Envaya

Envaya

Wafadhili

Maeneo ya ukurasa huu yametafsiriwa toka Kiingereza kwa Kiswahili. Ona asili · Hariri tafsiri

Trust for Conservation Innovation

Kama mdhamini wa fedha katika Envaya, Mdhamini huyu anaisaidia na ataendelea kuisaidia envaya na mipango yake yote.Envaya ni mradi usiojikita katika kupata faida ulioanzishwa kisheria chini ya Trust for Conservation Innovation.kama mradi unaofadhiliwa, Envaya inalenga katika malengo yake ya programu, wakati uendeshaji wa vifaa vyake na usimamizi wa fedha zinazotumika Envaya husimamiwa na Shirika hili la "Trust for Conservation Innovation". Trust for Conservation nchini Marekani huwa linapata msamaha wa kodi kwa kupitia mwamvuli wa shirika hisani kutoka kwa shirikisho la kodi chini ya Kanuni ya 501 (c) (3).

Google Inc

Google kwa ukarimu imekuwa ikitoa msaada kwa envaya kwa kutoa ruzuku kupitia Google Inc. Pesa inayotolewa kama hisani ya Tides Foundation.Envaya hutoa zana za kiprogramu ambazo zinatumika kuyawezesha mashirika madogomadogo ya kijamii katika bara la Afrika kuwa na tovuti zao na kuunganishwa na mtandao. Envaya inaishukuru Google kwa kuendelea kujitolea katika kusaidia upatikanaji wa habari duniani kote, na ushirikiano huu ni hatua kubwa kuelekea kuunganisha ulimwengu wote katika mfumo wa dijitali.

Twaweza

Twaweza ni Shirika la kiraia la hapa nchini Tanzania ambalo linafanya kazi ya kimaendeleo katika jamii za kiraia. Twaweza inafanya kazi ya kuifanya Envaya iweze kusonga mbele katika juhudi zake za  kuleta mabadiriko katika asasi za kiraia katika nchi za Afrika Mashariki.Twaweza imetoa kwa Envaya ruzuku kwa ajili ya maendeleo zaidi na kupelekwa kwa zana za kimtandao ili kuziwezesha asasi za kijamii kuwa bora zaidi na kwa urahisi kuwasiliana, kuandaa na kushirikiana.

Digital Opportunity Trust

The Digital Opportunities Trust (DOT) imewezesha zaidi ya vijana 2,000 duniani kote kwa kufundisha matumizi bora ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Habari (ICTs). ikiwa inafanya kazi katika nchi 13, DOT imejenga mtandao mkubwa sana na viongozi wa jumuiya na mashirika. Envaya na DOT kwa sasa wanashirikiana kupeleka Envaya nchini Rwanda.

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia

Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ni shirika la umma ambalo lina wajibu wa kuratibu na kukuza utafiti na shughuli za maendeleo ya teknolojia nchini. Ni mshauri mkuu wa serikali ya Tanzania juu ya mambo yote yanayohusu sayansi na teknolojia na namna inavyotumika katika maendeleo ya jamii na uchumi wa nchi. Makao makuu ya Envaya katika Afrika yako katika jengo la COSTECH jijini Dar es Salaam, Tanzania.kwa dhati kabisa tunaishukuru COSTECH kwa msaada wao.

Foundation for Civil Society

Foundation for Civil Society (FCS) ni msingi wa kitanzania usiotegemea faida kutoka sehemu yoyote ambao unaziwezesha jamii kwa kutoa ruzuku, kuwezesha uhusiano, na kuendeleza utamaduni wa kujifunza unaoendelea katika vyama vya kiraia. FCS ni moja ya njia kubwa ya msaada kwa ajili ya mashirika ya kiraia nchini Tanzania na nia yao ni kutoa ruzuku na kusaidia juhudi za kujenga uwezo na kuimarisha mapambano ya kupunguza umaskini.

Envaya inashirikiana na FCS katika kuendeleza teknolojia ili kuzisaidia asasi za kiraia nchini Tanzania. Foundation hutoa ujuzi wa kina kwa asasi za kiraiaTanzania katika kusaidia taarifa ya maendeleo ya Envaya ya teknolojia muhimu, na inatoa uwezo wake wa kiutendaji katika Tanzania.Pia inasaidia kupeleka na kutathmini teknolojia hii sehemu husika. FCS inajumuisha teknolojia ya Envaya katika kujenga uwezo kwa asasi za kiraia Tanzania, kutambulisha mashirika kwa  Envaya, kuziwezesha asasi kujenga tovuti zao wenyewe na mawasiliano bora kwenye mtandao.

Family Giencke Trust

Trust Giencke Family ina nia katika kufanya mabadiliko katika maisha ya watu moja kwa moja kama iwezekanavyo. Trust inasaidia mashirika kama vile Mfuko wa Jimmy kwa utafiti wake wa kansa, MinutemanSenior.org kwa ajili ya kazi yao ya kutoa huduma muhimu kwa wazee na walemavu, vilevile inatoa msaada kwa Envaya katika kusaidia mashirika ya kiraia katika nchi zinazoendelea.

Peace Corps Tanzania

Peace Corps Tanzania inaisaidia Envaya katika shughuri zake za kujitolea na katika vipindi vya kutoa mafunzo kwa jami. Pamoja na wanaojitolea kote Tanzania katika elimu, afya, na sekta ya mazingira, Peace Corps Tanzania itasaidia Envaya kuendelea na kuboresha shughuri zake.