Envaya

Envaya

Shirikiana nasi

Maeneo ya ukurasa huu yametafsiriwa toka Kiingereza kwa Kiswahili. Ona asili · Hariri tafsiri

Ungana Nasi!

Je unataka kushiriki nasi? Wasiliana nasi kutumia info@envaya.org!

Tunatafuta watu wenye moyo watakaopenda kuchangia katika jitihada zetu za kuwezesha jamii za kiraia kwa njia ya teknolojia. Kama wewe ni mtaalamu wa maendeleo ya kimataifa au mtaalamu wa programu za kompyuta, au mtaalamu asiyetaka faida yoyote anayeweza kusaidia shirika letu kukua na kuchangia fedha ili liweze kujiendesha, tunapenda sana kusikia kutoka kwako. 

Envaya pia inaendelea kujenga ushirikiano na mashirika ya maendeleo duniani kote. Nia yetu ni kushirikiana na mashirika yenye uzoefu na kupanua kazi ya Envaya kijiografia na kiuwezo.

kutafsiri Envaya katika lugha nyingine

Utusaidie kupanua kazi yetu duniani kote kwa kuchangia kwenye ukurasa wa kuhariri (Translations site). Mtu yeyote anakaribishwa kusaidia kutafsiri Envaya katika lugha mbalimbali kwa kuchangia uhariri mpya, na kwa kupiga kura na kutoa maoni juu ya tafsiri zilizopo. Unaweza pia kutumia ukurasa wa kuhariri kusahihisha vitu vilivyotafsiriwa vibaya. Kwa maelekezo zaidi, bonyeza hapa .

Kuchangia Code

Kama wewe ni mwendeleza programu, unakaribishwa kusaidia kuboresha programu zetu kwa kuchangia kwenye code yetu!

Code ya Envaya inapatikana katika Github saa youngj / Envaya . Kuna project ndogo ndogo ambazo softeare developers wanaweza kufanyia kwazi; zinapatikana kwenye : masuala ya ukurasa Github .

Code ya Envaya (isipokua baadhi yao) inaleseni chini ya open-source MIT License. Kwa kuanzia tutafute kwenye Github!