Respondent: | Promotion of Education Link Organisation (PELO) |
---|---|
Time Submitted: | 29 Januari, 2012 22:42 EAT |
Mtaa: mabibo relini
Tulikuwa na kivuko cha kuvukia kwenda reline kupanda mabasi ambacho kimesombwa na mafuriko.Kipo kivuko kidogo tu cha muda ambacho hata mvua ya kawaida itakaponyesha kitamezwa.Bado hata bila masika kwa udongo kilionao asubuhi tunapanga foleni kupita katika kivuko hiki kwa udogo kilionao.Serikali itusaidie kutengeneza kivuko kama kilichosombwa na mafuriko.
Kama unavyoona narudia kujenga upya karibu nusu ya nyumba yangu iliyobomolewa na mafuriko
Mmomonyoko huu wa udongo ambao umepanua kingo za mto huu ni tishio kwa makazi yetu.Wadau wa mazingira waangalie namna ya kutusaidia kukabiliana na mmomonyoko huu.
Wake zetu walipata shida ya kutafuta maji ya bomba nyakati za mafuriko.Kidogo naona kuna unafuu kwa wakati huu.Hiki nadhani ni kiashiria kwamba vyanzo vya maji viliathiriwa na mafuriko.Yawezekana serikali imechukua hatua.Ila bila hata mafuriko,mabibo maji ya bomba ni tatizo.
Kabla ya mafuriko: Dakika 40 | Sasa: Dakika 40 |

Sehemu ya nyumba katika mtaa wa mabibo relini iliyoathiriwa na mafuriko ambayo ilibomolewa na mafuriko huku makazi yakiendelea kukabiliwa na changamoto ya mmomonyoko wa udongo katika kingo za mto

Haya ni masalia ya daraja lililokuwa likitegemewa sana na wakati wa mabibo relini wanapokwenda kupanda mabasi ya kwenda tabata,ubungo na buguruni.Kwa sasa kuna daraja la muda ambalo wakati wa masika halitaweza kuwasaidia.Angalia picha zinazofuata utaona daraja la muda lilivyo.
« Rudi nyuma kwenye ripoti