa wafadhili mbalimbali ikiwamo (FCS).

Kimsingi, uelewa huo wa AZAKI juu ya umuhimu wa kushiriki katika michakato ya uandaaji wa mipango na bajeti za maendeleo katika Serikali za Mitaa umetokana na utekelezaji wa shughuli za mradi huu uliofadhiliwa na The foundation for Vicil Society.

Pia kumefunguliwa ukurasa mpya wa ushirikiano na mahusiano kati ya AZAKI na Madiwani katika maeneo yao kuhusu kushiriki na kushirikishana katika michakato ya maendeleo tofauti na hali iliyokuwepo awali ambayo baadhi ya Madiwani wamekiri uwepo wa Asasi za kiraia kwenye maeneo yao isipokuwa hawakutambua umuhimu na wajibu wa Asasi hizo katika kuchangia kuchochea na kuleta ufanisi wa kimaendeleo. Madiwani wameahidi kutoa ushirikiano kwa Asasi za kiraia kwa kuwashirikisha kwenye vikao vya WDCs na maeneo mengine muhimu ya kimaendeleo.

Asasi za Kiraia kujitambua uwepo wao na fursa walizonazo katika kuchangia ufanisi wa michakato mbalimbali ya mipango kwa mujibu wa mifumo ya mamlaka za serikali za mitaa mfano.
Asasi za Kiraia hadi mwisho wa semina kwa makundi yote zimeonyesha uelewa wao namna ya kuchangia ufanisi wa mipango na bajeti na hivyo kuahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa Serikali za Mitaa ngazi za; Mitaa, Vitongoji, Vijiji na Kata ili kuhakikisha miradi yenye tija kwa wananchi inaibuliwa pamoja na kuboresha dhana ya utawala bora na uwajibikaji katika maendeleo kwa kuandika na kuwasilisha maandiko miradi kwa wafadhili mbalimbali.
Umahiri, ustadi na uzoefu wa mwezeshaji katika kufanya uwezeshaji shirikishi

Lessons Learned

Explanation
Serikali za Mitaa hazizingatii utaratibu wa kuibua miradi ya maendeleo kwa wananchi kwa kutumia Fursa na Vikwazo vya Maendeleo (O & OD) badala yake wananchi hushirikishwa kinadharia lakini bado utaratibu unatoa fursa kwa wataalamu wa Halmashauri kupanga kwa niaba ya wananchi (TOPDOWN) katika uteuzi wa miradi ambayo inakusudiwa kupelekewa kwa wanajamii katika maeneo yao. mfano wa hii ni pale mshiriki Bi Bora Makubui alipochangia juu ya hili kuwa kijiji cha Mungurumo walikuwa na kipaumbele cha ujenzi wa chumba cha darasa badala yake waliona unaletwa mradi wa ukarabati wa machinjio ya Nguruwe tena haukuwa kwenye ndoto yao na utekeleza haukushirikisha Halmashauri ya kijiji mradi ulisimamiwa na Uongozi wa Halmashauri hadi ukarabati huo uliishia.
Vikao vya Kamati ya Wataalamu ya Halmashauri (CMT) havizingatii vipaumbele vya miradi inayowasilishwa kutoka kwa Wananchi badala yake wao hufumua upya miradi yote na kuweka vipaumbele vingine kwa utashi wao ambavyo vinaleta mapokeo na matokeo mabaya na kwa kufanya hivyo miradi inayopata fedha haiungwi mkono na wananchi na hivyo kukosa ubora na tija kwa walengwa
Ufahamu mdogo wa madiwani juu ya uibuaji wa miradi kwa kutumia dhana shirikishi ya O & OD hutoa mwanya kwa watalamu wa Halmashauri kupanga miradi ya maendeleo kwa niaba ya wananchi pengine tofauti kabisa na vipaumbele walivyoainisha.
Wananchi wengi bado wana uelewa mdogo juu ya wajibu na haki yao ya kushiriki katika vikao na mikutano mbalimbali ya kisheria katika maeneo yao na hivyo hupelekea maamuzi mengi kufanya na watu wachache
Katika Kata nyingi na vijiji hakuna Benki ya miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa katika miaka iliyopita hivyo kupelekea kutofahamu taarifa za miradi iliyokwishatekelezwa na kiwango cha mafanikio yaliyopatikana
Wananchi wengi hawashiriki katika miradi na shughuli za maendeleo kwa kuwa wamekata tamaa kutokana na miradi mingi iliyokwisha kutekelezwa kutokidhi ubora, haja na mahitaji yao.

Challenges

ChallengeHow it was overcome
Waheshimiwa madiwani kudai posho walipwe kwa viwango vya Halmashauri ya Wilaya husika tofauti na bajeti ya mradi ilivyopangwa na kupitishwa.Mratibu alijitahidi kuelezea hali halisi ya mifumo na Miongozo ya wafadhili tofauti na utofauti wa viwango vya posho ukilinganisha na mamlaka za serikali za mitaa.

Aidha aliwaomba na kuwasisitizia wakiwa wawakilishi wanapaswa kufanya kazi na wadau mbalimbali ikiwamo AZAKI bila kujali kiwango cha posho kinacholipwa.

Waheshimiwa Wadiwani waliridhia maelezo hayo na mafunzo yaliendela.
Kutotengwa kwa bajeti ya kugharamia waandishi wa habari wakati wa matukio ya utekelezaji wa shughuli za mradiKuomba kuidhinishiwa kufanya mabadiliko ya matumizi ya fedha za kifungu 1.7 baada ya kupitia upya bajeti na kubaini kuwepo zidifu ya fedha katika shughuli no 1.7 kutokana na hesabu kukosewa ambayo ni posho ya washiriki 74@10,000xsiku 3 =2,960,000/= badala ya usahihi wake wa 2,220,000/= hivyo kulikuwa na zidifu ya 740,000= ambayo tulitoa taarifa kwa msimamizi na kuturuhusu tutumie kuwalipa waandishi wa habari wawili kutoka Lindi (Magazeti na Radio)
Washiriki wa mafunzo kutoka AZAKi kudai posho za kujikimu na malazi ni ndogo ikilinganishwa na hali ya ugumu wa maisha ilivyo sasa.Kuwaelimisha na kuwahamasisha kwamba malipo yote yanafanyika kwa mujibu wa bajeti iliyopitishwa katika makubaliano kati ya FCS na ULIDINGO
Kukatika katika kwa nishati ya umeme wakati wa maandali na uendeshaji wa mafunzo hali iliyopekea baadhi ya maandalizi kutokamilika kwa wakati muafakaKutumia huduma za wafanya biashara ya kupiga chapa na kurudufu nyaraka wa kujitegemea ambao huwa na majenereta madogo ya kufua umeme ili kuhakikisha maandali yanafanyika na kukamilika kwa wakati hatimaye kufanikisha uendeshaji wa mafunzo

Linkages

StakeholderHow you worked with them
Mkuu wa WilayaKufanya ufunguzi rasmi wa mafunzo na kutoa nasaha kwa washiriki ili kuhakikisha kwamba wanazingatia maarifa na stadi watakazopatiwa
Mkurugenzi Mtendaji (W)Kupata ushauri wa namna ya kuleta ufanisi wa mafunzo ikiwa ni pamoja na kuwahimiza madiwani kuhakikisha wanashiriki mafunzo kikamilifu
Asasi (AZAKi) wanachama wa ULIDINGOKusimamia uteuzi wa wawakilishi wawili walioshiriki mafunzo ya kujenga uwezo kwa viongozi wa Asasi juu ya umuhimu wa ushiriki wao katika michakato ya uandaaji mipango na bajeti mamlaka za zerikali za mitaa
Waandishi wa HabariKuhudhuria mafunzo na kuchukua taarifa za mradi na kuhabarisha wananchi ndani ya wilaya na kwingineko
Afisa Maendeleo ya Jamii (W)Kuongozana na Kaimu Mkuu wa Wilaya - Liwale wakati wa Ufunguzi rasmi wa Mafunzo kwa wawakilishi wa AZAKi.

Future Plans

Activities Planned1st Month2nd Month3rd Month
Kuendesha mafunzo kwa Watendaji wa vijiji&kata 96 kwa awamu 2 ya siku 2 juu ya wajibu wao na mfumo wa uandaaji wa mipango na bajeti za miradi ya maendeleoV
Kufanya ufuatilaji wa maendeleo ya utekelezaji wa mradiVV

Beneficiaries Reached

    Direct BeneficiariesIndirect Beneficiaries
WidowsFemale1212o
Male16160
Total28172
People living with HIV/AIDSFemale110
Male110
Total220
ElderlyFemale16160
Male14140
Total30300
OrphansFemale--
Male--
Total--
ChildrenFemale--
Male--
Total--
DisabledFemale110
Male110
Total220
YouthFemale36360
Male28280
Total64640
OtherFemale660
Male550
Total11110
(No Response)

Events Attended

Type of EventWhenLessonsActions Taken
Kushiriki warsha ya upashanaji wa habari juu ya uombaji ruzuku The foundation for civil society.June 2009-Nachingwea mjini Kutambua malengo ya kuanzishwa kwa The foundation na maeneo wanayofadhili na wasiofadhili pia namna ya kuomba na muda wa kuwasilisha maombi.Kufanyia marekebisho andiko letu la PETS lililorudishwa The foundation kwa awmu mbili mfululizo na hatimaye kupata ufadhili.
Kuhudhuria mafunzo ya usimamizi wa ruzuku kwa AZAKI zilizopata ufadhili kutoka The foundation.October-2009 Dodoma mjini-Dhana ya ushirikishaji katika hatua za uandaaji wa mradi
-Bao la mantiki
-Uandishi wa taarifa utekelezaji na za kifedha
-utunzaji na uandishi kumbukumbu za fedha
umuhimu wa ufuatiliaji na tathimini ya mradi
Viongozi kwa ushirikiano wa pamoja tumesimamia mradi na kutoa ripoti kwa wakati kama ilivyokusudiwa kwa mujibu wa mkataba
Kushiriki mafunzo ya utunishaji wa mfukoMarch-2010 Mbezi beach Dar es SalaamMambo ya msingi wakati wa kuandaa mradi mfano;
Namna ya kubaini tatizo,uchambuzi wa wadau,hatua za kufuata wakati wa uchambuzi wa mti wa matatizo,Bao mantiki,uandishi wa bajeti n.k.
Kuandaa andiko jipya ambalo limepata ufadhili kutoka The foundation na limetokana na utekelezaji wa mradi uliopita
Kushirirki mafunzo ya usimamizi wa ruzuku(M&E)Desemba-2011-Mambo ya msingi wakati wa kuandaa mradi
-Namna ya kubaini tatizo
-Uchambuzi wa wadau na hatua ya kufuata wakati wa uchambuzi wa mti wa matatizo
-Bao mantiki
-Uandishi wa bajeti
-Uandishi wa taarifa ya utekelezaji na fedha
Kurekebisha baadhi ya viambatanisho ikiwamo bao mantiki,mpango kazi,mpango wa ufuatiliaji wa matokeo na hatimaye kusaini mkataba wa mradi huu wenye namba FCS/MG/3/11/110.

Attachments

« Previous responseNext response »

« Back to report