Envaya

Envaya

Dar es Salaam Flooding Community Survey

Respondent: Promotion of Education Link Organisation (PELO)
Time Submitted: January 29, 2012 at 10:10 PM EAT
mabibo bondeni

Siku zote mabibo maji ya bomba ni tatizo.Maji ya uhakika ni ya kununua kwa wanaotembeza kwenye mikokoteni ambayo ni ya chumvi.
Choo cha nyumba yangu vimesombwa na maji,kwa sasa tunajisaidia nyumba ya jirani.
Kama unavyoona nyumba yangu iko kwenye hatari ya kubomoka kama mvua za masika zijazo zitakuwa kubwa.Tunajitahidi kuweka magunia ya michanga kuzuia mmomonyoko wa udongo uliosababishwa na mafuriko usiendelee lakini uwezo sina wa kugharimia kununua kokoto kuudhibiti mmomonyoko kama inavyofanya kampuni ya AMI pale mabibo relini.
Sielewi kama vimepata athari au la kwa kuwa maji ya mabomba yanatoka kwa nadra toka hata kabla ya mafuriko.Labda wanawake ambao ni wachotaji maji wanaweza kugundua kama kuna athari.
Before flooding: Saa moja Now: Saa moja
Hizi ni baadhi ya nyumba jirani za eneo la mabibo bondeni zilizobomolewa na mafuriko.Wakazi wanajitahidi kuweka kifusi kilichoko katika magunia kuzuia tishio la kuharibika zaiidi kwa nyumba zao mara masika yanapoanza.
Hizi ni baadhi ya nyumba zilizonusulika kusomba na maji katika eneo la mabibo bondeni.Mmomonyoko wa udongo uliochochewa na mafuriko umezidi kupanua kingo za mto na kufanya wakazi wanaoishi kando ya mto kuwa katika hatari ya makazi pindi mvua za masika zitakapoanza kunyesha.
« Previous responseNext response »

« Back to report