Envaya

Envaya

Kuhusu Sisi

Maeneo ya ukurasa huu yametafsiriwa toka Kiingereza, lakini tamko la Kiswahili ni la zamani. Ona asili · Hariri tafsiri

Envaya inaumba na kueneza programu ya kompyuta ili kuyawezesha na kuyaunganisha mashirika ya jumuiya ya kiraia duniani.
 

Tunaumba vifaa vinavyoyaruhusu kujenga tovuti zao wenyewe, na kutoa vifaa kwa NGOs kubwa kusaidia bidii hizi za jamii.

Usuli

Duniani kote, mashirika mengi ya jumuiya ya kiraia yanafanya kazi kuboresha jamii zao. Yanatetea mabadiliko chanya, kuhimiza utawala bora, kuendeleza mbinu mpya ya kupunguza umaskini, na kuongoza miradi mbalimbali kutoka mipango ya elimu ya VVU/UKIMWI kwa kuendesha nyumba ya yatima kwa kupanda miti.

Kama teknolojia inaenea duniani kote, mashirika zaidi na zaidi yanataka tovuti zao wenyewe ili kuwasiliana vizuri na wengine duniani. Lakini kwa watu katika nchi zinazoendelea kama Tanzania, kuunda tovuti ni vigumu.

 

Je, Envaya ni nini?

Kama mradi wa kwanza, Envaya imeanzisha envaya.org, njia rahisi kuunda tovuti ambayo imesanifiwa kwa mahitaji ya mashirika ya jumuiya ya kiraia. Asasi zinaweza kujenga na kuhariri kwa urahisi tovuti zao juu ya envaya.org, kutoa sauti yao kwa intaneti ambapo zinaweza kuandika kuhusu miradi yao na kugawa rasilimali na mawazo na mashirika mengine na watu duniani kote.

 

Mpango ya kwanza Tanzania

Mei, 2010, Envaya ilianza mpango wake wa majaribio Tanzania, ambapo umekuwa kupokelewa kwa shauku. Teknolojia ya kuweza kutumika kwa asasi ya Tanzania imepungukiwa, na tovuti mpya ya Envaya imewahi kutoa tofauti ya maana kwa kuleta asasi za kiraia kwenye intaneti. (Angalia mashirika ya mfano yanayotumia Envaya)

Kwa sasa, Envaya inatumia maoni kutoka watumiaji wake wa awali ili kuboresha programu yake na kuendelea kuhamasisha mashirika kuchapisha kwenye intaneti.

 

Mipango ya baadaye

Envaya inaendelea kufanya kazi ili kukuza programu mpya na bora kwa mashirika ya jumuiya ya kiraia, na kuanzisha tovuti ni mwanzo tu.

Hivi karibuni, Envaya inapanga kuwezesha asasi kupanga upya tovuti zao kwa kutumia simu zao za mkononi. Watu wengi Tanzania hawawezi kutumia intaneti kwa urahisi, au wanahitaji kulipa kwa kutumia internet cafe, kwa hivyo ni vigumu kwa baadhi ya mashirika na kutumia tovuti. Namba ya SMS ya bure ingeweza kuruhusu watumiaji wa Envaya kuchapisha habari na picha kwa urahisi kwa kutumia simu yake ya mkononi.

Katika miezi ijayo, Envaya inapanga kuzindua mradi wa mfumo wa taarifa ya intaneti kwa kushirikiana na Foundation for Civil Society (FCS), moja la mashirika makubwa Tanzania ya kusaidia jamii. Mashirika yanayopata kuchangia kutoka FCS yataweza kuwasilisha taarifa za mradi kielektroniki na kuchapisha taarifa zao juu ya tovuti zao za Envaya. Kikamilifu kupatikana na inayoonekana kwa wageni wa nje, mfumo huu utaboresha uwazi katika maendeleo ya kimataifa.

Katika siku za hivi karibuni, tunapanga kueneza Envaya kwa nchi nyingine katika Afrika Mashariki na duniani.

 

Sisi ni nani

Envaya ni mradi bila faida 501(c)(3) ambayo inafadhiliwa kisheria Marekani chini ya Trust for Conservation Innovation. Inaongozwa na timu ndogo ya watu kutoka Marekani, Tanzania, na Canada.

Saidia Envaya kwa kuchangia katika intaneti leo!